Kipi kinaanza Mema / Wema au Imani / Mungu

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Najiuliza kwa mukstakabari wa Afya ya Jamii na Amani kipi kinatakiwa kiwe Kipimo cha Matendo ya Wanajamii kuyafanya Imani yao inavyowatuma (bila kuangalia matokeo) au Matokeo (yaani wanachofanya kuhakikisha hakiumizi yoyote) hata kama kinaendana tofauti na Imani yao ?

Hata Kama Imani hio ni ya wengi je inamaanisha hata wale wachache wanaobaki waumie ili hao wengi waridhishe Mungu / Imani yao ?

After all Kama Simba Wawili na Binadamu mmoja wakisema wapige Kura ya Chakula cha Kula, Binadamu lazima ndio atakuwa Kitoweo....
 
Kabla ya yote kinachoanza ni Imani,

Imani inaweza ikatafsirika kwa tafsiri mbali mbali ila imani ninayoiongelea hapa ni Imani "Kuamini" ya ile hali ya huruma,kuthamini watu au kitu chochote kile hata kama sio chako basi hutakiwi kukiharibu,

Unapokua na imani ndipo matendo mema hufuata halafu ndipo huja ile hofu ya Mungu,unaweza kua na imani hata kama hauna dini unayo iamini.
 
Kabla ya yote kinachoanza ni Imani,
Kipi kinaanza (take precedence) wema / mema au Imani ?

Kuna kitabu cha Imani kuna mtu aliambiwa amtoe mwanae wa pekee sadaka na alikuwa tayari kufanya lile tendo (ndio swali langu linakuja ni sawa afanye tendo hilo sababu ya Imani yake kubwa au alipinge mara moja sababu linaumiza mwingine) ?

Kuna watu wanaumiza wenzao sababu Imani yao ni kwamba ndio wanatenda jema; kuna watu wanapigia kelele wenzao kwa kuabudu; kuna watu wanawashika wengine miezi fulani wakitaka kula au wakila barabarani sababu kwa imani yao wanatenda dhambi; kuna wengine wanapinga wengine wasinywe kilaji (the list is endless); Hata zamani kuna wale waliozikwa na wafalme ili wawatumike huko wafalme wanapoenda
Imani inaweza ikatafsirika kwa tafsiri mbali mbali ila imani ninayoiongelea hapa ni Imani "Kuamini" ya ile hali ya huruma,kuthamini watu au kitu chochote kile hata kama sio chako basi hutakiwi kukiharibu,
Unless wewe ni Rastafarian nadhani utakubaliana nami kwamba sio kweli Imani zote zinatoa Huruma kwa kila Kiumbe; Hukumu imekuwa ni jambo la kawaida kwenye Imani nyingi....; Unless unataka kuniambia yote yanayoaminiwa ni Mema...., Je wale wanaotenga / harass wengine kwa mgongo wa Mapepo sijui utawaweka kundi gani (Je wanawahurumia mapepo)?
Unapokua na imani ndipo matendo mema hufuata halafu ndipo huja ile hofu ya Mungu,unaweza kua na imani hata kama hauna dini unayo iamini.
Usipokuwa na Imani hautendi Mema ?; Imani ni nini Huwezi kusema wasioamini hizi Imani nao wanaamini (Hapo tutakuwa petty na tunaingia kwenye Semantics) swali langu ndio maani limesema Imani / Mungu
 
Unaanza wema kwa mtu aliye na akili timamu. Imani yaweza kuwa hata ya ukatili kuua wasiokuunga mkono kama wayahudi na waislamu pasipo wema.

Wema unahusisha akili wakati imani ni upumbavu
 
Na nadhani watu wakiwa Wema Jamii itanufaika zaidi Yaani ni bora kuwa na wapagani Wema kuliko Religious Fanatics, ...; Kwa jicho la AMANI na Utulivu....
 
Kipi kinaanza (take precedence) wema / mema au Imani ?

Kuna kitabu cha Imani kuna mtu aliambiwa amtoe mwanae wa pekee sadaka na alikuwa tayari kufanya lile tendo (ndio swali langu linakuja ni sawa afanye tendo hilo sababu ya Imani yake kubwa au alipinge mara moja sababu linaumiza mwingine) ?

Kuna watu wanaumiza wenzao sababu Imani yao ni kwamba ndio wanatenda jema; kuna watu wanapigia kelele wenzao kwa kuabudu; kuna watu wanawashika wengine miezi fulani wakitaka kula au wakila barabarani sababu kwa imani yao wanatenda dhambi; kuna wengine wanapinga wengine wasinywe kilaji (the list is endless); Hata zamani kuna wale waliozikwa na wafalme ili wawatumike huko wafalme wanapoenda

Unless wewe ni Rastafarian nadhani utakubaliana nami kwamba sio kweli Imani zote zinatoa Huruma kwa kila Kiumbe; Hukumu imekuwa ni jambo la kawaida kwenye Imani nyingi....; Unless unataka kuniambia yote yanayoaminiwa ni Mema...., Je wale wanaotenga / harass wengine kwa mgongo wa Mapepo sijui utawaweka kundi gani (Je wanawahurumia mapepo)?

Usipokuwa na Imani hautendi Mema ?; Imani ni nini Huwezi kusema wasioamini hizi Imani nao wanaamini (Hapo tutakuwa petty na tunaingia kwenye Semantics) swali langu ndio maani limesema Imani / Mungu
Unachanganya mambo mengi sana mpaka unakua hueleweki,halafu ni kama vile umeshajikoki kubishana,

Ngoja nikuache.
 
Imani huleta wema
Naweza ninakupa Mifano isiyo na Mwisho ambayo Imani ya baadhi ya watu haijaleta Wema...; labda kabla sijafika mbali nikuulize Imani ni Nini ? (Wewe kama wewe unavyoitafsiri kwenye muktadha huu)
 
Sawa
 
Najiuliza kwa mukstakabari wa Afya ya Jamii na Amani kipi kinatakiwa kiwe Kipimo cha Matendo ya Wanajamii kuyafanya Imani yao inavyowatuma (bila kuangalia matokeo) au Matokeo (yaani wanachofanya kuhakikisha hakiumizi yoyote) hata kama kinaendana tofauti na Imani yao ?

Hata Kama Imani hio ni ya wengi je inamaanisha hata wale wachache wanaobaki waumie ili hao wengi waridhishe Mungu / Imani yao ?

After all Kama Simba Wawili na Binadamu mmoja wakisema wapige Kura ya Chakula cha Kula, Binadamu lazima ndio atakuwa Kitoweo....
Kipimo ni wema na si Imani. Jamii yenye wema, ni Bora zaidi kuliko yenye Imani tu, na hasa Imani inapokuwa potofu, hakuna wema potofu.
 
Wakati kuna watu wanaamini kwamba kuua wenzao na kuchukua viongo vyao ndio chanzo cha mafanikio yao nachelea kusema Wema ndio kila kitu hata kama kinaendana tofauti na Imani.......

Mfano Ibrahim alivyoambiwa amchinje mwanae angesema mhh hapo utanisamehe hii inakwenda tofauti na kutenda wema
 
Naweza ninakupa Mifano isiyo na Mwisho ambayo Imani ya baadhi ya watu haijaleta Wema...; labda kabla sijafika mbali nikuulize Imani ni Nini ? (Wewe kama wewe unavyoitafsiri kwenye muktadha huu)
Naomba unipe mifano kwenye biblia
 
Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za
malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba
iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na
unabii, na kujua siri zote na maarifa yote,
nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza
kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu
mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha
maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue
moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.

1 Kor 13:1-3
 
Naomba unipe mifano kwenye biblia
Kabla sijaingia deep naomba nikupe mzizi wa fitina...

Dini nyingi hazivumilii haki ya dini nyingine kuwepo - kwamba sisi tupo sawa wale wanakosea. Kwa muktadha huo mifarakano mingi imetokea kwa madai ya ukandamizaji wa kidini au kwa sababu ya ukandamizaji halisi wa kidini.

Unapoamini kwamba wewe ndio chaguo na inakupa justification fulani kufanya mambo ambayo sio mema kwa mwenzako ni kuparaganyisha jamii (mfano Kina Musa walivyoamini wao ndio watu wa Mungu na Mungu kutoa mapigo kwa wale wengine.., Je wale walikuwa watu wa nani na inaleta precedent gani katika kuwaadhibu watu tena mbaya zaidi kuna pigo lililopiga kila mzaliwa wa kwanza) Je hii kama mafundisho kwa wanajamii tunawafundisha nini ? Au tunawapa loopholes za kuwa watu wa visasi na ghadhabu ?

Dini nyingi kiuhalisia zinatangaza amani kwa watu wa imani zao wengine wote wanawaona kama uchafu utakaokwenda motoni; kwangu mimi hii haina tofauti na wapiga ramli wanaotwambia kwamba huenda bibi yako au shagazi yako ndio amekuloga....
 
Nadhani kuuliza swali kirahisi zaidi labda niseme Kuhubiri Wema / Upendo ni sawa na kuhubiri Injili / Dini Imani ?

Yaani nikishakuwa wa Imani fulani na kufuata yale ya kwenye Imani automatically nakuwa mtenda wema kwa jamii nzima ? (kwa waumini na sio waumini)?
 
Well said lakini hapokuna loophole kama siambiwi nimpende shetani pia na kuna uwezekano wale ambao sikubaliani nao nikaona ni watumishi wa Shetani hivyo kuwatenda au kutokuishi nao kwa karibu na kuwanyima hata undugu (wanapokuja kutaka kuoa kwangu au wakipendana na watoto wangu kuwakataza wasiwe ndugu)...., Je huo ndio Upendo ?
 
Kabla sijaingia deep naomba nikupe mzizi wa fitina...

Dini nyingi hazivumilii haki ya dini nyingine kuwepo - kwamba sisi tupo sawa wale wanakosea. Kwa muktadha huo mifarakano mingi imetokea kwa madai ya ukandamizaji wa kidini au kwa sababu ya ukandamizaji halisi wa kidini.

Unapoamini kwamba wewe ndio chaguo na inakupa justification fulani kufanya mambo ambayo sio mema kwa mwenzako ni kuparaganyisha jamii (mfano Kina Musa walivyoamini wao ndio watu wa Mungu na Mungu kutoa mapigo kwa wale wengine.., Je wale walikuwa watu wa nani na inaleta precedent gani katika kuwaadhibu watu tena mbaya zaidi kuna pigo lililopiga kila mzaliwa wa kwanza) Je hii kama mafundisho kwa wanajamii tunawafundisha nini ? Au tunawapa loopholes za kuwa watu wa visasi na ghadhabu ?

Dini nyingi kiuhalisia zinatangaza amani kwa watu wa imani zao wengine wote wanawaona kama uchafu utakaokwenda motoni; kwangu mimi hii haina tofauti na wapiga ramli wanaotwambia kwamba huenda bibi yako au shagazi yako ndio amekuloga....
Kaka nimekuelewa!! Sana
Nitakuuliza swali wewe je ni bora umependeze Mungu au Mwanadamu?
 
Nadhani kuuliza swali kirahisi zaidi labda niseme Kuhubiri Wema / Upendo ni sawa na kuhubiri Injili / Dini Imani ?

Yaani nikishakuwa wa Imani fulani na kufuata yale ya kwenye Imani automatically nakuwa mtenda wema kwa jamii nzima ? (kwa waumini na sio waumini)?
Ndio ni sawa
Chemuchemu ya kwanza ya moyo ni imani .
Kila kitu tunafanya kwa imani hata matendo mabaya na mema yote
 
Kaka nimekuelewa!! Sana
Nitakuuliza swali wewe je ni bora umependeze Mungu au Mwanadamu?
Mungu yupi ? Sababu tukiangalia kwa haraka haraka kuna Mungu tofauti kulingana na Imani za watu tofauti..., Mimi hapa naweza kuwa nina Mungu wangu ambaye anataka nitoe kafara watumwa au watoto wanaozaliwa na kilema..., sasa hapo ni bora nimpendeze huyo Mungu ? (As far as Kilema is concerned jibu ni hapana)

Kwa kujibu swali lako ni kwamba binafsi naona kwa jamii yenye afya tunapaswa kutomtendea mwanadamu yoyote jambo ambalo linaweza kumuumiza hatuwezi kuishi kwa kupendezana sababu kinachokupendeza wewe huenda kikawa ni sumu kwa mwingine (Ukifanya mema kwa kila anayekuzunguka ni bora hata ukiwa mpagani kuliko yule anayeamini Imani fulani inayopelekea kuniletea mimi Shida)
 
Ndio ni sawa
Chemuchemu ya kwanza ya moyo ni imani .
Kila kitu tunafanya kwa imani hata matendo mabaya na mema yote
Okay kwahio unakubali kwamba kuna imani ambazo zinaleta matendo mabaya (be it ni Imani Potofu or Otherwise) na sababu ni Imani huenda wewe ukadhani upo sawa kumbe umepotoka (its all good to each their own)..., ila kupotoka kwako kunaweza kukawa ni hasara na hatari kwa jamii...

Hivyo conclusion ni kwamba ni bora kitu ambacho tuna uhakika nacho ambacho ni wema tukaendelea nacho kuliko kile ambacho hatuna uhakika na kinaweza kuleta madhara
 
Back
Top Bottom