Mkuu Meshack Asante kwa kuuliza,
Kimsingi hoja zako ni kama zinazoulizwaga mala kwa mala na Atheist, bahati nzuri wewe haukani uwepo wa Mungu kama Atheist. Hoja zako zinafika mpaka katika mada nyingine kabisa ya chanzo cha uharibifu duniani(Shetani ), lakini tusiingie huko ni mada nyingine. Lakini ngoja nikujibu briefly kwa engo hiyo, kwasababu namjibu mtu ambae sio Atheist.
HAPO MWANZO.
Mungu baada ya kuumba kila kitu katika ulimwengu unaooenekana kwa macho, Mungu alimuumba kiumbe binadamu KE na ME, viumbe hawa wawili waliumbiwa upeo/akili/utashi/maarifa/ makubwa kuliko viumbe wengine wanaoonekana kwa macho. Kiumbe huyu binadamu KE na ME wakaingiwa na uharibifu kupitia kudanganywa na (shetani), uharibifu ukaingia duniani kinyume na kusudio la Mungu tangu mwanzo, kiumbe ME na KE wakaendelea kuijaza dunia, uzao wa binadamu ukaendelea kwa uharibifu na dunia ikaendelea kuharibika, binadamu wakaendelea kufanya mambo maovu kinyume na matakwa na kusudio la Mungu. n.k
Sasa tuendelee,
1. Pamoja na kuwa Mungu ni Upendo kumekuwa na chuki From Bible kwamba watu wamekuwa wakipigana vita Israel sijui na wapi, Wamisri wameuliwa baharini( sidhani kama huu ni upendo ninaoufahamu)
Hoja yako hapa tayari inajibiwa na uharibifu ulioingia duniani, kiumbe binadamu ameendelea kufanya uharibifu mkubwa kama wa kupigana vita n.k
2.Mungu Amekuwa akibadilika, badilika kwamba Leo ni mwema Kesho si mwema, Mara anatoa uzima mara Anaua etc
Ulimwengu huu aliouumba na vyote vilivyomo ni MALI YAKE, ana mamlaka ya kufanya chochote muda wowote kamwe kiumbe binadamu hawezi kumuingilia au kumpangia Mungu nini cha kufanya.
3.Mungu wa Haki, kuna baadh ya vifungu kwa Bible vimeonesha haki ya Mungu ikienda upande wa taifa fulani, na huku wengine wakiporwa haki kwa kupigwa na kuhamishwa katika maeneo yao.
Mungu huu ulimwengu ni mali yake, so narudia kusema tena ana mamlaka ya kufanya vyovyote atakavyo yeye ikimpendeza yeye, nakupa mfano mdogo katika sayari hii dunia baba mzazi anakuwa na kiwanja na akaamua kumpa uthiri mtoto wake A kiwanja kikubwa na mtoto wake B kiwanja kidogo au asimpe kabisa akampa kitu kingine, yeye baba mzazi ndiyo mwenye mali na mamlaka ya kugawa vyovyote atakavyo.
4.Almight God( Hili ndilo haswa Contradiction inaponipataga; Mungu ni muweza wa yote ni yote kweli? au yote kwenye specific parameter? Maana kama yote; Huwa napata shida Kujiona mimi nimezaliwa ni full na mwingine amezaliwa Akiwa na mguu mmoja, na huwa naambiwa ni mipango/ mapenzi ya Mungu how comes? hii si Aina ya Ubaguzi kwamba mwingine mzima mwingine anachangamoto ya Viungo? Anyway lets say imetokea hivyo Kwanini basi Asifanye utaratibu wa kuhakikisha Mtu akizaliwa hivyo anamuweka sawa mwenye viungo dhaifu? Yeye ni muweza wa yote kama ambavyo imekuwa tukifundishwa enzi na enzi? Je kwa uweza wake hakuna namna anaweza kufanya watu wote tukawa na Uelewa mmoja kuhusu yeye? kwanini ameficha mambo kiasi kwamba Contradiction zinaibuka huku yeye kama muhusika mkuu na Muweza wa yote akiacha tukae katika Giza la kutokumjua vyema? au Kumjua kwa mashaka?
Narudia kusema HAPO MWANZO MUNGU ALIUMBA KIUMBE BINADAMU ME na KE VIKIWA KAMILI.
Uharibifu(dhambi) ulipoingia tu, ulileta na madhara hasi mengine mengi kama ifuatvyo:-
1. Uharibifu wa maadili
2. Uharibifu wa mtindo wa maisha(lifestyle)
3. Utumiaji wa pombe
4. Uvutaji sigara
5. Kemikali hatari viwandani
6. Mifumo mibovu ya kuandaa na kula chakula
7. Madhara hasi ya teknologia
8. Madhara hasi ya madawa
9. Mifumo mibaya ya ukulima na umwagiliaji kwa kutumia madawa ya kila aina ambayo yamesababisha vyakula kuwa na sumu nyingi
n.k
Hivyo, uharibifu wa baadhi ya vitu tajwa hapo juu umeathiri kwa kiasi kikubwa mwili wa binadamu na utendaji kazi wake, umeathiri kwa kiasi kikubwa homoni, seki n.k. Mtu kuzaliwa na kasoro kunasababishwa na factors nyingi ndani yake.
Madhara makubwa yaliyotokea baada ya uharibifu(dhambi) kuingia duniani kumesababishwa na kiumbe binadamu mwenyewe ikiratibiwa na mpango kazi wa shetani.
MWISHO, mkuu aonavyo Mungu au atakavyo yeye kifanyike au kisifanyike kitabaki kuwa ni maamuzi yake yeye mwenyewe. awazavyo Mungu ni tofauti na binadamu, perception zake Mungu ni tofauti na binadamu. Huu ulimwengu ni yeye ndiye akiyeuumba inabaki mikononi mwake hatima ya kila kiumbe alichokiumba. Wewe unaweza kuhoji kwa akili za kibinadamu kwanini hivi kwanini vile n.k lakini haibadilishi chochote yeye Mungu anabaki kuwa Mungu Tu.
UNACHOTAKIWA NI KUSHUKURU TU, Kwa sababu unavuta pumzi yake, chakula chake n.k