Genius Man
JF-Expert Member
- Apr 7, 2024
- 3,558
- 7,935
Siku ya sabato mwanzilishi ni mungu mwenyewe kulingana na maandiko, na inatambulika na ushahidi wa maandiko upo.
Dhehebu la usabato mwanzilishi ni Ellen G White halitambuliki na biblia na hakuna kielelezo chochote kuhusiana nalo kwenye biblia zaidi ya maelezo ya kujitegemea ya Ellen G White mwenyewe kujitetea uhalali wake.
Lakini pia madhehebu mengine mengi tunayo yapenda katika uhalisia hayana ushahidi wa kimaandiko zaidi ya kujitetea yenyewe nje ya maandiko, hakuna kielelzo cha ulokole au ukaroriki .nk
Swali la kutafakari. (ASOMAYE NA HAFAHAMU)
yesu ni kweli alikuja ili kutuonesha njia ? ndio ila wengi hawamuelewi.
1 Yohana 1:1-7
1 Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima;
2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);
3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.
4 Na haya twayaandika, ili furaha yetu itimizwe.
5 Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza lo lote hamna ndani yake.
6 Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli;
7 bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.
Wakristo wanapaswa kumfuata yesu alikuja ili kuonesha njia na yeye ndie njia hamaanishi useme tu mdomoni kuwa ni njia ya uzima kama wengi wanavyo fanya hapana.
anamaanisha kwamba uishi kama yeye ufuate nyayo zake jinsi alivyoishi ndio utashinda dhambi na uongo au upotoshaji.
Namaanisha kama yesu hakuwa mkatoriki au mlokole au msabato basi unapaswa na wewe ushike njia hiyo, na kama hakuiba au kutukana basi na wewe ushike hayo hii ndio ile nuru inayohubiriwa na ya kweli lakini wengi hawaioni, wengi hawaielewi. (ASOMAYE NA AFAHAMU)
Yesu ndio msingi wa yote hamaanishi tu ujitamkie bali muelewe anamaanisha nini hapa nina maandiko tofauti tofauti kisha mwisho nitaweka maandiko ya unabii wa watakao okolewa ni wakina nani ili uchukue hatua sahihi. (ASOMAYE NA AFAHAMU)
. 1 Petro 2:21
Matendo ya Mitume 4:12
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Yohana 14:6
Maandiko hayo yanamaanisha huendi mbinguni ila kwa kupitia yeye yani kwa kufuata nyayo zake jinsi alivyoishi tu, je wewe ni mkatoriki au mlokole ndivyo yesu alivyoishi hivyo ? (ASOMAYE NA AFAHAMU)
Mwisho tafakari watakao okolewa ni akina nani kwenye unabii wa siku za mwisho kisha tulinganishe na haya maneno hapa juu tufahamu siri iliyojificha hapo.
Ufunuo 12:17
ufafanuzi kidogo yesu akuwa mwizi, hakuwa mzinzi, kutokufanya hivi ndio kushika amri kumi kwahiyo wanao mfuata nyayo zake kwa kufanya hivi moja kwa moja wanashika amri hizo bila hata kujua.
Lakini fungu hilo la kiunabii linasema joka ambaye ni shetani anafanya vita na watu wenye ushuhuda wa yesu, yani wale wanao mfuata nyayo zake sio wakatoliki kwani wana mshuhudia yesu hakuwa mkatoriki, hao watu sio wasabato kwani wanamshudia yesu hakuwa masabato maandiko yana ongezea hakupenda maisha yao hata kufa na walimshinda shetani kwa ushuhuda wao huo.
soma tena (ASOMAYE NA AFAHAMU)
Ufunuo 12:17
Watu wenye ushuhuda wa yesu hawa ndio wanaofuata nyayo za yesu hawa watapitia njia zile zile alizotumia yesu kumshinda shetani na sio kupitia sehemu nyengine nime eleweka sijui ?
Lakini (ASOMAYE NA AFAHAMU)
Ufunuo 12:11
Unabii unasema watamshinda shetani na uongo na upotoshaji wake kwa kupitia yesu nao wataenda zao mbinguni kama yesu alivyo shinda na kuondoka zake mbinguni kwasababu wanafanya yale yesu aliyo yafanya na sio kitu kingine wapo tayari kufa lakini sio kufanya kinyume na matendo ya yesu hapa ndipo watamshinda shetani na kuwa watakatifu.
Hii ndio sababu hakuna usabato au ukatoriki au ulokole kwenye biblia wengi hawaelewi maandiko sasa nime wafafanulia kazi kwako kuamini au kuendelea kufuata njia ya kushindwa na shetani.
Kuna baadhi ya maandiko nime yafupisha ili kufocus kwenye mada husika hasa hizo aya za kiunabii ni zinaelezea uhalisia wa unabii wa siku za mwisho jinsi itakavyokuwa.
Kama mlivyomuona yesu akienda zake mbinguni baada ya kushinda ndipo watakatifu wake wamfuatao wataenda vile vile wao watafanya matendo sawa na yake wakiwa duniani yeye ndie njia ya namna ya kushinda madehebu ya uongo, na upotoshaji.
Kumbuka uwepo wa madhehebu mengi lazima kuwe na madhehebu ya uongo hapo haiwezekani madhehbu yote yamzungumzie yesu kwa naman tofauti lakini maandiko yanatupasha habari namana ya kushinda hapo wewe mfuate yesu yani fanya matendo yake alisaidia watu na wewe saidia alikuwa mwema na wewe kuwa mwema, hakuwa msabato ba wewe usiwe msabato.
Tumalize na hii ya mwisho
Mathayo 7:13-14
Njia iendayo uzimani imejificha sana nayo ni ndefu sana waionayo ni wachache sana inasikitisha,
Basi mimi na wewe tutasimama katika kura zetu siku za mwisho. Amina

“Maana mliitiwa hayo; kwa sababu Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akiwaachia kielelezo, ili mfuate nyayo zake.”
Matendo ya Mitume 4:12
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Yohana 14:6
“Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”
Maandiko hayo yanamaanisha huendi mbinguni ila kwa kupitia yeye yani kwa kufuata nyayo zake jinsi alivyoishi tu, je wewe ni mkatoriki au mlokole ndivyo yesu alivyoishi hivyo ? (ASOMAYE NA AFAHAMU)
Mwisho tafakari watakao okolewa ni akina nani kwenye unabii wa siku za mwisho kisha tulinganishe na haya maneno hapa juu tufahamu siri iliyojificha hapo.
Ufunuo 12:17
“Naye yule joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda kupigana na wale waliobaki wa uzao wake, wanaozishika amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu.”
ufafanuzi kidogo yesu akuwa mwizi, hakuwa mzinzi, kutokufanya hivi ndio kushika amri kumi kwahiyo wanao mfuata nyayo zake kwa kufanya hivi moja kwa moja wanashika amri hizo bila hata kujua.
Lakini fungu hilo la kiunabii linasema joka ambaye ni shetani anafanya vita na watu wenye ushuhuda wa yesu, yani wale wanao mfuata nyayo zake sio wakatoliki kwani wana mshuhudia yesu hakuwa mkatoriki, hao watu sio wasabato kwani wanamshudia yesu hakuwa masabato maandiko yana ongezea hakupenda maisha yao hata kufa na walimshinda shetani kwa ushuhuda wao huo.
soma tena (ASOMAYE NA AFAHAMU)
Ufunuo 12:17
“Naye yule joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda kupigana na wale waliobaki wa uzao wake, wanaozishika amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu.”
Watu wenye ushuhuda wa yesu hawa ndio wanaofuata nyayo za yesu hawa watapitia njia zile zile alizotumia yesu kumshinda shetani na sio kupitia sehemu nyengine nime eleweka sijui ?
Lakini (ASOMAYE NA AFAHAMU)
Ufunuo 12:11
“Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.”
Unabii unasema watamshinda shetani na uongo na upotoshaji wake kwa kupitia yesu nao wataenda zao mbinguni kama yesu alivyo shinda na kuondoka zake mbinguni kwasababu wanafanya yale yesu aliyo yafanya na sio kitu kingine wapo tayari kufa lakini sio kufanya kinyume na matendo ya yesu hapa ndipo watamshinda shetani na kuwa watakatifu.
Hii ndio sababu hakuna usabato au ukatoriki au ulokole kwenye biblia wengi hawaelewi maandiko sasa nime wafafanulia kazi kwako kuamini au kuendelea kufuata njia ya kushindwa na shetani.
Kuna baadhi ya maandiko nime yafupisha ili kufocus kwenye mada husika hasa hizo aya za kiunabii ni zinaelezea uhalisia wa unabii wa siku za mwisho jinsi itakavyokuwa.
Kama mlivyomuona yesu akienda zake mbinguni baada ya kushinda ndipo watakatifu wake wamfuatao wataenda vile vile wao watafanya matendo sawa na yake wakiwa duniani yeye ndie njia ya namna ya kushinda madehebu ya uongo, na upotoshaji.
Kumbuka uwepo wa madhehebu mengi lazima kuwe na madhehebu ya uongo hapo haiwezekani madhehbu yote yamzungumzie yesu kwa naman tofauti lakini maandiko yanatupasha habari namana ya kushinda hapo wewe mfuate yesu yani fanya matendo yake alisaidia watu na wewe saidia alikuwa mwema na wewe kuwa mwema, hakuwa msabato ba wewe usiwe msabato.
Tumalize na hii ya mwisho
Mathayo 7:13-14
“Ingieni kwa mlango mwembamba; kwa sababu mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao waendao kwa njia hiyo ni wengi. Na mlango ni mwembamba, na njia imebana iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.”