Kipindi Kipi Cha Radio Kinakukumbusha Mbali Sana??

Kipindi Kipi Cha Radio Kinakukumbusha Mbali Sana??

1.Shambani Shambani jamani twende shambani
2.Kipindi Cha Salama Jabri East Radio(Usiku)
3.DJ JD-Luv n' Dedication 101.4
4.The Crewz-Ya DJ JD
5.Rovin DJ--Young Millionea Jacob Nsungu
 
1) Malenga wetu 2) Club raha leo show na Julius Nyaisanga 3) The Cruz East Africa radio na John Dilinga (naamini itachukua miaka mingi sana kupata kipindi bora kama hiki kwa R&B and Hip hop!
 
Mi Nakumbuka Kipindi Cha Hongera RTD kilikuwa mida ya mchana wakati ndo narudi shule nikiwa STD 1,2 hivi. Nmechoka jua kali njaa ya kutosha nmechafuka ile mbaya.. Nikifika 2 ndani friji liko wapi nipooze rejeta.
Kipindi cha pili kilikuwa Love and Dedication Zone kilikuwa kinaendeshwa na John Dilinga (DJ JD) alipokuwa 101.4fm. Nakumbuka nilikuwa O'level tym hizo ndo nilikuwa napiga msuli taratibu. Kipindi kikiisha naenda zangu kulala.
Dah! Long tym yaani..
Wewe unakumbuka kipindi kipi?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Wakati umeenda sana....kipindi hicho DAR ES SALAAM inanukia dah! natamani maisha yangekuwa tape ningerudisha nyuma ili yaanze tena....mimi nakumbuka kipindi cha SIKILIZA BWANA UMEME.
 
Chombeza - Radio One. toka enzi hizo nalala na baba na mama
 
"MICHAKATO" cha RTD. Kinaaanza na kumaliza na sebene la " Msondo namba 5"


Sent from my Nokia 8310 using Tapatalk
 
Kipind cha Ujumbe wa leo

Kila siku saa mbili na robo usiku, enzi za uhai wake Mwl JK Nyerere. alitisha sana kwa umahili wakuchambuwa mambo.

Lazima nimsogelee baba akiwa na Radio yake ya mbao 277 redio zilizoonekana imara wakati huo
 
kitu KBC NAIROBI MPANGO MZIMA WA PATAPATA,
PIa MICHEZO BY EZEKIEL MARONGOOOOOOOOOOOOOO
 
Sayansiiii na Teknolojia kila ijumaa saa tatu kasorobo usiku na kale kawimbo ka kuanza na kumalizia kipindi na kipindi cha CLUB RAHA LEO SHOOOOOO NA Somebody Ponela
 
Mi Nakumbuka Kipindi Cha Hongera RTD kilikuwa mida ya mchana wakati ndo narudi shule nikiwa STD 1,2 hivi. Nmechoka jua kali njaa ya kutosha nmechafuka ile mbaya.. Nikifika 2 ndani friji liko wapi nipooze rejeta.
Kipindi cha pili kilikuwa Love and Dedication Zone kilikuwa kinaendeshwa na John Dilinga (DJ JD) alipokuwa 101.4fm. Nakumbuka nilikuwa O'level tym hizo ndo nilikuwa napiga msuli taratibu. Kipindi kikiisha naenda zangu kulala.
Dah! Long tym yaani..
Wewe unakumbuka kipindi kipi?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Kumbe wewe wa juzi tu!!! Mi nilifikiri unatukumbusha enzi zile mwanzoni mwa miaka ya 80 au kati-kati ya miaka ya 70. Yaani DJJD unayemsema ameanza utangazaji na UDJ juzi tu.... wewe vipi?? Ungetukumbusha vipindi kama vile "kijaluba' kilichokuwa kinatangazwa na Abdallah Mlawa au Mikingamo kilichokuwa kikitangazwa na Juma Ngalawa ama Ahmed Kipozi (enzi zile za uhujumu uchumi). Na vingine vingi tu...... Pole sana kijana wangu (mtoto), kwa kuvifikiria vipindi vya juzijuzi tu wewe unadhani imekuwa "long time'?
 
Hisia na Muziki

Walikuwa wanasema, "Kwa mara nyingine tena Redio Tanzania Dar es Salaam inawaletea Hisia na Muziki, Msimulizi wenu ni Angalieni Mpendu." Ala ya muziki ya kipindi naifananisha na ya Wimbo Asha Bora wa Sikinde.

Katika kipindi hicho ndiyo niliusikia Wimbo Sabalkheri Mpenzi wa kundi la Mila na Utamaduni Zanzibar, masikio yangu yaliniambia ni wimbo mzuri sana. Nilikuwa nimefungwa kanga nyuma ya shingo baada ya kutoka kuoga (kuogeshwa).

Mtindo wa kipindi hiki unafanana na Muundo wa Filamu ya 20 Percent "Furaha Iko Wapi?"


Enzi hizo...!!!!
 
Mchezo wa redio hasa ule wa akina Jangala yaani we acha tu!
Kiatu
Mzee Mundu
Mshamu (jangala alikuwa akiita 'Nsamu')
Mzee Kagunga



Kha ha ha ha haaaa! Umenikumbusha mbali kweli kweli!
Enzi hizo radio ni chache sana! Tunakusanyika mpaka,kisa mchezo wa CHIBUKU!
 
Mchezo wa redio hasa ule wa akina Jangala yaani we acha tu!
Kiatu
Mzee Mundu
Mshamu (jangala alikuwa akiita 'Nsamu')
Mzee Kagunga

Kuna mchezo waliucheza ulikuwa unahusu Malaria....

Basi wakuu mzee Jangala aliugua malaria ila yeye alikuwa anaiita "manyeria" akapelwa hosptali yeye alikuwa akiita "shipitali". Daktari alimwambia anaumwa malaria ambayo inaenezwa na mbu. Daktari alimwelekeza Mzee Jangala kuwa lazima akaariibu mazalia ya mbu ambayo ni madimbwi na vichaka vinavyozunguka nyumba.

Basi wakuu, katika kutekeleza maagizo ya daktari, Mzee Jangala alienda kufyeka bustani ya mbogamboga pamoja na shamba la maharage....mkewe aliporudi... mzozo uliotokea hapo ukizingatia ubishi wa mzee Jangala yaani usipime !!


Mzee Kagunga yeye alikuwa na kigugumizi cha kutisha, kama siyo mzoefu wa kigugumizi yaani itakuhitaji utumie FOUR WHEEL DRIVE kutoa neno moja kwa kigugumizi cha Mzee Kagunga....
 
Back
Top Bottom