Nzige Mdudu
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 1,048
- 830
Mkuu, dunia na vyote vilivyomo alivyoviumba Mungu ni mali yake, kama ni mali yake ANA MAMLAKA YA KUFANYA CHOCHOTE, sisi viumbe hatuna uwezo wa kupingana nae.Hapa ndipo Mashaka yananijaa; hata nikisiaga Wahubiri wanasema; Ivi Kwanini aamue tu vyoyote? hata vitu vinavyoumiza aliotuumba yeye mwenyewe? Believe me Hii mijadala imekuja kwasababu kumekuwa na side mbili tangu mwanzo; Kama Mungu ahata anguko angelizuia; Kusingekuwa na Mtu wa kuwaza kinyume maana angezuia pia watu kuwaza kinyume, Asingekuwepo mtu mingoni mwetu anyewaza kuuwa mtu, Infact hata ukimuua Mtu hafi etc. Maswali haya nimekuwa nikijiuliza sana; Ivi kweli Binadamu wote tunajua kwamba tunahitaji kuwa na wapendwa wetu wanafariki wengine wakiwa na Umri mdogo sana, Wanatoweka Duniani ili hali iko katika uweza wa Mungu kuwafanya waendelee kuwa nasi? Je Mungu yeye anapenda Huzuni yetu? anapenda kutuona sisi tunahuzunika kwa kupoteza watu ambao tunawapenda? Kwa kuruhusu watu wa taifa moja kupigana na kuuwa watu wa taifa jingine; kitu ambacho si kizuri, na kwa uwezo wake ambao nimefundishwa anaweza kuzuia lakini hafanya hivyo, hapa ndipo wakati mwigne napata mashaka ndugu; How comes mambo mabaya yaje asizuie? Dini kadhaa wa kadhaa zinapingana kuhusu tabia za Mungu, kwanini asifanaye namna kwamba Watu wote tumwelewe bila support ya Dini? kiasi kwamba Tunadanganywa kwamba Mungu yupo ivi au Yupo vile; Kweli napata shida
Mfano wewe ukiwa na mali, unakuwa na mamlaka ya kufanya chochote utakacho.
Hoja zako ni maswali fikirishi, kuna maswali mengine majibu yake anayo Mungu pekee(kwanini hivi, kwanini vile n.k)
Kuna maswali mengine huwezi kumuuliza baba au mama unayaacha.
Kama binadamu tunachotakiwa kufanya ni kuacha kutenda dhambi, kuyashika na kuyaishi mafundisho ya kweli ya kumtii Mungu na kutenda mema.