Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
KIPINDI CHA MR. RIGHT NI KIZURI ILA NAMNA KINAVYOFANYIKA KINAAIBISHA NA KUDHALILISHA WANAWAKE.
Anaandika, Robert Heriel
Kuhani.
Ingawaje ni aibu kubwa Kwa mwanamke kutoka hadharani na kutangaza kukosa mume WA kumuoa lakini hiyo tunaweza kusema ni kasumba tuu Mbaya. Taikon ninaamini hata mwanamke anayohaki ya Kueleza yanayomkabili ikiwemo Masuala ya kihisia.
Kasumba hiyo nafikiri imejengwa katika msingi kuwa Mwanamke mzuri hawezi kosa mwanaume wa maana WA kumuoa,
Uzuri na thamani ya mwanamke ndio humpa jeuri, maringo na aibu ya kutokumfuata na kumtongoza mwanaume.
Mwanamke kutangaza hadharani kuwa amekosa mwanaume wa kumuoa tafsiri yake unamaanisha; Sio Mzuri, hana soko, au anamapungufu Fulani ambayo yeye mwenyewe anaweza kuyajua zaidi kuliko wanaomtazama.
Hata hivyo hiyo yote ni Dhana potofu na kasumba iliyomo katika jamii nyingi Duniani.
Ingawaje ni Dhana potofu na kasumba lakini inauhalisia Mkubwa. Mwanamke ni kitu cha thamani zaidi ya dhahabu hapaswi kujirahisisha na kujitangaza hadharani anatafuta mume.
Wanasema kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.
Kipindi cha Mr. Right kitasaidia kutoa Uelewa na kuondoa Dhana potofu kuwa mwanamke naye anauwezo wa kuelezea hisia zake lakini hakitaweza kubadili uhalisia.
Hata hivyo kipindi cha Mr. Right mbali na dhima kuu ya kuunganisha warembo na waume sahihi lakini pia ni kipindi kinachofunza na kuonyesha nini wasichana na warembo wanachokipenda na kipi hawakipendi kutoka Kwa wanaume. Ni wazi mbali na uzuri/muonekano wa mwanaume lakini kitu kikubwa wanawake hupenda Economy Status ya mwanaume.
Tatizo kuu la Kipindi cha Mr. Right ambalo ndilo limenifanya niandike mada hii ni; Uvaaji wa warembo wa kipindi hicho.
Uvaaji huo unadhalilisha na kuabisha wanawake.
Uzuri wa mwanamke sio mpaka Avae nguo za kuonyesha uchi wake au kubana maungo yake.
Uzuri wa mwanamke ili uitwe uzuri lazima ustiriwe, ulindwe kwani hiyo ndio Heshima ya uzuri. Huwezi kuta dhahabu inazagaa mitaani au kuchomwa na Jua.
Warembo, kutafuta mwanaume wa kukuoa kusikufanye ujidhalilishe, watu waone vitu wasivyopaswa kuona. Huko ni kujidharau, na kutafuta kudharauliwa.
Kipindi hicho kingekuwa ni sehemu muhimu ya kutangaza na kuhamasisha uvaaji wa stara na adabu, na kutangaza utamaduni wa jamii zetu.
Lakini sio kutangaza uhuni na kudhalilisha wanawake.
Gara B na wenzake liangalieni Jambo hili ikiwa kweli lengo Lenu ni Kutoa burudani pamoja na kutoa elimu katika kipindi chenu.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam