Kipindi hiki cha likizo ya sensa Wazazi wawalinde watoto wao, mitaa imefurika

Kipindi hiki cha likizo ya sensa Wazazi wawalinde watoto wao, mitaa imefurika

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
kuna likizo ndefu kwa ajili ya sensa ya watu na makazi nchini, ambapo wanafunzi kuanzia ngazi ya chekechea hadi vyuo wapo mtaani, na kiukweli mitaani pamefurika kuna kila aina ya makundi na watu wa rika tofauti tofauti.

Sasa huu ni muda wa wazazi kuchukua kila aina ya tahadhari kwa ajili ya kulinda watoto ambao muda mwingi watakuwa wanzagaa mitaani na hasa kwenye michezo yao mbalimbali.

Wazazi wengi pamoja na kwamba wapo katika harakati za hapa na pale za utafutaji wa maisha lakini ni vyema pia wakapangilia muda wao vizuri kwa ajili ya usalama wa watoto wao,ama kukabidhi watoto wao sehemu salama pindi waendapo kwenye utafutaji wao.

Kipindi hiki cha likizo ambapo kuna kila aina ya watu mitaani watoto hupitia changamoto nyingi kama vile kubakwa, kulawitiwa, kupigwa na kujeruhiwa, kujifunza mambo ya hovyo kutoka kwa watoto wa mtaani.

Wazazi wasisubiri kila kitu kuambiwa na serikali bali wao wenyewe wachukue tahadhari juu ya watoto wao.

download.jpeg
 
Unaposema mitaa imefurika unamaanisha nini?
Asilimia kubwa ya watoto wa kitanzania wanasoma wanakoishi na hawakai boarding! Usisahau kusema hiyo mitaa imefurika Arusha au mkoa gani
 
Unaposema mitaa imefurika unamaanisha nini?
Asilimia kubwa ya watoto wa kitanzania wanasoma wanakoishi na hawakai boarding! Usisahau kusema hiyo mitaa imefurika Arusha au mkoa gani
Wazazi tumemuelewa vizuri. Tunashukuru kwa kujali kwake.
 
Back
Top Bottom