Kwani Mungu ameshindwa kupika wali ulioiva bila kupika wali mbichi?
Kwa nini uhuru uwe muhimu zaidi ya kuondoa uwezekano wa mabaya?
Nikisema wewe ni baba, una mtoto wako mchanga uwezo wake wa kuchagua ni mdogo, anaweza kushawishika kuchagua kitu kibaya badala ya kizuri.
Situation A.
Una uwezo wa kufanya nyumba yako iwe na maziwa tu, mtoto akinywa chochote apate virutubisho vya maziwa.
Situation B
Na pia, una uwezo wa kuweka maziwa na sumu sehemu nyiingi nyumbani kwako, mtoto wako awe na uhuru wa kuchagua maziwa ama sumu. Akinywa maziwa aishi, akinywa sumu afe.
Hapo unatakiwa kuchagua A au B.
Wewe kama baba mwenye uwezo huo, ujuzi huo na mapenzi kwa mwana wako, utachagua A au B hapo?