Kipindi Kipi Cha Radio Kinakukumbusha Mbali Sana??


Halafu ndo ule wakati shairi flan hivi linaimbwa au...
 
Mie huwa nakumbuka kipindi cha muziki wa reggae kilichokuwa kinaendeshwa na ras Tkupitia external service ya RTD.
 
Mtaa wa mangoma - Redio one jumapili (huwa wananikumbusha miaka ya 1980)
 
Maswali kwa wanafunzi , kilikuwa kinarushwa na KBC (idhaa ya kiswahili ya Kenya) kila jumapili asubuhi, wakati shule za UPILI zilikuwa zina shindana kujibu maswali. mtangazaji mwendeshaji nimemsahau.

"Je huu ni ungwana", "Mchanganyiko maalum" vyote KBC (idhaa ya kiswahili ya Kenya) mtangazaji alikuwa Leornad Mambo Mbotela.
 
Majira cha subuhi yaani kikianza tu unamsikia baba anaita we fulani amka uende shule hapo naenda kunawa maji ya kwenye pipa ya baridiii huku unasikia mziki wa komoa tirindindindi eeeeeeeh,tirindindindi komoa au lile la mshindi,mshindi ni sabuni yenye nguvu yenye kutakasha kuliko zote mshindi eeeeeh!...
Pia kipindi kimoja hivi kilikuwa RFA usiku mnene kilikuwa kikiitwa salaaaam chapchap!.....
 

Sio Ben Omala (marehemu sasa)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…