Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Unauliza maswali na kujiwekea mwenyewe majibu, ndio maana nakuuliza hapo utakuwa umeelewa nini?
Inategemeana na jibu utalonipa

Kwenye haya maswali utayajibu vipi ili nikuambie namna nilivyoelewa?

Maswali yangu yenyewe ni haya

Je Mungu hana chanzo au anacho?

Kama jibu litasema "sijui" maana yake utakua hujui hicho chanzo cha mungu ila hautakubali kuwa mungu hana chanzo?
 
Kwa hiyo wewe ulipokua unasema swala la mungu ni imani ulikua huelewi imani ipo katika state gani?
Nilikwambia useme jambo moja tu ambalo wewe unaliamini baada ya kupata uthibitisho ila hujafanya hivyo, matokeo yake ukaja na swali la kuniuliza kama najua kuwa imani si jambo la hakika? nikaamua kukuomba unieleweshe kuhusu hilo, ila hunieleweshi unaendelea kunipiga maswali tu.
 
Ok twende unavyotaka dogo.

Ili nijibu swali lako naomba kujua unamzungumzia mungu gani au mwenye sifa zipi?
 
Kwa hiyo uliniambia niseme jambo moja la imani kwasababu hujui imani ni hakika au lah na hivyo ulikua unasubiria jibu langu?

Katika maelezo yangu kuna sehemu yeyote nimedai kuna jambo ambalo naliamini?

Katika huu mjadala hivi ni nani kati ya mimi na wewe aliyekuja na hoja kuhusu mambo ya imani?
 
Ok twende unavyotaka dogo.

Ili nijibu swali lako naomba kujua unamzungumzia mungu gani au mwenye sifa zipi?
Ulipokua unasema mungu yupo, ulikua unakusudia mungu gani na mwenye sifa zipi?
 
Ulipokua unasema mungu yupo, ulikua unakusudia mungu gani na mwenye sifa zipi?
Humu nishajadili hadi mungu beyonce, ndio maana nakuuliza huyo mungu unayemkusudia wewe ni yupi ili nimjue niweze kujibu swali lako.
 
Ndio ungejibu sasa kuwa huna jambo unaloamini.
 
Humu nishajadili hadi mungu beyonce, ndio maana nakuuliza huyo mungu unayemkusudia wewe ni yupi ili nimjue niweze kujibu swali lako.
Kwa hiyo beyonce ndio mungu unaye muamini?
 
Nani tena aliyekupa akili na ufahamu?

Nachouliza ni kwamba tunamthibitishaje huyo Mungu yani tukakuoneshe huko aliko umuone mwenyewe au vp hasa huko kumthibitisha Mungu kunapaswa kuwa?
katika namna ambayo Ni tofauti na namna iliyofanya wew ukathibitisha kuwa yupo.
 
formation ya hivyo vyote ndio inathibitisha uwepo wa mungu?
Ni kwa vipi haithibitishi kwamba,. kama Kuna aliyeumba hiyo formation Basi pia kuna aliemuumba huyo aliyeumba hiyo formation!?
 
kila kitu Kama kipi?
 
katika namna ambayo Ni tofauti na namna iliyofanya wew ukathibitisha kuwa yupo.
Mimi sina uthibitisho bali naamini yupo bila ya shaka, sasa wewe unataka uthibitisho ndio sielewi utahitaji picha yake au umuone mwenyewe ama vp
 
Kwani Katika huu mjadala hivi ni nani kati ya mimi na wewe aliyekuja na hoja kuhusu mambo ya imani?
Ni mimi, na ndio nikasema kuwa hatuamini jambo kwa sababu ya uthibitisho.
 
Kwa hiyo beyonce ndio mungu unaye muamini?
Umeniuliza nilikuwa nazungumzia mungu gani ndio nimekujibu kuwa nimezungumzia miungu mingi hadi mungu beyonce.

Nachotaka ni wewe unitajie huyo mungu ambaye unataka nikwambie kama ana chanzo au hana chanzo, sasa sijui unakwama wapi au hautaki nikujibu?
 
Mimi sijakuuliza miungu uliyoitaja, nimekuuliza imani yako ya mungu unayemuamini ni yupi

Kama beyonce ndio mungu unayemuamini niambie tu
 
Allah(swt) ambaye ndie mungu yupo na quran tukufu inatuthibitishia juu ya uwepo wake na pia zipo dalili wazi wazi zinazo thibitisha wazi kabisa juu ya uwepo wake allah(dhul-jalal). Tafuteni elimu vijana msidanganyane kuwa mungu hayupo yupo. Msiongee bila kuwa na elimu.Elimu ni jambo la muhimu sana japo watu tunalipuuzia laiti mngekuwa na elimu sidhani kama mngekaa kupoteza muda kubishana kuwa mungu hayupo. Unataka uthibitishi soma quran na tafsiri yake yotee. Quran uthibitisho tosha kabisaa juu ya uwepo wake allah(swt).

Kumhusu sheitwani.Sheitwani ni kiumbe aliyeumbwa kutokana na moto naye alikuwa ni mchamungu kiasi cha kuambatana na malaika. Ila ilipotolewa amri yakuwa malaika wote akiwemo ibilisi ambaye alikuwa akiambatana nao kutokana na uchamungu wake wamsujudie adam walisujudu wotee isipokuwa ibilis akakata na kuingia na kibri na kusema mm ni bora kuliko adam kwa sababu umeniumba mm kwa moto na umemuumba adam kwa udongo. Kwa kile kiburi chake basi akalaaniwa na kutolewa katika rehma za allah(swt) na kuambiwa kuwa ataingia motoni siku ya qiyama.

Kisha baada ya hapo ndipo ibilis akaomba dua ya kukaa mpaka cku ya mwisho na kisha kuahidi ya kuwa atafanya kila awezalo kutupoteza na kuhakikisha tunaangamia katika moto wa jahannam pamoja na yeye.Kwasababu uwepo wetu ndoo umefanya yeye alaaniwe basi anamchukia adam pamoja na vizazi vyake na anafanya kila awezalo kuhakikisha tunaangamia. Kisha allah(swt) akatuomba sisi wotee in spiritual form na kutuweka katika kikao na kutuuliza je “mm sio mola wenu” wotee tukajibu na kusema hapana wewe ni mola wetu.

Kisha akatuonya juu ya sheitwani na kutuambia ya kuwa nitawaletea mitume huko dunia kukuonyeni na atateremesha vitabu vyake na teyar ameshafanya hvyo. Kwa hiyo kiufupu sheitwani yupo yeye ndoo source ya maovu yotee duniani yanayofanyika. Jambo la kuwa kwamba tukienda pepo napo watu watakuwa wanatenda maovu hilo halipo kwa sababu allah(swt) anasema ndani ya quran ya kuwa “hatasikia humo upuuzi wala uongo”.

Kwahiyo wazi kabisa mwisho wa dhambi ni hapa hapa duniani.Allah(swt) kwahiyo rai yangu ni kwamba tusomeni badala ya kukaa na kubishana mungu yupo au hayupo.Soma kwanza alafu kisha ufanye uamuz uamini au la!.Na ikiwa hutaamini jua makaz yako ni motoni na allah(swt) atuepushe sotee ameen
 
Mimi sijakuuliza miungu uliyoitaja, nimekuuliza imani yako ya mungu unayemuamini ni yupi

Kama beyonce ndio mungu unayemuamini niambie tu
Mungu anayemuamini mimi hana chanzo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…