Kipi ni kigezo sahihi pindi unapochagua mtu wa kuoa?

luis diaz

Member
Joined
Feb 28, 2022
Posts
86
Reaction score
208
Habarini naomba kuuliza, ukiachana na kumpenda mpenzi wako je, ni kigezo gani kingine unaangalia mpaka unafikia kusema huyu anafaa kuwa mke?

Na je, mdada anaesali sana ni moja ya kigezo? Je, mtu akiwa na hofu ya Mungu inatosha kuwa kigezo? Au kuna mengine tofauti na hayo?
 
Likifika swala la kuoa huwa hakuna vigezo sahihi. Moyo ukishaamua yake hata akiwa jambazi utamuona malaika tu.
Kikubwa kama hujaoa/olewa muombe Mungu wako aelekeze moyo wako sehemu sahihi tu.
 
Angalia familia ambayo baba ni baba kweli siyo zile familia ambazo kila mtu ni kambale. Swala la hofu ya Mungu ni kichaka.

Usichague siku ya sherehe, hata ukivutiwa fanya ziara ya kushtukiza kabla hajapiga mswaki usijekuchanganywa na kope bandia, vigodoro, make up n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…