Kipindi unafurahia kulipwa mshahara mkubwa wakuanzia mil 3-5, basi tambua kuna watu nchi hii wanalipwa mpaka mil 13-27 private sector

Kipindi unafurahia kulipwa mshahara mkubwa wakuanzia mil 3-5, basi tambua kuna watu nchi hii wanalipwa mpaka mil 13-27 private sector

Yeah kuna jamaa mmoja private company alikuwa production engineer ilikuwa anavuta 10 million per month.
Kuna Jamaa pia naona kaitwa kwenye interview mara tatu, kafanya oral yakwanza walikua kama Saba akapenya, akaenda oral ya pili akakuta Kuna wengine 2 jumla wakawa 3 lkn hao wawili kwenye lile group lakwanza hawakuwemo, Sasa napo yapili kapenya, Leo kapiga interview ya 3. Mshahara ni mill 17 kwenye international company. Mungu amsimamie aisee.
 
17,000,000/- sio mchezo
 
Kulipwa hela nyingi ni kitu kimoja, halafu kuweza kuzitunza na kuzizungusha hizo pesa ni kitu kingine.

Watu wengi wanapolipwa hela nyingi, matumizi yao yanaongezeka pia.

Kwa hivyo, unaweza kukuta mtu analipwa kidogo halafu ana uwezo wa ku save na ku invest sana, wakati kuna mtu mwingine analipwa zaidi, lakini maisha yake yana matumizi mengi sana ndiyo kwanza analipa madeni, hata ku save hawezi.

Kwa hivyo, mnavyoangalia wanaolipwa zaidi, na hili nalo mkaliangalie [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mkuu mtu analipwa milioni 10+ awe na matumizi ya ovyo kiasi gani mpaka ashindwe kusave akiba kama ya anaelipwa milioni 1?
 
Mkuu mtu analipwa milioni 10+ awe na matumizi ya ovyo kiasi gani mpaka ashindwe kusave akiba kama ya anaelipwa milioni 1?
Kwani milioni 10 unaiona hela nyingi sana?

Hiyo hela inaweza kuwa si nyingi sana, ila labda wewe unatoka jamii yenye per capita income ndogo sana unaiona hiyo hela ni kubwa sana.

Miaka ya 90 nilikuwa nafanya deals fulani mjini Dar. Nikawa katika mzunguko nipo ofisi fulani hapo IPS Building.

Sasa, katika kumsubiri boss mkubwa, nikawa hapo mapokezi napiga stories na jamaa wa ofisi hiyo. Ofisi ina watu wa kila daraja, kuanzia madereva wa mishahara ya chini mpaka wafanyabiashara wakubwa.

Sasa, yakatokea mazungumzo, ukipata shilingi milioni 100 utafanya nini?

Jamaa mmoja, kati ya wale wa miashahara midogo, akasema akipata shilingi milioni 100 atastaafu hapo hapo atulie na kula maisha.

Kuna jamaa mmoja mfanyabiashara Mchaga akawa kama anamshangaa huyo aliyetaka kustaafu kwa milioni 100 sana, yani akasema utaridhika na kustaafu kabisa kwa shilingi milioni 100? Mbona hela ndogo sana na hata mtaji wa biashara kubwa haijafika?

Kwa hivyo, hela ile ile milioni 100, mtu mmoja aliiona kubwa sana kiasi cha kuweza kustaafu nayo, mwingine akaiona ndogo sana kuridhika nayo, hata mtaji wa biashara kubwa haijafika.

Inategemea na maisha gani unataka kuishi.

Kuna watu wanataka maisha ya mikopo, mijumba, mi V8 ya bei mbaya, full bata, mke wa nne, kimada wa tano, likizo za Ulaya na Marekani, ma shopping ya kimataifa sehemu za bei mbaya, ma private school ya bei mbaya, ma college ya kimataifa. Ukishaanza kuingia mambo ya kimataifa tu ndiyo utajua kuwa milioni 10 ya kibongo si hela.

Nafikiri wewe unapiga hesabu za ki local local sana ndiyo maana unaiona milioni 10 kwa mwezi hela nyingi.

Na kadiri unavyozidi kupata hela, ndivyo vishawishi vya matumizi vinavyozidi.
 
joh Dae Unafikiri mtu aliyekuwa analipwa Tshs. 1M akianza kulipwa Tshs. 10M ataendelea kuishi maisha yale yale ya awali?
[/QUOTE]
Wahindi wengi wanaishi maisha yaleyale wanaweza kujibana kuliko sisi wabongo.
 
Kuna Jamaa pia naona kaitwa kwenye interview mara tatu, kafanya oral yakwanza walikua kama Saba akapenya, akaenda oral ya pili akakuta Kuna wengine 2 jumla wakawa 3 lkn hao wawili kwenye lile group lakwanza hawakuwemo, Sasa napo yapili kapenya, Leo kapiga interview ya 3. Mshahara ni mill 17 kwenye international company. Mungu amsimamie aisee.
Yeah hata hyo ni international company mkuu wana hela sio mchezo training za nje kibao kila mwisho wa mwaka.
 
Mkuu mtu analipwa milioni 10+ awe na matumizi ya ovyo kiasi gani mpaka ashindwe kusave akiba kama ya anaelipwa milioni 1?
Hayo mambo yasikie tu..kuna jamaa yuko private company flani kama sales Director, mshahara wake ni around 9m, ila ikipita mwezi hajanipiga kizinga cha walau laki moja basi ni bahati sana...mpaka mtu unakua unamhisi jamaa labda mshirikina.
 
Back
Top Bottom