Kipi Mungu anachoweza kukifanya kikanisaidia?

Tukiachana na hadithi nzuri tunazosimuliwa kuhusu nguvu za Mungu, nahitaji kufahamu ni kipi anachoweza kunisaidia maana kila kitu nafanya peke yangu.

Naamka asubuhi naenda kupambana nikipata pesa namshukuru Mungu, kwanini Mungu asinipe pesa mimi nikae? Je, hawezi? Au hataki?

Kuna kipindi niliugua sana nikaomba Mungu sikupona mpaka nilipotibiwa na wahindi. Je wahindi wanamzidi Mungu akili?

Kama ameshindwa kunipa ninachokitaka nikiwa hai, je nikifa atanipa uzima alioahidi?

SWALI: JE, NI KIPI MUNGU ANAWEZA KUNISAIDIA KIKAONEKANA?

Swali linatakiwa kuwa: Nifanye nini kutimiza wajibu wangu kwa Mungu ili niweze ku access uweza wake alioutoa bure kupitia Kristo.
 
Mawazo yake si kama yako.
Yeye ni mwelevu zaidi kuliko wewe

Kiufupi yote unayoyaona yanatakiwa kuwa kama yalivyo

Na wakati mungu atamfanyia kila mtu hayo ynayoyasema dunia itakosa maana na hata yeye mwenyewe hatokua na maana tena

Jaribu kutafakari kama kweli unaakili utaelewa na maanisha nini!
Hii lugha uliyotumia,ni ngumu kueleweka,
Hao madokta wa kihindi,waliokusaidia,wamepewa uwezo na Mungu/super power,
Isingewezekana wakorea,wakae tu waombe Dua,Mungu awatengenezee simu Bomba kama Samsung,ilibidi wasome,waumize bongo,wajiamini,leo wanatishia Dunia nzima kwa bidhaa yao moja.
Hata Eron musk,uwezo wake kapewa na Mungu,alijiamini,akatumia mikono yake kutengeneza vitu,Mungu atakupa pumzi na huo ubongo,Mengine lazima ushiriki,huwezi kulishwa kama kinda la Ndege,
 
Mungu Alisha kusaidia ila hujamwona (Neno linasema atainua watu Kwa ajili yako Amemuinua mhindi kukutibu Kwa dawa alizoziumba Mungu

Mungu ndiye hutupa nguvu ya kupata UTAJIRI Hivyo afya uliyonayo ni Mungu kakupa

Hivyo Mungu kakusaidia Wewe hujui
 
Hii lugha uliyotumia,ni ngumu kueleweka,
Hao madokta wa kihindi,waliokusaidia,wamepewa uwezo na Mungu/super power,
Isingewezekana wakorea,wakae tu waombe Dua,Mungu awatengenezee simu Bomba kama Samsung,ilibidi wasome,waumize bongo,wajiamini,leo wanatishia Dunia nzima kwa bidhaa yao moja.
Hata Eron musk,uwezo wake kapewa na Mungu,alijiamini,akatumia mikono yake kutengeneza vitu,Mungu atakupa pumzi na huo ubongo,Mengine lazima ushiriki,huwezi kulishwa kama kinda la Ndege,
Point
 
Maandiko yapi?
Mimi nakuambia uhalisia wa mambo siongei miujiza hapa. Wengi wanapenda maandiko ya kimiujiza.

Mwanadamu amepewa uwezo wa kufanya kazi na Kutumia Akili na sio kutenda miujiza.
Kuomba Mungu ni kutafuta miujiza, yaani Jambo lililokushinda

Sasa Jambo lililokushinda wewe mwingine halimshindi, mfano Mimi labda sina pesa alafu wewe unazo, siwezi muomba Mungu kitu ambacho ninaweza kukipata Kwa binadamu mwingine.
Labda ndio maana ukaambiwa ombeni nanyi mtapewa lakini ni kuomba binadamu wenzako vile ambacho hauna.

Mfano mwingine ni wewe mwenyewe, ulisema ulikuwa unaumwa Sana nusura tuchangishe rambirambi. Lakini wakatokea Wahindi wakatoa Dawa.
Sasa ulitaka Mungu akusaidie Jambo ambalo Wahindi wanaliweza?😂😂😂

Kwa mfano, waafrika hatuwezi kuomba Mungu atupe teknolojia ya magari, au simu Wakati wapo watu weupe(wazungu na Wachina) wenye uwezo wa hizo teknolojia.

Hivyo tunachoweza kukifanya ni kuwaomba Watu hao watufundishe nasi tuweze kutengeneza hiyo teknolojia. Kama hawataki basi tunaouwezo WA kuzuia baadhi ya malighafi tulizonazo ambazo wanazihitahi Kutoka kwetu.

Mambo yako Hivyo.

Kuomba Mungu sio rahisi kama hivyo. Ni utovu WA adabu tuu.
Wengine wanafunga ,kuomba na kusali Mungu awapatie Majumba na Magari
 
Tukiachana na hadithi nzuri tunazosimuliwa kuhusu nguvu za Mungu, nahitaji kufahamu ni kipi anachoweza kunisaidia maana kila kitu nafanya peke yangu.

Naamka asubuhi naenda kupambana nikipata pesa namshukuru Mungu, kwanini Mungu asinipe pesa mimi nikae? Je, hawezi? Au hataki?

Kuna kipindi niliugua sana nikaomba Mungu sikupona mpaka nilipotibiwa na wahindi. Je wahindi wanamzidi Mungu akili?

Kama ameshindwa kunipa ninachokitaka nikiwa hai, je nikifa atanipa uzima alioahidi?

SWALI: JE, NI KIPI MUNGU ANAWEZA KUNISAIDIA KIKAONEKANA?
Huna uwezo wa kufa mwenyewe kwa hiari yako; atakusaidia kufa kwa kukuondolea pumzi ya uhai!
 
Kwa namna ulivyoandika inaonekana ni jinsi gani huna imani na Mungu, na km huna imani na Mungu huwezi kuona msaada wake kwa namna yoyote, Mimi ni shuhudu, kuna vitu vinmenitokea maishani baada ya kumuomba Mungu na mwisho wa siku nikakiri kwa kinywa changu kwamba ni Mungu aliyenisaidia, kwa hiyo jifunze zaidi kuhusu Mungu ili imani yako ikue.
 
Ni kwamba nataka nikiomba kitu kije kimiujiza, sio mimi nikitafute tena

Maana nikitafuta bila kuomba nitapata tu
 
Baada ya miaka mia toka sasa, kutakuwa hakuna tena huu ujinga unaoitwa dini. Maswali ni mengi kuliko majibu.
 
Mungu hawezi kukusaidia mpaka maombi yako umshirikishe mtu mwingine.
Waislamu wanaiita "shirk",wanasema "shirk" ni makosa. Waislamu wabishi sana. SHIRK NI LAZIMA. Waislamu pia wanamshirikisha Mtume na Mungu.
Ndiyo maisha. Unatibiwa hospitali unamshirikisha daktari na Mungu. Unajifunza physics shuleni unamshirikisha mwalimu na Mungu. Mke na watoto wanakutegemea wanakushirikisha wewe na Mungu.
Na Mwislamu pia,mpaka hapo akili yake itakapokomaa,anategemea Sunna ya Mtume. Mpaka hapo akili yake itqkapokomaa,anaitegemea akili ya Mtume . Mtume ana ushawishi kwa Muumbaji.
Karika yoga zipo chakra tisa. Itachukua muda mrefu sana kuelezea function zake.
Lakini ipo muladhara chakra,swadhisthana chakra,manipuraka chakra,anahata chakra,visuddha chakra,ajna chakra,Nirvana chakra,guru chakra,na sahasrara chakra. Guru(ambayo maana yake ni mwalimu,mkufunzi,etc),ipo karibu,na inafanya kazi kwa ukaribu na sahasrara chakra ambayo inakuunganisha na Mungu.
 
Sawa, kwaiyo yeye peke yake hawezi kunipa nachotaka, mfano nataka pesa anipe?
 
Back
Top Bottom