Swali zuri sana. Kwa uelewa wangu na kwa ufupi; Mwenyezi MUNGU ni mkuu mno. Halinganishwi na chochote wala yeyote. Yaani hata kwa binadamu, yeye ni mkuu mno japokuwa binadamu tumeumbwa kwa upendeleo kuliko viumbe wengine (wote), na sio ajabu ndio maana tunapata utashi wa kuhoji kama hivi.
Nirudi kwenye jibu, ni kuwa; ukuu wa MUNGU ni mkuu kuzidi mahitaji ya kawaida ya mwanadamu. Mfano: wewe una mtoto unaempenda sana na kujitahidi kumtimizia kila aina ya mahitaji yake. Lakini huwezi kamwe kumtimizia kila hitaji lake la sivyo hatakuwa mtoto bali mdoli. Kamwe huwezi kulala badala yake, huwezi kuchukua uchovu kwa badala yake (uchovu wake uuchukue wewe), huwezi kuanza kujifunza kutambaa, kutembea, kuanguka, kuhisi njaa, kiu, badala yake, hali kadhalika kuugua homa, kunya au kukojoa kwa niaba yake. Ni lazima hivyo vyote avifanye yeye mwenyewe ILI awe binadamu aliyekamilika (atake au asitake).
Vivyo hivyo kwa upande wa MUNGU BABA, yeye huanzia pale tunaposhindwa kwa uwezo wetu wa kibinadamu. Kumbuka binadamu tuna akili sana. Bongo zetu upo complex sana. Ni jinsi gani tu tunavyozitumia (katika nyanja nyingi) ndivyo tunavyofanikiwa ku-achieve mambo mengi zaidi. Mfano: fikiria majiji makubwa nje ya Africa, wazia maghorofa, vyombo vya usafiri, na teknolojia walizo nazo. Vyote vimeundwa kwa akili za wanadamu- tunao fanana nao kibaiolojia kuanzia Kingdom hadi Specie. Hata hizo dawa za Wahindi, zilitokana na tatizo kuwakumba wao sawasawa na lilivyokukumba wewe na si ajabu kwao mtu/watu walifariki, ndipo na wao wakapata maarifa ya kukabiliana na hilo tatizo kwa kutengeneza dawa ambayo ikaja pia kukusaidia.
Hivyo basi Imani huja pale ubinadamu unapokwama kabisa.. na msaada wa MUNGU huibuka kwa namna ya pekee ambayo haielezeki kibinadamu. Baadhi yetu husema, "ana bahati/nyota/machale, n.k" ila mara nyingi ni msaada wa Mwenyezi MUNGU unaofanya kazi. Msaada huu huja kwa wakati wake, hautegemei maombi yako, kufunga kwako, wala sadaka zako.. hivyo vyote tunavifanya na ni muhimu ili kutuweka kuwa karibu zaidi na MUNGU na sio guarantee ya kutuletea msaada wa MUNGU.
Barikiwa sana kwa swali zuri.