Kipi kimezikumba hizi biashara za hawa macelebrity

Business ni strategy biashara sio sawa na umaarufu. Ukiwa maarufu ukailewa biashara inataka nini una advantage kuliko unaoshindana nao kibiashara. Tatizo celebrities wetu wanaleta first world businesses katika mazingira ya third world wakidhani wanaweza tusua kutumia majina yao pasi ya kujua in first world kuna middle class ya kutosha, huku kwetu makapuku ndio wengi. Wabongo wengi hatujafikia level kununua brand tunafanya manunuzi kukidhi mahitaji, ya mini ninunue mofaya 4000 wakati kuna Mo Energy drink 500, au Chibu Perfume wakati kuna vidude vya buku 5 tu sinuki jasho.
 
True
 
Kwenye FYN By Falsafa umebugi, inauzika mtaani kama njugu!
 
Uko sahihi
 
Ndio maana makampuni kama ya kina Bahkresa au sijui Mo wao wana target bidhaa za lazima kwa kila family utanunua tu unga sijui mikate au mafuta muhimu huwezi kuingia nyumba hawatumii bidhaa yao moja. Sasa wewe unakuja na perfume kitu ni kama luxury hakina umuhimu wowote nani atanunua na maisha yenyewe haya. Hakuna akili za kibishara wale wahindi wauza sekera na chips tu wanapiga pesa sababu utakula tu ni lazima.
 


Nikuongezee na Juma Jux na Tshit zile za African boy
 
Sio lazima uuze bidhaa ya lazima ndio biashara iende mfano Makjuice zile juisi ni lazima, kuna mwengine anauza uji Happap ni lazima, Energy drink kama mofaya inafanya vizuri SA na Africa sio bidhaa ya lazima, Jux mavazi yake ya African boy sio lazima nk
 
Jamani katika wasanii Diamond ndio mjasiriamali/mfanyabiashara namba moja tatizo munaangalia wazalisha bidhaa sio watoa huduma...kampuni ya WCB na wasafi media ni millions company.
 
Umenikumbusha p diddy aliintroduce kinywaji chake Nigeria akaishia kula za uso. Eti chupa moja anauza dola 40 halaf kinywaji chenyewe ni maji tu yenye ladha ya nazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…