Kipindi Kipi Cha Radio Kinakukumbusha Mbali Sana??

Kiswahili Lugha ya taifa

Hasa wimbo wake ule wakufungulia na kufungia kipindi..." na visiwani ooh !! Ni kiswahili cha tumika...kiswahili lughaa.. ya taifaaa... ya taifa...!" Kilikuwa kina rushwa na RTD nyakati za usiku.
 
Vipindi vya salamu vya Kenya Broadcasting Cooparation idhaa ya kiswahili,hasa kuanzia saa kumi jioni baada ya taarifa ya habari vipindi hivyo vilikuwa vinaendeshwa na mtagazaji Omuga Kabisae... nilikuwa nafurahia jinsi mtuma salamu maarufu wa Kenya "Sura Mbili Kiyango Mumanyi" alivyokuwa akitajwa mara nyingi katika vipindi hivyo.

Omuga Kabisai alikuwa anaupenda sana wimbo huu>>>http://www.youtube.com/watch?v=sanrGIbr_kk
 
michezo redio tanzania, ile mbili kasoro inanikumbusha 32 yrs ago nikiwa sumbawanga haha tumezunguka jiko hapo tunaota moto wali umepaliwa mkaa umewekwa juu ya mfuniko, hapo tunanjaa vilivyo basi kale ka mziki kanaanza kupigwa dah tunabwaga moyo sasa msosi bd dk 15 maana ilikuwa mbili kamili kitu kinaanza pakuliwa. Hapo napo si wajua ukifunika jungu la wali juu ukaweka mkaa wa moto ndani ule wali wa juu unatengeneza utando wa ukoko mlaini, sasa wakipakuwa wanautoa ule utando si kuugombania na mdogo wangu wa kike. Kipindi cha pili ni majira pale ilikuwa ukisikia kale ka mziki ka majira ujue muda wa kulala, mshua aliweza kuhakikisha muda huo shughuli zote zimekwisha. Kwa watani wetu wa jadi Kenya, nilikuwa mpenzi sana wa idhaa ya kiingereza hasa kulikuwa na kipindi cha chaguo la msikilizaji kikiitwa yours for the asking miaka ya 90 hadi 95 kilikuwa jmosi na jpili asubuhi saa tatu hadi saa sita mchana. Lkn kulikuwa na reggae time kila alhamis saa mbili mpaka saa tatu, mtangazaji akiwa Jeff Mwangeni aka crucial Jeff jamaa alikiendesha kipindi vizuri sana na selection zake from top of the hill! Ma irie toka kibera massive walituma sana barua kuomba nyiko. Nakumbuka kuna siku nilirekodi kipindi kizima kikimzungumzia bob marley ile kanda sijui ilipotelea mbali
 
East Africa radio jamani miaka ya 2000 mpaka 2004 sijajua km kiliendelea Sista Dread c'mon sis' ile kipindi ya reggae asylum jmosi saa tatu usiku hadi saa sita nadhani baadae mpaka saa saba, inanikumbusha dating zile tamu tamu na shemeji yenu, wakati huo chaser mayai ndo inaishia ishia umaarufu baloon inatake over, bd niko kwa bro na yeye kwa maza wake mdogo nishampeleka kwao na mie nisharudi home hapo, nakaa nje nafungulia blast ile intro ya kipindi inapiga ilikuwa very heavy utasikia tu irie man loves reggae! aah sista dread! Kile kilikuwa kipindi sijui nani alikivuruga mpaka kikaondolewa.
 
"....sasa vita imetangazwaa jaama...wananchi wote tuwe imaraaa...vijijini na mijini tusisite kuwafichua wahujumu na walanguziii...!"

wimbo huo ulikuwa ukisikika nyakati za usiku nadhani kwenye kipindi cha ....."Mikingamo"...kama sijakosea.

Sijajua walitumia kigezo gani kufuta kipindi hicho. kwamba waliridhika kuwa uhujumu uchumi na ulanguzi umekwisha nchini?
 

1. KOMBORA saa kumi na moja asubuhi kila siku
2. Salamu za Wagonjwa Mahospitalini jumapili saa tatu/nne asubuhi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…