Kiranga na jamaa zake wanaweza wasionekane kwenye thread mbalimbali lakini uzi wowote unaomsifia Mungu huwakosi

Kiranga na jamaa zake wanaweza wasionekane kwenye thread mbalimbali lakini uzi wowote unaomsifia Mungu huwakosi

Huwa najiuliza sana kwanini huyu Kiranga na wengine wengi huwa wanajitokeza kwenye uzi wowote ule unao muhusu Mungu na lengo ni kupinga uwepo wake.

Haijarishi hujamu mention dk1 ni nyingi hawa hapa.

Ni kwamba wakuu msipopita kimyamya tu mkatuacha sisi tunaokubali na kuamini uwepo wa Mungu tuendelee na mjadala huwa mnapungukiwa kitu?

Huyu Bush Dokta Kaja kwa kasi sana kwenye kupinga uwepo wa Mungu.Ninaomba mwe mnatuchie mjadala sisi tunao amini uwepo wa Mungu asee huwa mnatuvuruga sana maana mnajua wazi majibu hatuna hivi ni vitu vya Imani sasa imani utaithibitisha vipi? Ni sawa na kuambiwa nenda kaniletee upepo.

RAMADHAN KAREEM
Kiranga ndio Ibilisi tunaemsoma kwenye vitabu vya dini.
 
Kazi ya kupinga uwepo wa Mungu ni kazi endelevu.

Kila siku wanazaliwa watoto wapya wanapewa mafundisho ya uongo kwamba Mungu yupo.

Sasa tutaridhika vipi tukae kimya ikiwa uongo huu unafundishwa kila siku?

Ulishaona makanisa yanaridhika yanasema tusifundishe tena watu habari za uongo huu wa kuwapo Mungu?

Ulishaona misikiti inaridhika na kusema sasa tumeridhika kusema habari za uongo kwamba Mungu yupo?

Sasa kama hawa wasema uongo wa makanisani na misikitini na wengine wengi kama wao hawaridhiki kusema uongo, unapata wapi uhalali wa kutuambia sisi tunaonyoosha mambo na kuhoji uongo huo turidhike?

Jibu hoja, acha kushambulia watoa hoja.

Kushambulia mtoa hoja badala ya kujibu hoja ni logical fallacy.

Ni tabia ya watu wasio na hoja.

Ni ad hominem logical fallacy.

Unajua logical fallacy ni nini?
Muda mwingine naona kubishana na hawa watu wa dini kunaharibu afya yangu ya akili

Kwanza hata wakimuamini huyo mungu hawamfanyi awepo

Sema na wewe una hoja, tukinyamaza hii falsafa itaenea vipi?

Kuwa atheist kazi sana.
 
IMG-20250304-WA0000.jpg
 
Muda mwingine naona kubishana na hawa watu wa dini kunaharibu afya yangu ya akili

Kwanza hata wakimuamini huyo mungu hawamfanyi awepo

Sema na wewe una hoja, tukinyamaza hii falsafa itaenea vipi?

Kuwa atheist kazi sana.
Mkuu,

Ni kweli kuna watu wengine ukibishana nao unaweza kuharibu afya yako ya akili.

Na mimi ninatumia sana ignore list.

Lakini pia, sitaki kuitumia kirahisi, kuna watu wana engage vizuri tu, hata kama ni kwa bias na ujinga, lakini kama mazungumzo hayajafika kwenye disrespectful discourse hapo tunaelezana tu.

Haya mambo yameelezwa kwa miaka mingi sana. Epicurus aliandika Epicurean paradox miaka mingi kabla ya kuzaliwa Yesu. Epicurus alizaliwa takribam miaka 341 kabla ya Yesu. Na yeye wala hakuwa wa kwanza kufikiria hivyo, mawazo hayo yalikuwapo maelfu ya miaka kabla ya Epicurus.

Na hata huku Afrika watu walikuwa na imani nyingi sana tofauti kabla ya kuwapo Uislamu na Ukristo. Na wengine hawakuamini Mungu kabisa. Tatizo watu hata historia hawasomi.

Sasa, kujifunga kwenye imani fulani tu ni ushamba. Hata historia yetu Afrika ya kuwa very diverse kwenye mambo ya imani tunaifuta, na kuweka imani chache tu, na kuwafanyia censorship watu wasioamini Mungu.

Tena kivivu na kijinga sana tu.
 
Huwa najiuliza sana kwanini huyu Kiranga na wengine wengi huwa wanajitokeza kwenye uzi wowote ule unao muhusu Mungu na lengo ni kupinga uwepo wake.

Haijarishi hujamu mention dk1 ni nyingi hawa hapa.

Ni kwamba wakuu msipopita kimyamya tu mkatuacha sisi tunaokubali na kuamini uwepo wa Mungu tuendelee na mjadala huwa mnapungukiwa kitu?

Huyu Bush Dokta Kaja kwa kasi sana kwenye kupinga uwepo wa Mungu.Ninaomba mwe mnatuchie mjadala sisi tunao amini uwepo wa Mungu asee huwa mnatuvuruga sana maana mnajua wazi majibu hatuna hivi ni vitu vya Imani sasa imani utaithibitisha vipi? Ni sawa na kuambiwa nenda kaniletee upepo.

RAMADHAN KAREEM
Hiyo kisaikolojia maana yake ni kwamba Awa amini kile wanacho.kiamini..
KUNA MAKUNDI MATATU
1)WANAO AMINI MUNGU YUPO
2)WASIO AMINI KUWA MUNGU YUPO
3)WANAO JUA KUWA MUNGU YUPO...
Katika haya makundi 3 kundi la wapumbavu ni ilo la kwanza na kundi la pili ni kundi la watu walio anza kutumia akilli zao vizuri ...na kundi la 3 nilile watu wenye akili kuliko kundi la 1 na la 2
 
Akina kiranga ni wazee wa theory za binadamu alikuwa nyani, hata sisi huko shule ya msingi tulisoma vitabu vya historia ya binadamu kubadiika kutoka kuwa nyani, lakini tulivyokuwa na ufahamu wetu tumechanganya za kuambiwa na za kwetu wenyewe.
 
Mkuu,

Ni kweli kuna watu wengine ukibishana nao unaweza kuharibu afya yako ya akili.

Na mimi ninatumia sana ignore list.

Lakini pia, sitaki kuitumia kirahisi, kuna watu wana engage vizuri tu, hata kama ni kwa bias na ujinga, lakini kama mazungumzo hayajafika kwenye disrespectful discourse hapo tunaelezana tu.

Haya mambo yameelezwa kwa miaka mingi sana. Epicurus aliandika Epicurean paradox miaka mingi kabla ya kuzaliwa Yesu. Epicurus alizaliwa takribam miaka 341 kabla ya Yesu. Na yeye wala hakuwa wa kwanza kufikiria hivyo, mawazo hayo yalikuwapo maelfu ya miaka kabla ya Epicurus.

Na hata huku Afrika watu walikuwa na imani nyingi sana tofauti kabla ya kuwapo Uislamu na Ukristo. Na wengine hawakuamini Mungu kabisa. Tatizo watu hata historia hawasomi.

Sasa, kujifunga kwenye imani fulani tu ni ushamba. Hata historia yetu Afrika ya kuwa very diverse kwenye mambo ya imani tunaifuta, na kuweka imani chache tu, na kuwafanyia censorship watu wasioamini Mungu.

Tena kivivu na kijinga sana tu.
Huyu kiranga msimwamini ana uwezo mdogo sana wa uelewa ...ushahidi ninao ila kanipiga ban ya ignore list
 
God exist

Atheists ni watu ambao bado wapo katika hatua za Kati za ukuaji wa ufahamu.

Kitu Ambacho hakipo ni dini but not God
Upo Sahihi kwenye Atheists kuwa wapo daraja ya kati maana kuna madaraja 3 ...mawili yanayo sema mungu yupo na moja linalo kanusha .....kati ya hayo madaraja lililo la wapumbavu kabisa ni mojawapo ya hayo mawili yanayo sema mungu yupo...na daraja la Atheists ni lenye watu wenye akili akili siyo wapumbavu kivileee ila lipo daraja la watu wenye akili kamili na timamu katika kupambanua mambo nalo linasama MUNGU YUPO NA AIWEZEKANI KUWE HAKUNA MUNGU
 
NISAIDIE JIBU LA HILI SWALI "JE SHETANI YUPO?"

Shetani ni nini? Watu tofauti wanaweza kutafsiri neno "Shetani: kwa maana tofauti.

Kuna watu wanamuita Vladinir Putin Shetani. Hivyo, kwa muktadha wa definition yao, Shetani yupo.

Lakini, mimi niweke muktadha wa kidini tunaouzungumzia hapa.

Kwa mujibu wa mapokeo ya kidini, mfano Ukristo, Uyahudi na Uislamu,
Shetani ni sehemu ya hadithi ile ile ya uongo ya Mungu kuwapo.

Kumetungwa sehemu mbili, Mungu akiwakilisha mazuri, na Shetani akiwakilisha mabaya.

Wote hawa ni wahusika wa hadithi za kutungwa na watu.

Ukisoma dini utakuta hizi habari za mnyukano wa Good and Evil zilikuwapo zamani sana tangu enzi za Zoroastrianism. Wangapi wamesoma Zoroastrianism hapa hata kwa dondoo tu?

Hizi habari za Mungu na Shetani ni jitihada za watu kupambana na hali zao tu.

Watu waliona mabaya mengi katika jamii, wakajua kuwa hawa wanajamii kuwa control kwa sheria za watu ni kazi sana, basi viongozi wakaona ngoja tuseme kuna sheria kubwa zaidi ya sheria ya watu, tuseme kuna Mungu, na Mungu kaweka sheria yake, na kuna shetani mbaya anawashawishi mfanye mabaya. Muepukeni Shetani msifanye mabaya, fuateni sheria za Mungu.

Hizi ni hadithi za kutungwa na watu kujaribu ku control watu.

Ndiyo maana ukichunguza utaona sehemu zilizokuwa na dola zenye nguvu ndizo sehemu zilizoanzisha na kueneza dini kubwa. Ubabeli, Misri, Uchina, mpaka Ugiriki na Roma.

Dini ni nyenzo ya kutawala watu. Ilikuwa lazima dola zitumie dini na idea ya Mungu/Shetani iki kutawala watu. Kwenye dola kama za Misri ya kale ilifikia mpaka Mfalme ndiye akikuwa Mungu katika dini zao.

Tatizo kadiri muda ulivyoenda kumekuwa na manipulation nyingi zaidi sana za kisiasa zimeingia katika hizi hoja.

Kwa hivyo, kujibu swali lako, Shetani naye hayupo, ni sehemu ya hadithi ile ile ya uongo ya Mungu kuwapo.

Kuna mtu aliniambia mimi ni Freemason, muabudu Shetani. Kwa kuwa napinga uwepo wa Mungu.

Na pia naona hofu hii ipo kwa watu wengi hawa wanaoanzisha hizi mada za "Kwa nini mnapinga sana uwepo wa Mungu?". Wengine wanafikiri tunapinga uwepo wa Mungu jwa sababu tunamtetea Shetani.

Huyo mtu aliyeniambia mimi Freemason nilimuel8misha kitu kuhusu Freemasons. Nilimuambia hivi, wewe unayeamini Mungu uko karibu zaidi na Freemasons kuliko mimi.

Yani ni hivi, ili kuwa Freemason, moja ya sharti unalotakiwa kutimiza ni kuwa na imani fulani ya Mungu au miungu. Ukiwa atheist huamini kabisa Mungu huruhusiwi kuwa Freemason.

Kwa hiyo, kama kuna ntu ana hofu kwamba mimi soecifically nipo hapa kama mtu wa "Kanisa la Shetani" kueneza neno la Shetani, mimi sipo huko.

Siamini si tu Mungu, sababu ike ike inayonifanya nisikubalinuwepo waMungu ndiyo inayonifanya nisikubali uwepo wa Shetani, pqmoja na uchawi, malqika, majini.

Sio tu sikubali uwepo wa Mungu.

Sikubali supernatural phenomena yote.

Ambayo inajumuisha Mungu, Shetani, majini, malaika, vibwengo, popobawa, uchawi na vitu vyote vinavyofanana navyo.
 
Akina kiranga ni wazee wa theory za binadamu alikuwa nyani, hata sisi huko shule ya msingi tulisoma vitabu vya historia ya binadamu kubadiika kutoka kuwa nyani, lakini tulivyokuwa na ufahamu wetu tumechanganya za kuambiwa na za kwetu wenyewe.
Wewe hata huko shule hukuelewa ulichofundishwa.

Au labda hata hao walimu waliokufundisha hawakuelewa wanachotakiwa kufundisha.
 
Hili ni jukwaa huru Kila mmoja anao Uhuru wa kukubaliana ama kutokukubaliana na Jambo Fulani as long as hatukani mtu wala kumkosea heshima. Just ignore them kama unaona wanachoandika hakiendani na wewe
😄😄😄Though umeonyesha hawa watu wakikaza kukushawishi unaweza kushawishika
 
Back
Top Bottom