Kipi kinamfelisha msanii Ruby kuendelea kufanya vizuri katika muziki?

Intelligent businessman

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
31,913
Reaction score
65,514
Ruby, moja ya wasanii wenye vipaji vikubwa katika muziki, kuanzia sauti mpaka uwasilishaji wake lazima vitakuvutia.

πŸ‘‰ Nyimbo kama Jela, Yule na Forever ni moja ya hits pendwa, ambazo zimeendelea kumpa sifa au kuuonyesha ubora wake.
πŸ‘‰ Nimejiuliza kipi kinachomfanya asiendelee kuwika katika zama hizi za streams? Maana wenzie kama Nandy, Zuchu, Maua Sama na sasa Phina wanazidi kumuacha mbali.

Boomplay streams;
~ Nandy 50M+
~ Zuchu 50M+
~ Sama 25M+
~ Ruby 5MπŸ™‰

Je shida au tatizo ni Menejimenti mbovu, nidhamu mbovu, au kakosa vichwa vyenye madini kama kina Ruge?



 
Ruby anaponzwa na dharau,majivuno,kiburi,kujiamini kulikopitiliza,sifa na kujitenga..
Hakuna management itaweka hela kwa ruby,kana kiburi sana.

Yani ruby na baraka da prince hawatakuja sainiwa kwenye lebo yoyote ile hapa africa...
 
"Ruby aligombana na mawingu ndio waka m'boost mchumba wa ruge Nandy" alisikika mpita njia
 
Muziki kwa watoto Wa kike unachangamoto Sana. Wanalazimika kutumika kibaba na mama ndio promo iwepo. Sasa Ruby Hana trakoo, mabraza wanaona hailipi. Pili huyu Dada Alisha kuwa labeled kama mkorofi, Hana nidhamu, jeuri, kibri, mshari na mwenye kuparamia yeyote kwa kifujo. Kupitia hivyo anakosa endorsement
 
Tatizo linajulikana,
Ni akiwa stejini hatumuoni, tunamhisi tu.
Aongeze nyama bana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…