Kipindi cha Mzee Kikwete hakuna aliyehitimu ualimu au udaktari akakosa ajira. Wote walikuwa wanapangiwa tena unachagua pa kwenda

Kipindi cha Mzee Kikwete hakuna aliyehitimu ualimu au udaktari akakosa ajira. Wote walikuwa wanapangiwa tena unachagua pa kwenda

Ndo aliharibu kila kitu,aliajiri zaidi ya uwezo wa serekali kulipa,huwezi lundika walimu bila kuangalia ability to pay on long run

Sio kweli. Tuongee ukweli wa mambo. Aliyeharibu ni yule aliyeanza kuzuia ajira kwa Miaka mitano.
 
Hujui utendendalo soma mambo ya nyakati.hakuna hata nchi moja duniani ambayo imeweza kuwapatia ajir a wahitimu wake wote ila tu ungesema ijenge mazingira ya uwekezaji ili wengine wakaajiriwe huko.kwa kuwa serikali yetu ni ya kishetani inajenga mazingira hayo ili itawale milele
Ni jk tu aliweza kuwaajiri wote ndo mana nasema tutamkumbuka
 
Jk alikua na mipango ya kutengeza ajira delta binafsi kwa kutengeza middle class wengi,akaja yule akavuruga kila kitu

Na huu ndio ukweli. Sijui kwanini watu wanaopinga hawataki kukubali wanalazimisha Hali hubadilika. Kipindi Cha JK mtu unamaliza ualimu tayari ulishapangiwa kituo Cha kazi. Ilitakiwa tumuulize aliwezaje?. Sio kukimbilia zama zimebadilika.
 
Mmeanza tena kumsakama marehemu, anayewalipa kufanya haya ni nani na lengo lake ni lipi?
 
Sikatai lakini pia na yeye angefikia Kokomo. Unawahitimu zaidi ya laki moja Kwa mwaka then Pato lako la taifa karibia 70% linalipa Deni la taifa na mishahara na posho Kwa watumishi alafu uwe na uthubu wa kuajiri kama mnavyofikiria

Hata wakati wa JK pesa ilikuwa nje nje sio Kama Sasa hivi. Ndio maana aliweza kuajiri watu wengi. Cha msingi ni kumuuliza aliwezaje na alitumia mbinu gani?.
 
Kimsingi aliyeharibu maisha ya watanzania wengi ni huyo ndugu aliyempokea JK kijiti!Sina hakika kama mambo yatakuja kukaa Sawa tena!Tuendelee kumuombea mama kwani hata yeye hana namna kwa vile alikuta kila kitu kimevurugwa!

Na hili watu wengi hawalioni. Wakati wa JK Mzunguko wa pesa ulikuwa mkubwa na ajira serikalini zilipatikana nk. Ila baadae sijui Nini kilitokea tumefika mpaka hapa. Yani ualimu ni wa kutumia maombi.
 
Watu tulikua na one lakini tukasoma education kwa sababu tu ya ajira.... Ningekua madogo wa cku hizi nisingesoma usenge wa education

Yes, umenikumbusha mbali Sana. Kipindi Cha JK watu wengi walisoma education kwa sababu ya ajira ya ualimu kuwa nje nje.
 
Mmeanza tena kumsakama marehemu, anayewalipa kufanya haya ni nani na lengo lake ni lipi?
Ndo aliyesababisha kusakamwa kila mara mana nchi iliihalibu sana na akawa anajigamba eti yeye ndo ananyoosha nchi. Aliwasiriba akina Ben mkapa na jk kumbe yeye ndo mharibifu sana ila media zikaogopa kuhoji chochote. Sasa kafa Wacha watu wapumue mana tulibanwa sana na hapakuwa na room ya kuongea
 
Katika utafiti wangu mdogo, nimebaini kwamba Walimu ambao wamekumbwa na tatizo kubwa zaidi la ukosefu wa ajira ni wale ambao waliosomea Masomo ya Sanaa (Arts). Wale waliosomea Masomo ya Sayansi na wamefaulu vizuri katika masomo yao, tatizo hili la ukosefu wa ajira linaonekana kuwa siyo kubwa sana kwao.
Wito: Someni Masomo ya Sayansi, kwani yana uwanja mpana wa kujiajiri au kuajiriwa, hata nje ya mipaka ya Tanzania.
Hapo tatizo hili limetoka kuwa la kila mtu n kuwa la kikundi cha watu Fulani wenye sifa zinazofanana
 
Uchumi feki nchi ikijengeka kila kona,nagari ikawa kawida kwa watanzania, GDP ikapaa,wakulima wakaishi maisha mazuri,miundombinu ikajengwa,fdi ikamiminika...acha ujinga babu

Sema JK hakuwa mpenda sifa Kama wengine. Ila kwa Sasa naona jamaa alijitahidi Sana.
 
Tatizo ni kuwa hujui hiyo inawezekanaje lakini ninyi ndiyo ambao mnang'ang'ana sehemu zenye maamuzi huku hamna mnalojua kuhusu kutengeneza ajira hayo yakawezekana...Adui mkubwa wa watanzania kati ya wale wa nne wa Mwl Nyerere ni UJINGA. watanzania wengi siyo weledi lakini wanajimwabafai. Hakuna kitu kibaya kama uwe hujui kitu na bado hujui kuwa hujui. Kujua kutokujua ndiyo mwanzo wa kuleta suluhisho

Kweli kabisa mkuu. Mtu anasema haiwezekani kuajiri kisa tu uwezo wake wa kufikiri umeisha.
 
Kwa kweli nakazia hapo mwisho ulivyomalizia yule jamaa hakika alileta titizo kubwa mno bora hata alivyotangulia . Wahitimu wa mwaka 2015 , 2016 na 2017 . Mtaani wengi maisha yao yameyumba ukiangalia vizuri sababu ni lile jamaa .

Shida jamaa alitaka pesab za kuajiri ziende kununua ndege na kujenga SGR.
 
Unamtetea jiwe rais wa ovyo kuwahi kutokea Tanzania, jiwe alikuwa ni WA ovyo na mbaguzi, , alifukuza wafanyakazi hewa na vyeti feki lakini hakufanya replacement , akaajiri watu wa kabila lake , wasukuma wote ambao nimesoma nao, na niliokutana nao katika harakati za kusaka ajira walipata kazi, Mungu ni wa wote akafanya yake.

Yule jamaa sijui ilikuwaje akawa Rais, ameliacha taifa la hovyo kuliko alivyolikuta. Watanzania tulikuwa wamoja na kulikuwa na political consciousness, ila alipoingia yeye mambo yakawa hovyo, mara Sukuma Gang, mara chawa wa kumsifu na kuabudu nk. Aiseeh! Itachukua muda Tanzania kurudi kwenye Hali yake ya Mwanzo.
 
Ndo aliyesababisha kusakamwa kila mara mana nchi iliihalibu sana na akawa anajigamba eti yeye ndo ananyoosha nchi. Aliwasiriba akina Ben mkapa na jk kumbe yeye ndo mharibifu sana ila media zikaogopa kuhoji chochote. Sasa kafa Wacha watu wapumue mana tulibanwa sana na hapakuwa na room ya kuongea
Ulibanwa ukiwa unafanya nini? Kwasababu mmlikuwa kimya ghafla tu, boss wenu kapita kule Chato na ninyi mmeanza kumtemea mate marehemu.
Ninyi viumbe mnaroho gani? Hamridhiki tu na ukwasi mnaoupata kwa gharama za watanzania maskini?

Kwanini hampendi maskini wawe na amani hata kidogo?

Chama Cha Mapinduzi kimehama kutoka kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi kuwa chama cha 'wafanyabiashara' na 'wezi' lini chama hiki kitarudi katika dhumuni la kumuinua mkulima na mfanyakazi wa taifa hili?

Kwenu ninyi utaifa na maendeleo ni kuwapo kwa uhuru wa kukwapua na mifuko yenu kujawa maburungutu ya wizi?

Baada ya kukwapua na kushindwa kuendesha nchi mnaanza kumlaumu marehemu kwa kushindwa kwenu kutumia vyema hata pato lenu dogo mnalokusanya ndani.
 
Back
Top Bottom