Kipindi unafurahia kulipwa mshahara mkubwa wakuanzia mil 3-5, basi tambua kuna watu nchi hii wanalipwa mpaka mil 13-27 private sector

Kipindi unafurahia kulipwa mshahara mkubwa wakuanzia mil 3-5, basi tambua kuna watu nchi hii wanalipwa mpaka mil 13-27 private sector

Ukishalipwa pesa ya madafu tu utemi wako unaishia Vingunguti.

Kuna siku nilikuja likizo Bongo, nikabadili dola nyingi sana kwa matumizi yangu, mpaka likizo ilipoisha nikawa sijamaliza zile shilingi za Tanzania kutumia. Nikajisahau nikapanda nazo ndege kurudi New York City.

Nikasema ngoja nitafute Bureau de Change ya New York City inayoweza kununua hizi hela za Tanzania na kunipa USD.

Nilizunguka sana watu wanaziangalia pesa za bongo kama makaratasi tu, hawazitambui.

Na uhaba huu wa US dollar unaweza kuwa TZS ukakosa USD. Yani hela ubabe wake unaishia kwenye mipaka ya nchi sanasana utatesa nchi jirani. Ukiingia viwanja vya kimataifa proper hela ya kibongo inakuwa kama stamp tu.
Boss nisaidie laki mbili nina shida sana mpaka nahisi komwe langu linafuka moshi.
 
kha... hawa mnaowataja ni watanzania au foreigner maana ukoo wangu jumlisha na mtaa au mitaa niliyokaa hadi umri huu sijawahi kusikia jirani au ndugu analamba mamilioni kama hayo zaidi ya wabunge na wanasiasa..
 
Kulipwa hela nyingi ni kitu kimoja, halafu kuweza kuzitunza na kuzizungusha hizo pesa ni kitu kingine.

Watu wengi wanapolipwa hela nyingi, matumizi yao yanaongezeka pia.

Kwa hivyo, unaweza kukuta mtu analipwa kidogo halafu ana uwezo wa ku save na ku invest sana, wakati kuna mtu mwingine analipwa zaidi, lakini maisha yake yana matumizi mengi sana ndiyo kwanza analipa madeni, hata ku save hawezi.

Kwa hivyo, mnavyoangalia wanaolipwa zaidi, na hili nalo mkaliangalie [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Uko sahihi kabisa mkuu Kiranga
 
Back
Top Bottom