Kipi kitabu cha Mungu kwa wakati wetu huu kati ya Bibilia na Qur'an?

Vitabu ni vi4
Taurat- Mussa a.s
Zaburi- Daud A.s
Injili- Issa Bin Maryam
Qur' an - Muhammad (s.a.w)
Hapo nahisi ushapata jibu lako
 
Mkuu nimecheka sana hii mh! 🤣
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Wacha we!
 
Mungu hana kitabu cha kuabudiwa... Vitabu vyote ni maandiko ya wanadamu.
 
vitabu vyote vina mazuri ya kujifunza , ni vile tu ubongo wako utavyochukua unavyoona vitakufaa.
 
Iv ulichoandika umekielewa kweli kwanza umesema QUR'AN NI COPY YA BIBLIA

Hapo hapo tena ukaanza kutoa tofaut ya vitu ambavyo vipo kwenye biblia kwenye Quran hakuna au vipo lakin viko tofaut

Halafu unasema copy iv hunajua maana ya copy kweli we baba wa watu!!
 
Kwa hiyo yehova alizaa?? Duh
 
Ohh yes..... Qur'an is a really copy, kama tu bidhaa za Mohamed Enterprises
 
Vitabu vyote hivyo vimeongea uongo mkuu. Ni hadithi za watoto
 
Quran ni COPY ya biblia ila Yehova na Allah ni vitu viwili TOFAUTI
umeelewa ulichokiandika?
yaani Quran imekopi vitu vyote kwenye biblia ila imeshindwa kumkopy Yehova ?
 
Mosi,Mungu wa Biblia na quran ni just theory/Hayupo,Pili vitabu vyote viwili vinamapungufu/makosa lukuki ya kihistoria,Kimantiki na Kiuandishi na pia Vinachuki,Mauaji,Ujinga wa kiwango kikubwa...
Umeongea fact tupu
 
mungu wa wapi huyo amabye alishwahi kuwa na vitabu? Mungu pekee ndiyo ana vitabu, miungu hawana vitabu na kama wanavyo basi havijulikana na tulio wengi
 
Mosi,Mungu wa Biblia na quran ni just theory/Hayupo,Pili vitabu vyote viwili vinamapungufu/makosa lukuki ya kihistoria,Kimantiki na Kiuandishi na pia Vinachuki,Mauaji,Ujinga wa kiwango kikubwa...
Una kipi cha hekima kutueleza ndugu? Naona hoja yako imejaa ujinga ambao wewe unadhani ni hekima. Lete hoja tukujibu sawasawa ili usijejiona mwenye hekima machoni pako:

Mithali 26 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁴ Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Usije ukafanana naye.
⁵ Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake.
 
Katika Uislamu tumefundishwa kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha vitabu vinne (4) ambavo ni
i) Taurati aliyopewa Nabii Musa (A.S)
ii) Zaburi alipewa Nabii Daudi (AS)
iii) Injili aliyopewa Nabii Issa (AS)
iv) Quran aliyopewa Nabii Muhammad (S.AW)

Kila muislamu ni lazima aamini Mitume waliokuja zamani pamoja na vitabu vyao bila kubagua hata mmoja kati yao.


QURAN 3:2-4

2. Mwenyezi Mungu, hakuna Mungu ila Yeye Aliye Hai, Msimamizi wa yote milele.


3. Amekuteremshia Kitabu kwa haki, kinacho thibitisha yaliyo kuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili

4. Kabla yake, ziwe uwongofu kwa watu. Na akateremsha Quran . Hakika walio zikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu watakuwa na adhabu kali. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye kulipa.
'

QURAN 4: 136
136. Enyi mlio amini! Muaminini Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Kitabu alicho kiteremsha juu ya Mtume wake, na Kitabu alicho kiteremsha kabla yake. Na anaye mkataa Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya mwisho, basi huyo amekwisha potelea mbali.
136

QURAN 3; 84
84. Sema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na tuliyo teremshiwa sisi, na aliyo teremshiwa Ibrahim, na Ismail, na Is-haka na Yakubu na wajukuu zao, na aliyo pewa Musa na Isa na Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi. Hatubagui baina yao hata mmoja, na sisi ni wenye kusilimu kwake.


Ila sasa sisi wanaadamu tuliingia na kuharibu vitabu vya Mwenyezi Mungu na kutoa baadhi ya maneno na kuweka ya kwetu.

QURAN 11:110

110. Na kwa yakini tulimpa Musa Kitabu; kikatiwa hitilafu ndani yake. Na lau kuwa si neno lilio kwisha tangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi, (kuwa ipo siku maalumu ya hukumu) bila ya shaka ingeli hukumiwa baina yao (sasa hivi). Na hakika wao wamo katika shaka juu yake inayo wahangaisha.'


NB: Kama Taurati, Zaburi na Injili visingekuwa vimetiwa mikono na waandishi na kubadilishwa maana zake basi visingekuwa na tofauti yeyote na Quran, kwa sababu Mwenyezi Mungu huyo huyo mmoja ndio kateremsha vitabu vyote hivyo.

Ushauri wa bure tu; kwa kuwa wewe unataka kujifunza, basi soma vitabu vyote vya Mwenyezi Mungu usibague chochote, na muombe Mwenyezi Mungu akuongoze katika njia iliyo sawa.

 
Sisi wayahudi na Talmud yetu tuna parck wapi ??
 
Naona hilo swala la Birmingham umelikazania kweli , unajua kuwa Qur'an ilikuwa wakati mwingi ilikuwa inashuka kutokana na matukio ? sasa hiyo ya huko ilijuaje matukio yatakayotokea baadae tena mengine ikihusu watu na kutaja majina kabisa ?mfano Abu Lahab ,Zayd ambao walikuwepo wakati wa Mtume Muhammad SwallaAllahu'aleyhi wa salaam .

Mimi nimesoma kitabu cha historia ya Qu'ran na kueleza kila kitu hadi zilikohifadhiwa baadhi maandiko ya na zilifika vipi.

Mbona hizo taarifa unazo pekee yako na hizi taarifa official kutoka Birmingham University hakuna iliposemwa inaonyesha umeandika kabla ya Jibril ('Aleyhisssalaam) kushusha wahyi wa Qu'ran ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…