Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Unarudia kosa lile lile.
 
Huyu anajifanyisha na maswali yake ni ya upande mmoja na hataki jifunza kwa wengine. Maswali na logic zake ni za kitoto pia anashindana na hataki kuelewa wala kueleweshwa.
Sahihi kabisa,mbinu yao ni kukimbia maswali.
 
Ni sahihi bro, jamaa kaamua kujifunga ufahamu. Kesha conclude msimamo wake. Haya tutakayomueleza ni sawa na kumpigia 🐐 gitaa. Haruhusu wala hajaruhusu vitu vipya kuingia mawazo ni mwake.
 
Hskuna siku uliyo weza kuonyesha "contradictions" na ukazijengea hoja zaidi ya ku copy na ku paste,hili najua huliwezi mpaka unakufa.

Hapa unabaki kuwa muongo na mbabaishaji. Sasa usilete ubabaishaji weka hoja na ujibu hoja.
Hujathibitisha Mungu yupo.
 
Ni sahihi bro, jamaa kaamua kujifunga ufahamu. Kesha conclude msimamo wake. Haya tutakayomueleza ni sawa na kumpigia 🐐 gitaa. Haruhusu wala hajaruhusu vitu vipya kuingia mawazo ni mwake.
Kingine hata kutetea msimamo wake nako hawezi.

Huwezi kusema kwamba uwepo wa mungu ni hadithi tu pasi na kutuambia mchakato wa hadithi hizo ni upi ?

Huwezi kusema Mola hayupo kwa kuunga unga maneno bila ithibati.
 
Sahihi kabisa,mbinu yao ni kukimbia maswali.
Kuwa great thinker ni pamoja na kuruhusu mawazo mbadala. Watu wanaopinga uwepo wa Mungu wapo toka enzi na enzi. Paulo alienda Athens Ugiriki kuhubiri alikuta watu wale wanareason kuhusu Mungu na uwepo wake lakini walimpa muda Paulo kuwaelewesha. Sasa ndugu yetu Kiranga yeye toka miaka na miaka anaeshajipa majibu na maswali yake ni hayo hayo. Hataki wala haruhusu mawazo mbadala kwenye maisha yake. Mbona sisi tunaoamini kuhusu Mungu tunaruhusu mawazo mbadala, tunatafakari na kupata majibu.
 
Hujathibitisha Mungu yupo.
Nithibitishe mara ngapi ?

Hujaona aya niliyo kuwekea bali kuwepo wewe ni uthibitisho ya kuwa Mola yupo. Hili huwezi kupinga mpaka unakufa.
 
Hawawezi maana wamekariri theories za wengine bila hata kujiuliza maswali na ukiwatoa kwenye mstari wanapoteza mwelekeo kama ilivyofanya roketi ya Kichina iliyokuwa imetumwa kwenda kwenye sayari ya Mars (ilivyopoteza mwelekeo na 'kuangukia Bahari ya Hindi').
 
Asilimia90 ya atheists ni wakatoliki
Huko wanachanganywa sana! Mara "........mama wa Mungu! ".......yupo mkono wa kuume wa Mungu! Mara"......yeye ni Mungu 100% na mwanadamu 100%! Mara yeye"......mwanaye wa pekee! Na......alitufia kwa dhambi zetu! Mara ' kila MTU atauchukua mzigo wake mwenyewe! Nk
 
Mpaka sasa hakuna aliyethibitisha Mungu yupo.
 
Ndio maana nilipata wasiwasi kuhusu level yako ya kumbukumbu au kufikiri, nikuuulize vitu nilivyokutajia kuna mtu anaweza kuviunda?
kwani lazima viwe vimeumbwa?

Kuna relation gani kati ya mtu kushindwa kuunda kitu kuwe ndio sababu kitu hicho kiwe kimeundwa na mungu?

Kwasababu huwezi kuzuia treni kwa nyuzi za buibui, hiyo itathibitisha spiderman yupo?

Na hata nyinyi wenyewe mnao amini Mungu hamuwezi mka conclude kwa kuafikiana jibu moja kua ni Mungu gani miongoni mwa dini zenu ambaye ndiye muumbaji.
Nilishakujibu narudia tena kukujibu, huu ndio ulimwengu alipo Mungu ni ulimwengu usioonekana kwa macho(unlimited from time, space and matter)
unasema nithibitishe, je wewe unaweza kuthibitisha hisia/stress?
Bado hujajibu swali, kwasababu swali halijauliza kutaka kujua huu ni ulimwengu gani
Vinathibitisha kwamba Mungu yupo kwa maana hakuna anaeweza kuumba hivyo ila Mungu pekee
Bado hujathibitisha, kwasababu mtu kushindwa kuumba kitu maana yake ameshindwa na sio kitu kingine ambacho hakithibitishiki ndio kimeumba

We unaweza kubebwa na jogoo kichwa chini miguu juu? bila shaka huwezi.

Nikikuambia kuna mtu real anaitwa pazi yupo na ashawahi kubebwa kichwa chini na jogoo mdomoni, na uthibitisho wa ku prove kua tukio hilo lilifanyika na mtu huyo yupo ni kutokana na kushindwa kwako kubebwa na jogoo, hapo nitakua nimethibitisha pazi na jogoo pamoja na tukio hilo ni habari za kweli?
Kama uumbaji haukufanyika vilitokea wapi?
kwani lazima viwe na chanzo?
kuna chochote kwenye ulimwengu ulio limited to time, space and matter kinachoweza kutokea bila kuubwa?
kwanini isiwezekane?

Vyote vinathibitisha Mungu yupo na yeye pekee ndiye anayeweza kuumba hivyo
vinathibitishaje?
Kwahiyo hii ndo sababu unamkosoa Mungu?
Nakosoa dhana ya uwepo wa Mungu, kwasababu kihalisia hayupo
umewahi kujiuliza nini kilisababisha mpaka wakazaliwa hivyo? hiyo inategemeana na causes za ugonjwa husika
kwasababu ulimwengu huu hauna msimamizi mwenye ujuzi wote, muweza wa yote na mwenye upendo wote ambaye angeepusha dosari kama hizo
Nikuulize uwezo wako wa kufikiri na self control unafanana na kuku/ng'ome/mbuzi/samaki/simba?
Sijui unaposema kufikiri unalenga angle gani

Maana simba anauwezo wa kufikiri njia za kumkamata swala bila silaha na akampata

Simba ana uwezo wa kuona kwenye kiza bila msaada wa tochi

Samaki anauwezo wa kuogelea kwa muda mrefu kwenye maji

Samaki ana uwezo wa kupumua ndani ya maji

Nini kinachokufanya ujione special kwasababu umewazidi kitu fulani wanyama wakati nao kuna vingi wamekuzidi na huviwezi?


Mungu aliumba binadamu me na ke, hawa binadamu wakazaliana na kuijaza dunia.
Walikua na race gani?
Nimethibitisha Mungu yupo na nimekupa evidence ya uumbaji wake
Hujaweka evidence mahali popote
NB: KAMA UNASEMA MUNGU HAJAUMBA HIVYO VITU VYOTE UNAWEZA KUNIAMBIA VIMETOKEAJE?
Hata kama sijui vimetokaje lakini hiyo haimaanishi ni mungu
 
ndio, ni huo ulimwengu wenyewe!
Unanipa wasiwasi Mkuu kuhusiana na level yako ya kufikiri , umekiri huo ulimwengu wenyewe.

Kila kilichopo katika ulimwengu huu unaoonekana kwa macho(limited to time, space and matter) ni lazima kiwe kimeundwa na muundaji, hakuna kinachoweza kuwepo kisiwe kimeundwa na muundaji.

Katika kitu(Matter) chochote, lazima kuwe na muda(time) wa kuundwa na kuwepo na sehemu(Space) ya kukiweka/kinapostahili kuwepo.
Mfano:- Simu(Matter) imetengenezwa tarehe(Time) 12/3/1890 na kuwekwa sehemu(space) husika kwaajili ya mauzo.

"ndio, ni huo ulimwengu wenyewe!"
Kwa nukuu ya jibu lako hapo juu, umekubali kwamba kitu kinaweza kuwepo bila kuundwa.

Nakuuliza,

Katika ulimwengu huu unaoonekana kwa macho tunaoishi ulio (limited to time, space and matter) imewezekana vipi Vitu kuwepo bila kuundwa?
 
Mkuu, nakunukuu tena bado unaendelea kusema ulimwengu ulikuwepo haukuumbwa.

Hivyo vitu nilivyoviuliza kwenye post #584 ambavyo vipo katika ulimwengu unaoonekana kwa macho (limited to time, space and matter) VIMEWEZEKANA VIPI KUWEPO BILA KUUNDWA?
 
Ndio ni lazima ni lazima ni lazima viwe vimeundwa.

Kwanini?
1. Mwenye uwezo wa kuviunda ni MUNGU PEKEE
2. Kama nyie Atheist mnavyosema havijaundwa na Mungu, niambie vimetokeaje (Formation) yake/?

Nakufahamisha kuna level mbili za kuumba/kuunda
1. Uwezo wa uumbaji wa MUNGU
2. Uwezo wa uundaji wa binadamu

Uwezo wa uumbaji wa Mungu
Huu ni uwezo wa uumbaji ambao anao Mungu pekee, katika uwezo huu Mungu ameumba ulimwengu usioonekana kwa macho(unlimited from time, space and matter) kama malaika n.k na ulimwengu unaoonekana kwa macho (limited to time, space and matter) kama sayari zote, jua, mwezi na nyota zote, vimondo, hewa, madini, gas na mafuta ardhini, mito, maziwa na bahari, samaki wa kila aina, ndege wa kila aina, mimea, nafaka, miti na matunda, wanyama wa kila aina na binadamu (mpaka wewe Scars , Kiranga n.k )

NB:UWEZO HUU WA UUMBAJI ANAO MUNGU PEKEE

2. Uwezo wa uundaji wa binadamu
Huu ni uwezo ambao Mungu baada ya kumuumba binadamu akamuwekea akilini mwake, kupitia uwezo huu binadamu akaweza kuunda vitu kama magari, meli, nyumba, treni, ndege za angani, pikipiki, vitabu, peni, meza, viatu n.k

NB: KATIKA UWEZO HUU WA KIBINADAMU, HAUWEZI KUFANYIKA BILA KUTUMIA MALIGHAFI(RESOURCES) ALIZOZIUMBA MUNGU KABLA YA BINADAMU KUUBWA.

Kivipi,
Utaunda gari utatumia madini ya chuma, mafuta , waya nk as ingredients
utaunda meza utatumia mbao zitokanazo na miti aliyoumba Mung n.k

HIVYO,
Kushindwa kwa mtu kuumba kama katika level 1(Uwezo wa uumbaji wa Mungu) kunathibitisha MUNGU PEKEE NDIE ALIYEUMBA.

kwani lazima viwe na chanzo?
Ndio ni lazima viwe na chanzo, vitu vilivyo kwenye ulimwengu unaoonekana kwa macho (The limited universe to time, space and matter) vinawezaje kuwepo bila kuwa na chanzo?

kwanini isiwezekane?
Haiwezekani, kama inawezekana onesha au tuelezee inawezekanaje

vinathibitishaje?
Vinathibitisha kama ifuatavyo :-

Nakufahamisha kuna level mbili za kuumba/kuunda
1. Uwezo wa uumbaji wa MUNGU
2. Uwezo wa uundaji wa binadamu

Uwezo wa uumbaji wa Mungu
Huu ni uwezo wa uumbaji ambao anao Mungu pekee, katika uwezo huu Mungu ameumba ulimwengu usioonekana kwa macho(unlimited from time, space and matter) kama malaika n.k na ulimwengu unaoonekana kwa macho (limited to time, space and matter) kama sayari zote, jua, mwezi na nyota zote, vimondo, hewa, madini, gas na mafuta ardhini, mito, maziwa na bahari, samaki wa kila aina, ndege wa kila aina, mimea, nafaka, miti na matunda, wanyama wa kila aina na binadamu (mpaka wewe Scars , Kiranga n.k )

NB:UWEZO HUU WA UUMBAJI ANAO MUNGU PEKEE

2. Uwezo wa uundaji wa binadamu
Huu ni uwezo ambao Mungu baada ya kumuumba binadamu akamuwekea akilini mwake, kupitia uwezo huu binadamu akaweza kuunda vitu kama magari, meli, nyumba, treni, ndege za angani, pikipiki, vitabu, peni, meza, viatu n.k

NB: KATIKA UWEZO HUU WA KIBINADAMU, HAUWEZI KUFANYIKA BILA KUTUMIA MALIGHAFI(RESOURCES) ALIZOZIUMBA MUNGU KABLA YA BINADAMU KUUBWA.

Kivipi,
Utaunda gari utatumia madini ya chuma, mafuta , waya nk as ingredients
utaunda meza utatumia mbao zitokanazo na miti aliyoumba Mung n.k

HIVYO,
Kushindwa kwa mtu kuumba kama katika level 1(Uwezo wa uumbaji wa Mungu) kunathibitisha MUNGU PEKEE NDIE ALIYEUMBA.


kwasababu ulimwengu huu hauna msimamizi mwenye ujuzi wote, muweza wa yote na mwenye upendo wote ambaye angeepusha dosari kama hizo
Mungu ameumba binadamu wa kwanza ME na KE ili waijaze dunia, akawawekea uwezo katika akili wa kujitambua, binadamu hao hao kwa lifestyle yao mbovu wakasababisha matatizo duniani,

poor lifestyle in eating
poor moral lifestyle
war effects
poor medications
n.k

Kosa la Mungu ni nini hapo ikiwa alishaumba binadamu kamili, binadamu mwenyewe kwa lifestyle yake mbovu ikasababisha matatizo duniani, Mungu ana kosa gani hapo?

Unavuta sigara, unakunywa pombe, huli mlo kamili n.k Hilo ni kosa la Mungu au lako binadamu?


Nini kinachokufanya ujione special kwasababu umewazidi kitu fulani wanyama wakati nao kuna vingi wamekuzidi na huviwezi?
Mkuu wewe unaweza kutembea bila nguo mtaani kama wanyama?

Hujaweka evidence mahali popote
Ok, labda evidence nilizoziandika hapa akili yako haitaki kuelewa kwa makusudi.

Evidence ya kwanza ni wewe Scars (kwasababu wewe ni BINADAMU) umeumbwa na Mungu

Evidence zingine, unaweza kwa muda wako ukatoka nje kama ni usiku au mchana alafu ukaangalia jua, nyota, mwezi, mimea ardhini, miti na matunda, nafaka na mimea mbalimbali, mito, maziwa na bahari, samaki, ndege, wanyama, binadamu wenzio n.k

Hizo ni Evidence.

Hata kama sijui vimetokaje lakini hiyo haimaanishi ni mungu
Kwa kauli yako hiyo nahitaji kujua:-

Wewe haujui hivyo vitu vimetokeaje?
 
Kiranga naendelea kusubiri majibu ya kwenye post #584 mpaka sasa wewe na Atheist wenzio hamjatoa majibu. NA MSIPOTOA MAJIBU YA SWALI HILO HAMFAI KUWA ATHEIST

Kwanini?
Mtakuwa mmepotea kwa kusema hakuna uwepo wa Mungu ikiwa hamjui swali kwenye post #584, chanzo/formation ya ulimwengu huu unaoonekana kwa macho(limited to time, space and matter)

Formation of the followings:-
1. Jua, mwezi na nyota zote
2. Sayari zote
3. Ardhi na mimea ya kila aina
4. Madini ardhini, mafuta na gesi ardhini
5. Ndege na wanyama wa kila aina waishio nchi kavu na kwenye maji
6. Mito, maziwa na bahari
7. Upepo
8. Binadamu
9. Samaki wa kila aina
 
Unaukiza maswali irrelevant.

Nikikwambia sijui jibubla hata swali moja katibya hayo lakini najua jibubsi Mungu.

Kama ambavyo naweza kuwa sijui square root ya 2 ni nini, lakini najua si 10, utasemaje?

Unaelewa kwamba sihitaji kuelewa jibu sahihi ili kujua jibu fulani si sahihi?

Unajua kwamba sihitaji kujua umri wa mama yako mzazi ili kujua kwamba wewe hujamzidi umri?

Maswali yako ni sawa na kubishana na mimi, unaniambia wewe ni mkubwa kuliko mama yako mzazi.

Mimi nakwambia kitu hicho hakiwezekani. Kwa sababu kita cintrqdict ukweli kwamba huyo ni mama yaki mzazi.

Wewe unanijibu kwa kuniuliza umri wa mama yako mzazi ni umri gani.

Mimi nakwambia, hata bila ya kujua umri wa mama yako mzazi, ukweli kwamba huyo ni mama yako mzazi unamaliza mjadala wa nani mkubwa kati yake na wewe, huwezi kuwa mkubwa kuliko mama yako mzazi.

Bado unang'ang'ania nikupe umri wa mama yako mzazi.

Ukiendelea na ujinga huu nitashindwa kujadiliana nawe na kukuunganisha ignore list hata nisione unachoandika.

Sina muda wa kujadili upumbavu over and over again.

That is my first and last warning.
 
Mhu! Kukariri nadharia tu ni shida sana. Wewe ukiuliza swali unataka ujibiwe na linakuwa 'always relevant question'. Wengine wakiuliza, hawajaelewa na 'always wanauliza irrelevant questions au upumbavu'. Hapa tunalishwa matango pori.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…