Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

kuwepo bila kuundwa na muundaji?'
Inawezekana kabisa; Muundwaji hakuwahi Kuundwa kwa taarifa nilizofundishwa (Mungu hajawahi kuumbwa) Hivyo kwa mantiki hiyo inawezekana vitu vikawepo bila muundwaji as long as muundwaji hakuwahi kuumbwa.
 
Kitu kimoja umechanganya Mkuu, nazungumzia vitu vilivyopo katika ulimwengu huu tunaoishi, ulimwengu ulio limited to time, space and matter unaaonekana kwa macho yaana gari lipo kwasababu limeundwa na muundaji, ndege ipo kwasababu imeundwa na muundaji n.k

Lengo mama ni,
Nahitaji kujuzwa kama ifuatavyo:-

Formation of the followings:-
1. Jua, mwezi na nyota zote
2. Sayari zote
3. Ardhi na mimea ya kila aina
4. Madini ardhini, mafuta na gesi ardhini
5. Ndege na wanyama wa kila aina waishio nchi kavu na kwenye maji
6. Mito, maziwa na bahari
7. Upepo
8. Binadamu
9. Samaki wa kila aina

NB: Hivyo vyote vipo katika ulimwengu unaoonekana kwa macho(limited to time, space and matter)
 
Kitu kimoja umechanganya Mkuu, nazungumzia vitu vilivyopo katika ulimwengu huu tunaoishi,
Ok NImekupata Ndugu; Ivi kuna Ulimwengu mwingine tofauti na huu tunaoishi? una vitu hivi hivi kama tulivyonavyo? Ndo izo sayari nyingine tulizojifunza kwa Geography?
 
Nimekujibu hapa, nisome kiumakini

Ni kama vile ambavyo wewe humjui SNDANGUJA.. Au unamjua?

Unaweza kuthibitisha SNDANGUJA yupo? Unaweza kuthibitisha hayupo?

Well, kama huwezi haimaanishi hayupo, kwasababu yuko kichwani mwangu ameniambia yeye ndio muumba wa huyo mungu wako na sio kweli kua mungu wako ndo kaumba huu ulimwengu

Ushahidi wa kuonesha kua kaumba ulimwengu ni kupitia na vitu vilivyomo ndani ya ulimwengu

Na kwakuthibitisha kuwa SNDANGUJA yupo kihalisia nitamuacha aandike mstari wa mwisho kwenye hii post

MIMI NI SNDANGUJA MUUMBA WAKO NAONGEA KUPITIA SCARS UNATAKIWA KUTUMA 8,000,000 KWA SCARS HARAKA IWEZEKANAVYO
Mkuu, wewe ni Atheist unajinasibu kwamba hakuna uwepo wa Mungu na hivi vitu havijaumbwa na Mungu. Well

Mimi nimekuuliza unipe formation ya hivyo vitu vilitokeaje?

Ninachohitaji unipe majibu ya swali hilo wala usiingize mifano ambayo haiendani na swali.

Mimi nakuuliza unipe formation ya hivyo vitu wewe unaniambia kuhusu SNDANGUJA, ni vitu viwili tofauti.

Nipe formation Mkuu.
 
Hayo maandishi unayotumia tu ni nadharia za watu wengine.

Au ulitunga wewe alphabet?

Tunga maandishi yako, uyatumie kwenye internet yako utujulishe kwamba hutumii nadharia za watu wengine.

Wewe ngumbaru unaelewa kwamba ukitumia internet tu umeshatumia nadharia za Einstein?
Kiranga tafuta dini ya haki mkuu utaipata na utaishi kwa amani ...acha kutetea fikra zako ulizozipangilia kwa msawazo was maneno.
 
Ok NImekupata Ndugu; Ivi kuna Ulimwengu mwingine tofauti na huu tunaoishi? una vitu hivi hivi kama tulivyonavyo? Ndo izo sayari nyingine tulizojifunza kwa Geography?
Sisi kama viumbe hai vyote vinavyoonekana kwa macho(limited to time, space and matter), tupo tunaishi katika ulimwengu huu kwa sababu Mungu ametuumba tuishi katika ulimwengu huu.

Kuhusu kama kuna ulimwengu mwingine unaoonekana kwa macho ulio (limited to time, space and matter) wenye vitu kama hivi hivi tulivyonavyo, JIBU NI KIUMBE MIMI BINADAMU SIJUI ANAJUA MUNGU PEKEE.

Kwanini?
Kwa sababu yeye ndiye Muumbaji wa ulimwengu na vyote vilivyomo.
 
JIBU NI KIUMBE MIMI BINADAMU SIJUI ANAJUA MUNGU PEKEE.
Nadhani hapa labd ndipo jamaa wanapoulizia, lakini mimi pia ndipo panaponipa utata japo nimekuwa nikiamini uwepo wake kwa Mashaka; Maana kila nilipokuwa nauliza maswali kwa waze wangu, hata sasa watoto wangu wakubwa wananiuliza, ni mambo ambayo nje ya Kuamini ni Ngumu ku justify; Ndio maana tukaambiwa Tuamini, Ndio maana kuna beliefs nyingi kweli duniani; na kila moja inajieleza kuhusu Mungu; kitu ambacho kweli kimekuwa kikinifanya niamini kwa Shida Uwepo wake.
 
Wadau, vipi kiranga ametoa jibu la formation ya vitu kwenye post #584?

Au ameendelea kuliweka kwenye ignore list? Na hata kama halijui kwanini hataki kutuambia kwamba halijui? Na kama analijua kwanini hatupi majibu?
 
Nadhani hapa labd ndipo jamaa wanapoulizia, lakini mimi pia ndipo panaponipa utata japo nimekuwa nikiamini uwepo wake kwa Mashaka; Maana kila nilipokuwa nauliza maswali kwa waze wangu, hata sasa watoto wangu wakubwa wananiuliza, ni mambo ambayo nje ya Kuamini ni Ngumu ku justify; Ndio maana tukaambiwa Tuamini, Ndio maana kuna beliefs nyingi kweli duniani; na kila moja inajieleza kuhusu Mungu; kitu ambacho kweli kimekuwa kikinifanya niamini kwa Shida Uwepo wake.
Kitu gani kina kutatiza kuhusu uwepo wa Mungu? Niulize nikujibu
 
Mkuu, wewe ni Atheist unajinasibu kwamba hakuna uwepo wa Mungu na hivi vitu havijaumbwa na Mungu. Well

Mimi nimekuuliza unipe formation ya hivyo vitu vilitokeaje?

Ninachohitaji unipe majibu ya swali hilo wala usiingize mifano ambayo haiendani na swali.

Mimi nakuuliza unipe formation ya hivyo vitu wewe unaniambia kuhusu SNDANGUJA, ni vitu viwili tofauti.

Nipe formation Mkuu.
Nimekuambia kutokua na majibu sahihi ya swali haimaanishi jibu lisilo sahihi nikipewa siwezi kulijua

Sio mungu tu ambaye nasema hayupo, kuna unicorns, Flying Spaghetti, spiderman, batman, harrypoter, teapot orbiting the sun nk. Swali lolote nitakaloshindwa kujibu kuhusiana na hao niliowataja, je itathibitisha viumbe hao wapo?

Mfano wa hoja yangu kuhusu SNDANGUJA unahusiana kabisa na hoja yako. Madai yako ni kwamba ninapaswa kukubaliana na madai yako kua ni ya kweli kwasababu sijui majibu ya vitu fulani

Kwa fact hiyo nimeweka hoja ya SNDANGUJA kwa mtindo kama wako ili nawe ukishindwa kujibu maswali hayo ukubali kua jibu langu kua SNDANGUJA ndio mungu wa kweli aliye muumba mungu wako na habari ya kwamba mungu wako ndio muumbaji wa hivyo vitu inabakia kua ni uongo
 
Mfano wa hoja yako hauna uhusiano na swali nililokuuliza.

Kwanini?
Wewe ni Atheist na unasema hakuna uwepo wa Mungu na vitu vyote nilivyoviuliza kwenye post #584 havijaumbwa na Mungu.

Mimi ninachohitaji unijuze hivyo vitu vilitokeaje(formation) si unasema havijaumbwa na Mungu. Nipe formation ya hivyo vitu. Tetea hoja yako kwa kunipa formation.
 
We ni theist unakubali kua SNDANGUJA yupo?
 
Kitu gani kina kutatiza kuhusu uwepo wa Mungu? Niulize nikujibu
SIfa za Mungu ambazo nimekuwa nikizifahamu Kwa kufundishwa kutoka kwenye Bible
1. Mungu ni upendo
2. Mungu habadiliki
3. Mungu ni wa Haki
4. Mungu ni muweza wa yote (Almighty God)
5. Mungu inasemekana Alikuja ili watu wawe na uzima, kisha wawe nao tele.

Lakini kutokana na sifa hizo
1. Pamoja na kuwa Mungu ni Upendo kumekuwa na chuki From Bible kwamba watu wamekuwa wakipigana vita Israel sijui na wapi, Wamisri wameuliwa baharini( sidhani kama huu ni upendo ninaoufahamu)
2. Mungu Amekuwa akibadilika, badilika kwamba Leo ni mwema Kesho si mwema, Mara anatoa uzima mara Anaua etc
3. Mungu wa Haki, kuna baadh ya vifungu kwa Bible vimeonesha haki ya Mungu ikienda upande wa taifa fulani, na huku wengine wakiporwa haki kwa kupigwa na kuhamishwa katika maeneo yao.
4. Almight God( Hili ndilo haswa Contradiction inaponipataga; Mungu ni muweza wa yote ni yote kweli? au yote kwenye specific parameter? Maana kama yote; Huwa napata shida Kujiona mimi nimezaliwa ni full na mwingine amezaliwa Akiwa na mguu mmoja, na huwa naambiwa ni mipango/ mapenzi ya Mungu how comes? hii si Aina ya Ubaguzi kwamba mwingine mzima mwingine anachangamoto ya Viungo? Anyway lets say imetokea hivyo Kwanini basi Asifanye utaratibu wa kuhakikisha Mtu akizaliwa hivyo anamuweka sawa mwenye viungo dhaifu? Yeye ni muweza wa yote kama ambavyo imekuwa tukifundishwa enzi na enzi? Je kwa uweza wake hakuna namna anaweza kufanya watu wote tukawa na Uelewa mmoja kuhusu yeye? kwanini ameficha mambo kiasi kwamba Contradiction zinaibuka huku yeye kama muhusika mkuu na Muweza wa yote akiacha tukae katika Giza la kutokumjua vyema? au Kumjua kwa mashaka?

5. Alimtuma mwanawe pekee ili watu wawe na Uzima, kwamba uzima wa milele, Kweli anaumba watu then awape condition(amri) wakizishindwa basi sijui wanaenda Motoni, sijui Jehanam etc.

Kweli utakuwa umenisaidia sana.
 
Hayo maandishi unayotumia tu ni nadharia za watu wengine.

Au ulitunga wewe alphabet?

Tunga maandishi yako, uyatumie kwenye internet yako utujulishe kwamba hutumii nadharia za watu wengine.

Wewe ngumbaru unaelewa kwamba ukitumia internet tu umeshatumia nadharia za Einstein?
Huna jipya. Umezoe kuwalisha watu matango pori, huwezi kunilazimisha niyale. Kwa hiyo, umeona hata wewe hujawahi ku'prove' kitu chochote mbali ya kurudiarudia tu mawazo ya Einstein uliyokariri? Bure kabisa!
 
Kama kutumia theories za watu ni kitu kibaya, mbona wewe unatumia alphabet ya watu, hujatunga yako?
 
Kiranga tafuta dini ya haki mkuu utaipata na utaishi kwa amani ...acha kutetea fikra zako ulizozipangilia kwa msawazo was maneno.
Mnaonipinga jipangeni kwanza.

Mara natumia fikra zangu.

Mara situmii fikra zangu natumia theories za watu tu.

You are all over the map like a Magellan fleet.

Hamueleweki mnataka nini.

Mradi kila kitu kulialia tu.
 
Mkuu Meshack Asante kwa kuuliza,
Kimsingi hoja zako ni kama zinazoulizwaga mala kwa mala na Atheist, bahati nzuri wewe haukani uwepo wa Mungu kama Atheist. Hoja zako zinafika mpaka katika mada nyingine kabisa ya chanzo cha uharibifu duniani(Shetani ), lakini tusiingie huko ni mada nyingine. Lakini ngoja nikujibu briefly kwa engo hiyo, kwasababu namjibu mtu ambae sio Atheist.

HAPO MWANZO.
Mungu baada ya kuumba kila kitu katika ulimwengu unaooenekana kwa macho, Mungu alimuumba kiumbe binadamu KE na ME, viumbe hawa wawili waliumbiwa upeo/akili/utashi/maarifa/ makubwa kuliko viumbe wengine wanaoonekana kwa macho. Kiumbe huyu binadamu KE na ME wakaingiwa na uharibifu kupitia kudanganywa na (shetani), uharibifu ukaingia duniani kinyume na kusudio la Mungu tangu mwanzo, kiumbe ME na KE wakaendelea kuijaza dunia, uzao wa binadamu ukaendelea kwa uharibifu na dunia ikaendelea kuharibika, binadamu wakaendelea kufanya mambo maovu kinyume na matakwa na kusudio la Mungu. n.k

Sasa tuendelee,
1. Pamoja na kuwa Mungu ni Upendo kumekuwa na chuki From Bible kwamba watu wamekuwa wakipigana vita Israel sijui na wapi, Wamisri wameuliwa baharini( sidhani kama huu ni upendo ninaoufahamu)
Hoja yako hapa tayari inajibiwa na uharibifu ulioingia duniani, kiumbe binadamu ameendelea kufanya uharibifu mkubwa kama wa kupigana vita n.k

2.Mungu Amekuwa akibadilika, badilika kwamba Leo ni mwema Kesho si mwema, Mara anatoa uzima mara Anaua etc
Ulimwengu huu aliouumba na vyote vilivyomo ni MALI YAKE, ana mamlaka ya kufanya chochote muda wowote kamwe kiumbe binadamu hawezi kumuingilia au kumpangia Mungu nini cha kufanya.

3.Mungu wa Haki, kuna baadh ya vifungu kwa Bible vimeonesha haki ya Mungu ikienda upande wa taifa fulani, na huku wengine wakiporwa haki kwa kupigwa na kuhamishwa katika maeneo yao.
Mungu huu ulimwengu ni mali yake, so narudia kusema tena ana mamlaka ya kufanya vyovyote atakavyo yeye ikimpendeza yeye, nakupa mfano mdogo katika sayari hii dunia baba mzazi anakuwa na kiwanja na akaamua kumpa uthiri mtoto wake A kiwanja kikubwa na mtoto wake B kiwanja kidogo au asimpe kabisa akampa kitu kingine, yeye baba mzazi ndiyo mwenye mali na mamlaka ya kugawa vyovyote atakavyo.

4.Almight God( Hili ndilo haswa Contradiction inaponipataga; Mungu ni muweza wa yote ni yote kweli? au yote kwenye specific parameter? Maana kama yote; Huwa napata shida Kujiona mimi nimezaliwa ni full na mwingine amezaliwa Akiwa na mguu mmoja, na huwa naambiwa ni mipango/ mapenzi ya Mungu how comes? hii si Aina ya Ubaguzi kwamba mwingine mzima mwingine anachangamoto ya Viungo? Anyway lets say imetokea hivyo Kwanini basi Asifanye utaratibu wa kuhakikisha Mtu akizaliwa hivyo anamuweka sawa mwenye viungo dhaifu? Yeye ni muweza wa yote kama ambavyo imekuwa tukifundishwa enzi na enzi? Je kwa uweza wake hakuna namna anaweza kufanya watu wote tukawa na Uelewa mmoja kuhusu yeye? kwanini ameficha mambo kiasi kwamba Contradiction zinaibuka huku yeye kama muhusika mkuu na Muweza wa yote akiacha tukae katika Giza la kutokumjua vyema? au Kumjua kwa mashaka?
Narudia kusema HAPO MWANZO MUNGU ALIUMBA KIUMBE BINADAMU ME na KE VIKIWA KAMILI.
Uharibifu(dhambi) ulipoingia tu, ulileta na madhara hasi mengine mengi kama ifuatvyo:-
1. Uharibifu wa maadili
2. Uharibifu wa mtindo wa maisha(lifestyle)
3. Utumiaji wa pombe
4. Uvutaji sigara
5. Kemikali hatari viwandani
6. Mifumo mibovu ya kuandaa na kula chakula
7. Madhara hasi ya teknologia
8. Madhara hasi ya madawa
9. Mifumo mibaya ya ukulima na umwagiliaji kwa kutumia madawa ya kila aina ambayo yamesababisha vyakula kuwa na sumu nyingi
n.k

Hivyo, uharibifu wa baadhi ya vitu tajwa hapo juu umeathiri kwa kiasi kikubwa mwili wa binadamu na utendaji kazi wake, umeathiri kwa kiasi kikubwa homoni, seki n.k. Mtu kuzaliwa na kasoro kunasababishwa na factors nyingi ndani yake.

Madhara makubwa yaliyotokea baada ya uharibifu(dhambi) kuingia duniani kumesababishwa na kiumbe binadamu mwenyewe ikiratibiwa na mpango kazi wa shetani.

MWISHO, mkuu aonavyo Mungu au atakavyo yeye kifanyike au kisifanyike kitabaki kuwa ni maamuzi yake yeye mwenyewe. awazavyo Mungu ni tofauti na binadamu, perception zake Mungu ni tofauti na binadamu. Huu ulimwengu ni yeye ndiye akiyeuumba inabaki mikononi mwake hatima ya kila kiumbe alichokiumba. Wewe unaweza kuhoji kwa akili za kibinadamu kwanini hivi kwanini vile n.k lakini haibadilishi chochote yeye Mungu anabaki kuwa Mungu Tu.

UNACHOTAKIWA NI KUSHUKURU TU, Kwa sababu unavuta pumzi yake, chakula chake n.k
 
We ni theist unakubali kua SNDANGUJA yupo?
Nasikitika kusema bado unakwepa kujibu swali Mkuu.
Kama unalijua jibu naomba uniambie/utuambie.
Kama haujui jibu pia naomba uniambie/utuambie.
 
Back
Top Bottom