Auz
JF-Expert Member
- Apr 6, 2016
- 13,539
- 11,419
Kupambana kwako, kuponeshwa na Wahindi, ndio jinsi alivyokusaidia kupitia uwezo aliowajaalia nyie wote. Ukijisaidia, naye atakusaidia.Tukiachana na hadithi nzuri tunazosimuliwa kuhusu nguvu za Mungu, nahitaji kufahamu ni kipi anachoweza kunisaidia maana kila kitu nafanya peke yangu.
Naamka asubuhi naenda kupambana nikipata pesa namshukuru Mungu, kwanini Mungu asinipe pesa mimi nikae? Je, hawezi? Au hataki?
Kuna kipindi niliugua sana nikaomba Mungu sikupona mpaka nilipotibiwa na wahindi. Je wahindi wanamzidi Mungu akili?
Kama ameshindwa kunipa ninachokitaka nikiwa hai, je nikifa atanipa uzima alioahidi?
SWALI: JE, NI KIPI MUNGU ANAWEZA KUNISAIDIA KIKAONEKANA?