Kumbe wewe wa juzi tu!!! Mi nilifikiri unatukumbusha enzi zile mwanzoni mwa miaka ya 80 au kati-kati ya miaka ya 70. Yaani DJJD unayemsema ameanza utangazaji na UDJ juzi tu.... wewe vipi?? Ungetukumbusha vipindi kama vile "kijaluba' kilichokuwa kinatangazwa na Abdallah Mlawa au Mikingamo kilichokuwa kikitangazwa na Juma Ngalawa ama Ahmed Kipozi (enzi zile za uhujumu uchumi). Na vingine vingi tu...... Pole sana kijana wangu (mtoto), kwa kuvifikiria vipindi vya juzijuzi tu wewe unadhani imekuwa "long time'?