Fungulia tu hizo redio zao usikie habari za makongamano na ibada za kubariki,kukomboa, kutakasa n.k mwaka mpya ujao. Ukiwa mpumbavu fulani unajipeleka halafu unaambiwa toa sadaka au panda mbegu kwa ajili ya mwaka mpya uwe wa mafanikio. Pesa zile zinaingia mfukoni kwa mhubiri. Hivi watanzania tumefika kiwango kibaya namna hii kwenye afya ya akili hata utapeli ulio wazi kabisa hatuwezi kuung'amua?? Hili ni janga.