NAGAMAHONGA
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 11,131
- 9,301
Kwani huwaoni wakizaliwa au huna mke wala kimada?Kwa mtazamo wako,binadamu walitoka wapi mkuu?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani huwaoni wakizaliwa au huna mke wala kimada?Kwa mtazamo wako,binadamu walitoka wapi mkuu?
Takibiir.Nimecheka sana, yaani umeibuka less than 10 minutes, anyway I agree with you, the right to freedom of opinion and expression.
Tatizo Kuna watu na dini zao hata kichwa wanakukata.
Mbona huyo ni mtani wake? Acha wachangamshe jukwaa. Mi sioni kama kuna ubaya kwani hata huyo mmoja aliyeitwa ameriakti positivly.Kuanzisha mada kwa ajili ya mtu mmoja tu aidha ni chuki,shari uadui na au lipo jambo jifichi.
Dini zimeanza kupingwa miaka mingi labda akitaka kutumia uchangamfu na umaarufu wa kiranga kuukuza Uzi wake.Mbona huyo ni mtani wake? Acha wachangamshe jukwaa. Mi sioni kama kuna ubaya kwani hata huyo mmoja aliyeitwa ameriakti positivly.
Wewe jomba una busara ile laana.JF ni public forum, kila mtu ana uhuru wa kuchangia mada anayoitaka.
Na kila mtu ana mada zake pendwa, wengine mada za michezo hawakosi, wengine mada za siasa hawakosi. Na sisi hizi ndizo mada zetu, tatizo lako nini?
Usiulize kwa nini Kiranga anachangia sana mada hizi. Huu ni uhuru wangu. Jibu hoja.
Ukiuliza sana swali hilo utakuwa kama unafanya censorship hawa wakina Kiranga wasiandike.
Mimi hata sianzishi mada mkuu. Mada wanaanzisha wengine. Nyingine wala sizioni watu wananiita nichangie, wanapenda kujua mawazo yangu.
Tatizo lako nini?
Hupendi kuona mawazo tofauti na yako?
Kubali tu kuwa kuna watu tofauti na wewe.
Mbona sisi tumezungukwa na watu wanaoamini Mungu na kila siku tunalazimishwa kusikia habari za Mungu, ambazo tunaona ni uongo tu, na bado tunadunda tu?
Acha kufanya censorship.
Waachie watu waandike wanavyotaka.
Wewe pia unaruhusiwa kuandika unavyotaka hatujawahi kukuzuia kuanzisha au kupost mada zako.
Kwa nini umesema hivyo MamaSamia2025 ?Wewe jomba una busara ile laana.
Ndo manake. Si unaona tuko tayari uk. wa 4 na bado unaendelea kuchangiwa?Dini zimeanza kupingwa miaka mingi labda akitaka kutumia uchangamfu na umaarufu wa kiranga kuukuza Uzi wake.
Una uwezo mkubwa wa kujibu kitu kwa hekima hata kama ni cha kukera. Mko wachache wenye uwezo huo.Kwa nini umesema hivyo MamaSamia2025 ?
Kuna wengi wamejificha kwenye kichaka cha kumwamini Mungu lakini umbea wao, ufiraji wao, umalaya wao........Kwenye nyuzi zangu alijitokeza tokeza, "nikampasua kwa moto na nyundo ivunjayo miamba vipande vipande huyo shetani aliye nyuma yake." Amechukia sana mpaka ameamua kuniweka kwenye ignore list 🙂. Namuombea Mungu amhurumie na kumuokoa. Tumsamehe tu bure, hajui alitendalo. Hata sisi kabla Yesu hajatuokoa, tulikuwa kama yeye.
Na wewe tumia nyundo hii:
Yeremia 23:29 BHN
Neno langu ni kama moto; ni kama nyundo ipasuayo miamba vipandevipande.
Asante sana. Si rahisi lakini najitahidi.Una uwezo mkubwa wa kujibu kitu kwa hekima hata kama ni cha kukera. Mko wachache wenye uwezo huo.
Si kweli,hawa ni Wapingaji sio WanafunziLabda wanachungulia kama kuna neno la kuwaponya kwenye wanachokiamini bado hawakipati.
Umesema huna ufahamu kuhusu origin ya watu na viumbe wengine na bado unabisha kuhusu uwepo wa Mungu, kwa nini usiseme kwamba huna ufahamu pia kuhusu uwepo wa Mungu badala ya kuhitimisha kwamba Mungu hayupo? wee jamaa chenga sana.Kwanza kabisa hakuna binadamu. Unless one of your ancestors aliitwa Adam.
Neno "binadamu" lina mzizi wa ki etimolojia wa "bin Adam", kusema kwamba watu wote ni uzao wa Adam.
Huyo Adam hakuna ushahidi kwamba alikuwapo. Wasomi wa Biblia ya kiyahudi (Old Testament) wanasema huyo Adam hakuwapo, hiyo ni hadithi yabkuelezea mabadiliko ya jamii ya Kiyahudi tu.
Kasome kitabu cha Dr. James Kugel aliyefundisha masomo ya Biblia mpaka Harvard kinaitwa "How To Read The Bible : A Guide To Scripture Then And Now". Professor Kugel kaandika vizuri sana kuhusu habari hii.
Sasa, unless baba yako au ancestor wako mmoja anaitwa Adam, na wewe ni bin Adam kwa maana ya kwamba ni mtoto wa huyo baba/ babu anayeitwa Adam, jina "binadamu" ni misnomer.
Pili, kwa kujibu swali la "watu walitoka wapi", naweza kuwa sina jibu kamili la watu walitoka wapi lakini nikajua kuwa hawakuumbwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.
Swali la watu walitoka wapi ni kubwa, ni gumu, linahitaji maelezo mengi, maelezo ya kitaalamu, utaalamu ambao pengine sina, na hata ule ambao ninao mwingi una controversy, na mimi sipendi kujadili masuala argumentative ambayo siwezi kuyatatua kwa truth table.
Hapa kuna ujinga mwingi, kuna wajinga wengi, watu hawajui evolution tu ni nini, na mimi sina haja wala appetite ya kutoka kwenye reli ya mada yangu ya msingi.
Mada yangu ya msingi ni hii.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.
Swali la watu walitoka wapi si langu. Kwa sababu sijawahi kudai kuwa najua watu walitoka wapi. Hili ni swali la kila mtu.
Swali langu ni hili.
"Unasema Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo, unahakikishaje Mungu huyo si chanzo cha maisha ya watu?".
Swali hili ndilo langu. Kwa sababu linauliza kuhusu Mungu ambaye mimi nimesema hayupo.
Kama unaniuliza swali hilo, niko tayari kukujibu.
Lakini swali la mtu kaanza vipi naweza kukutafutia vitabu vya wanazuoni tusome wote tuelezane hapa aya kwa aya. Sitaki kukupa jibu kwa sababu hata mimi mwenyewe najaribu kujifunza zaidi kuhusu swali hili.
Lakini, kabla ya kujua jibu sahihi najua jibu si Mungu.
Umenielewa?
Unaniuliza uelewe au unanisimanga?Umesema huna ufahamu kuhusu origin ya watu na viumbe wengine na bado unabisha kuhusu uwepo wa Mungu, kwa nini usiseme kwamba huna ufahamu pia kuhusu uwepo wa Mungu badala ya kuhitimisha kwamba Mungu hayupo? wee jamaa chenga sana.
Kama kujua origin ya watu kumekutoa jasho, nilitegemea uamini uwepo wa nguvu kubwa zaidi ambayo inaweza kuhusika na origin ya watu ambayo huijui, ambayo ndo tunaita Mungu......naona mdogo mdogo umeanza kuelewa.Unaniuliza uelewe au unanisimanga?
Naweza kusema Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote hayupo kwa sababu ya conyradiction ikiyopo katika Epicurean paradox.
Unaelewa Epicurean Paradox ni nini?
Kwani nikiulizwa hivi.
What is the square root of 4?
Nikaajua kuwa the square root of 4 must be less than 4.
Siwezi kujua kuwa 10 haiwezi kuwa square root of 4 kabla hata sijajua square root of 4 ni nini, kwa sababu 10 ni kubwa kuliko 4 na hivyo haiwezi kuwa square root ya 4?
Kwani siwezi kujua jibu hili si sahihi, wakati natafuta jibu sahihi, bila kujua jibu sahihi?
Mbona unafanya logical non sequitur fallacy?
Hapana,Kama kujua origin ya watu kumekutoa jasho, nilitegemea uamini uwepo wa nguvu kubwa zaidi ambayo inaweza kuhusika na origin ya watu ambayo huijui, ambayo ndo tunaita Mungu......naona mdogo mdogo umeanza kuelewa.
Hapana ni mtu mwenye akili/ upeo mkubwa sana..nilishangaa alivyosema amesoma Muhimbili na Tambaza..nilidhani toka Msingi amesoma huko US..ingawa hilo la kutokuamini uwepo wa Mungu, hatupo pamojaKiranga ni psychopath..ni mgonjwa wa akili. Nimekaa paleee.