Dellaboss perfume ya Hajji manara hii aliizindua kwa mbwembwe zote huyu msemaji wetu wana msimbazi. Lakini sasa kimyaa hata mwaka haijamaliza.
Mofaya ya Alikiba, hii ni kama sijui kufata mkumbo maana tangu aizindue sikuwahi kukutana nayo kokote.([emoji3]sijui ndio kusema hapendi show off)
Chibu perfume ya Diamond. Hii nayo sioni chochote kikiendelea. Ila walio wahi kuitumia wanasema ni ya kawaida sana na bei ni kubwa mno(bei haiendani na bidhaa ni kama alikuwa anauzia jina)
Fynebyfalsafa ya Hamisi Mwijuma (mwana F.A), hii nayo naona kama haina maisha marefu maana hata promotion imepungua sana.
Mnaweza kuongezea biashara zingine za hawa ndugu zetu zilizokufa kifo cha mende.
Je, huwa wanakwama wapi labda?