Kipindi Kipi Cha Radio Kinakukumbusha Mbali Sana??

Kipindi Kipi Cha Radio Kinakukumbusha Mbali Sana??

adakiss23

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2011
Posts
4,945
Reaction score
5,380
Mi Nakumbuka Kipindi Cha Hongera RTD kilikuwa mida ya mchana wakati ndo narudi shule nikiwa STD 1,2 hivi. Nmechoka jua kali njaa ya kutosha nmechafuka ile mbaya.. Nikifika 2 ndani friji liko wapi nipooze rejeta.
Kipindi cha pili kilikuwa Love and Dedication Zone kilikuwa kinaendeshwa na John Dilinga (DJ JD) alipokuwa 101.4fm. Nakumbuka nilikuwa O'level tym hizo ndo nilikuwa napiga msuli taratibu. Kipindi kikiisha naenda zangu kulala.
Dah! Long tym yaani..
Wewe unakumbuka kipindi kipi?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mama na mwana RTD....ilikuwa siku ya jpil mchana kama sikosei!!
 
Salamu kwa wagonjwa RTD...saa mbili asubuhi, jumapili
 
Mchana mwema,nilikuwa sikipendi -tatizo ni mie si kipindi ,muda huo narudi kutoka skuli njaa ya ukweli tu ,nikifika tu bi mkubwa ndio kwanza ananituma nikanunue mkaa au mchele, whatever kuhusiana na msosi ili PA-PI-KWE!halafu mtangazaji aniambie ni mchana mwema?
 
Tukiacha utani rtd Ilikuwa na vipindi vya maana, hizi redio za siku hizi upuuzi mtupu. Yaani kuna vipindi ambavyo sidhani hata mtu mmoja anasikiliza.
 
Kumekucha jama kumekuchaa, paoja na majira ya asubuhi vilikuwa vinanikera sana maana ni mida ambayo dada alikuwa ananitilia timu kuniamsha niende shule na mdau kipindi hicho shule ilikuwa sawa na segerea kwangu. Ila namshukuru kwa purukushani zake baadae nikafyata na kupiga shule kwa sasa si haba ni miongoni mwa wasomi wachache sana wenye shahada zaidi ya 1 mtaani kwetu Mtogole.
 
Mi Nakumbuka Kipindi Cha Hongera RTD kilikuwa mida ya mchana wakati ndo narudi shule nikiwa STD 1,2 hivi. Nmechoka jua kali njaa ya kutosha nmechafuka ile mbaya.. Nikifika 2 ndani friji liko wapi nipooze rejeta.
Kipindi cha pili kilikuwa Love and Dedication Zone kilikuwa kinaendeshwa na John Dilinga (DJ JD) alipokuwa 101.4fm. Nakumbuka nilikuwa O'level tym hizo ndo nilikuwa napiga msuli taratibu. Kipindi kikiisha naenda zangu kulala.
Dah! Long tym yaani..
Wewe unakumbuka kipindi kipi?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Taarifa ya habari
 
Club raha leo, kipindi cha salamu kwa wagonjwa.
For some reason malenga wetu inanikumbumbusha huzuni flani. Nadhani nilikuwa nakisikiliza zaidi wakati naumwa.
 
NAKUMBUKA KIPINDI CHA KLABU RAHA LEO SHOW,NAKUMBUKA SAUTI YA UNCLE J NYAISANGA

UNCLE J;Kwa mara nyingine tena Redio Tanzania Dar es Salaam yawaletea klabu raha leo.....
MASHABIKI:Shoooo!
 
Club Raha Leo Show, Kijaruba Oyeee, Misakato, Pwagu na Pwaguzi, Mazungumzo Baada Ya Habari, Muziki Asilia, Mwanamuziki Wako...vyote hivi ni vya RTD!
 
Mchezo wa redio hasa ule wa akina Jangala yaani we acha tu!
Kiatu
Mzee Mundu
Mshamu (jangala alikuwa akiita 'Nsamu')
Mzee Kagunga
 
Ombi lako - saa tisa hadi tisa na nusu kabla ya kipindi cha Mkulima wa kisasa, ( Mkulima wa kisasa .... motomoto tanzania , wananchi). Mwaka 1979 enzi zangu huko karibu na Majohe ! lolol
Kwenda mjini usipopanda Ikarus basi tena!
 
Back
Top Bottom