Kiranga anatoa sadaka na anaamini stori za majini lakini haamini uwepo wa Mungu

A
 
Kwa nini A?

Huoni kwamba utamkosesha mtoto uhuru wa kuchagua mwenyewe kama anataka kunywa maziwa au sumu?

Unaelewa kwa mujibu wako, Mungu wako alikuwa na uchaguzi huo huo akachagua B?
Lakn kumbuka uliniambia kuwa huyo mtoto uwezo wake wa kuchagua ni mdogo, na haukumwambia kwamba akinywa sumu atakufa! kwahiyo yeye atakunywa hata sumu maana hajui kuwa inaua hiyo inamaanisha mfano wako hauendani na tunachojadili...maana sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu tuna ufahamu na tulipewa uhuru wa kuchagua kufuata mema au mabaya tofauti na mtoto anaefuata kila kitu anachoambiwa na baba yake.
 
Kama na sisi tunaweza kuchagua mabaya, na sisi uwezo wetu ni mdogo.

Sasa, kwa nini Mungu aliruhusu mabaya yawepo wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kuwepo?
 
Kama na sisi tunaweza kuchagua mabaya, na sisi uwezo wetu ni mdogo.

Sasa, kwa nini Mungu aliruhusu mabaya yawepo wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kuwepo?
Unaposema sisi unamaanisha wewe na nani?!! na shetani au? wewe kama umechagua kupinga Ufalme wa Mungu usidhani na mimi nitapinga maana umejuaje kila mtu hapa duniani amechagua mabaya sio mema?


Unaposema angeumba ulimwengu ambayo mabaya yasingikuwepo ndio tunarudi pale pale unataka kufanya Mungu aonekane ni Dictator kwa aonekane amewanyima uhuru kama madai ya uwongo aliyoyaanzisha shetani.
 
Dude,

Mungu wako mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.Umedanganywa kwamba yupo.

Angekuwepo, kusingewezekana kuwa na mabaya ya aina yoyote.

Mabaya kuweza kuwepo ni uthibitisho kwamba huyo Mungu hayupo.

Unaelewa hiyo mantiki ndogo kabisa?
 
Yeye kujua hatima yako inaharibu uhuru uliyonao ambao ndio hukupeleka kwenye hiyo hatima yako mwenyewe?
 
Ukute ametumia hilo tamko pasi na kujua maana yake. Hawa watu wana udhaifu mkubwa sana wa kujua maana za maneno.
Yupo bwege mwingine nayeye kasoma soma mythologies za zechariah sitchin kuhusu viumbe Anunnaki na ancient civilisation basi kajaa bila kujua maana kaingizwa chaka basi anajikuta yeye ni bonge la atheist,nimemsoma kwenye uzi mwingine nimekuta anazungumzia kuhusu Tanzania kubarikiwa rasilimali lukuki.
Nikajiuliza hivi hawa jamaa hawana akili unakataa uwepo wa Mungu huku unamkiri kwa maneno na pengine kwa vitendo.
Kweli wana udhaifu wa kujua maana ya maneno

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Na ni lazima yawepo manuizi moyoni mwa mtoa sadaka kwenda kwa anayepokea sadaka

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Kama Mungu hawezi kuwepo,basi tuambie anaweza nini?
Basi anaweza akawepo sio?

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo Mungu alimuumba makusudi mwanadamu aliyejua vyovyote vile ataasi? So aliumba makusudi kiumbe ambacho hakiko perfect ilikihasi halafu akiadhibu?
Yes Mungu alimuuumba makusudi kabisa binadamu na yote aliyofanya amefanya kwa makusudi kabisa kwa kadri alivyopenda yeye na anafanya na ataendelea kufanya kwa kadri ya kudra zake yeye peke yake.
Ndio anavyotaka hivyo kuwa ukitenda vyema atakubariki na ukitenda makosa atakuadhibu tu.
Huyo ndio Mungu yupo pale hayupo na hayupo pale yupo.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Kwani yupo au hayupo? Tuanze hapo kwanza.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote hayupo.

Dhana ya uwepo wake inajipinga yenyewe, pia inapingwa na ulimwengu tunaouona.
 
Ulimwengu ambao hauruhusu mabaya unafananaje? hebu tuelezee.
Hauwezekani kuwa na mabaya, hauna magonjwa, hauna majanga ya asili, hauna njaa, hauna uwezekano wa watu kufanya dhambi na hivyo hauna adhabu, hauna mtu kupata asichokitaka na kukosa anachokitaka na hauna contradiction katika yote hayo.

Fikiri kidhahania, usifikiri kwa kuwa limited na ukimwengu uliopo.

Mungu alishindwa kuuumba ulimwengu huo?
 
Kama Mungu hawezi kuwepo,basi tuambie anaweza nini?
Basi anaweza akawepo sio?

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
Mungu ni dhana tu, hayupo kiuhalisia. Hawezi chochote zaidi ya kufikirika, kwa sababu hayupo nje ya dhana.

Kama unabisha, thibitisha Mungu yupo nje ya dhana tu.
 
Mpaka sasa pia hujathibitisha Mungu hayupo.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
Uwepo wa mabaya katika ulimwengu huu ni uthibitisho kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Huyo Mungu ni wazo la kufikirika tu, hayupo kiuhalisia.

Lakini sitegemei uweze kuelewa hilo.
 
Na ni lazima yawepo manuizi moyoni mwa mtoa sadaka kwenda kwa anayepokea sadaka

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
Huu mjadala wa sadaka kimsingi ni mjadala wa watu wenye mawazo finyu wanaodhani dini yao inahodhi ukarimu na watu wenye mawazo mapana yanayokubali kwamba huhitaji kuamini dini au Mungu kuwa mkarimu.

Sasa mje mniambie tena mtu asiyeamini Mungu hawezi kuwa mkarimu, kwa sababu neno karimu lina mzizi wa kiarabu.

Wakati mimi hata sijaandika kiarabu hapa.

Freaking ridiculous religious arrogance..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…