Kiranga na jamaa zake wanaweza wasionekane kwenye thread mbalimbali lakini uzi wowote unaomsifia Mungu huwakosi

Point uliyoiruka ni kwamba agnostic wanasema hakuna njia ya kuweza kujua kuwa Mungu yupo au hayupo, kwahiyo theist akisema Mungu yupo agnostic atahoji amewezaje kujua? Na atheist akisema huyo Mungu hayupo pia agnostic atahoji amewezaje kujua?

Chengine ni kwamba si kuwa hakuna uthibitisho wa kuwepo Mungu tu bali pia hadi sasa hakuna ushahidi uliyoweza kuonyesha kutokuwepo kwa huyo Mungu, najua suala la uthibitisho linakupa shida kulielewa.
Kitu ni either kipo au hakipo.

Sasa wewe unakataa kwamba Mungu hayupo halafu bado umeshindwa kumthibitisha yupo.

Sasa unataka nini?
 
Hoja haijengwi kwa kusema 'wenzetu wanafanya, basi na sisi tufanye,' bali kwa kuleta uthibitisho wa wazi wa msimamo wako. Je, unaweza kuthibitisha kwa mantiki kuwa Mungu hayupo badala ya tu kusema kwamba kuna mafundisho yanayodai yupo?
Nithibitishe mara ngapi?

Unanifuatilia?

Mara ngapi nimeongelea Epicurean Paradox na The Problem of Evil?

Umefuatilia Epicurean Paradox na The Problem of Evil?

Umeelewa hoja zilizomo katika mantiki ya maswali yanayoibuliwa na the problem of evil?
 
Nikijua kwamba square root ya 4 ni lazima iwe ndogo kuliko 4, mtu akiniambia square root ya 4 ni 10, nashindwa kujua kwamba square root ya 4 si 10, kwa sababu 10 ni kubwa kuliko 4, hata kabla sijajua square root ya 4 ni nini?

Siwezi kujua jibu hili si sahihi, kabla ya kujua jibu sahihi ni lipi?

Nikijua kwamba hoja ya kuwapo Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ina contradiction kubwa sana ya the problem of evil, na hivyo Mungu huyo hayupo, nashindwa kujua kwamba Mungu huyo, kwa kuwa hayupo, hawezi kuwa chanzo cha uhai, kwa sababu hayupo, hata kabla sojajua chanzo cja uhai ni nini?

Juma, mwanamme mwenye miaka 30 leo, ambaye hamjui mama yake mzazi kibaiolojia ni nani, anashindwa kujua kuwa Jane, binti mchanga mwenye miezi 6 leo, hawezi kuwa mama yake mzazi wa kibaiolojia Juma, kwa sababu Jane ni mdogo sana kwa Juma, na mama yake Juma anatakiwa kuwa mkubwa zaidi ya Juma?

Juma anashindwa kujua kuwa Jane hawezi kuwa mama yake mzazi, kwa sababu tu Juma hamjui mama yake?

Hoja yako hapo ni kama vile unasema kuwa Juma hawezi kujua kuwa Jane si mama yake mzazi, kwa sababu tu hamjui mama yake mzazi ni nani. Unasema kuwa inambidi Juma, mwanamme mwenye miaka 30, amjue mama yake mzazi ni nani kwanza kabla ya kusema hiyu binti mchanga Jane hawezi kuwa mama yake mzazi.

Sihitaji kujua chanzo cha uhai kujua chanzo cha uhai si Mungu.

Nahitaji kujua tu kwamba Mungu hayupo, nikijua Mungu hayupo, nitajua chanzo cha uhai si Mungu, hata kabla sijajua chanzo cha uhai ni nini.

Sihitaji kujua jibu sahihi ili kujua jibu fulani si sahihi.

Mnalazimisha kuwa ni lazima kujua chanzo cha ihai ni nini ili useme Mungu hayupo.

That is a false dichotomy logical fallacy.
 
Kitu ni either kipo au hakipo.

Sasa wewe unakataa kwamba Mungu hayupo halafu bado umeshindwa kumthibitisha yupo.

Sasa unataka nini?
Tatizo unaruka hatua ambayo ni njia ambayo utatumia kuweza kujua hicho kitu kipo au hakipo. Wewe unaanzia tu kusema Mungu hayupo ila hujiulizi umewezaje kujua hilo? Chukua mfano embe lipo kwenye mti na limeiva kabisa, halafu anakuja mtu anakwambia kuwa hilo embe halina funza ndani, je wewe utakubali?
 
Dragons 🐉 watemao moto midomoni mwao, wapo au hawapo?
 
😂Aisee
 
Nithibitishe mara ngapi?

Unanifuatilia?

Mara ngapi nimeongelea Epicurean Paradox na The Problem of Evil?

Umefuatilia Epicurean Paradox na The Problem of Evil?

Umeelewa hoja zilizomo katika mantiki ya maswali yanayoibuliwa na the problem of evil?
Epicurean Paradox haithibitishi kuwa Mungu hayupo, bali inapinga uwezekano wa kuwepo kwa Mungu mwenye sifa za ujuzi wote, uwezo wote, na upendo wote.
Epicurean Paradox inahitimisha kuwa Mungu mwenye sifa fulani hayupo, si kwamba Mungu yoyote hayupo. Umewezaje kuthibitisha kuwa hakuna Mungu yeyote, hata asiye na sifa hizo? Kwa sababu hoja yako ni dhidi ya sifa, si uwepo wa Mungu kwa ujumla.
 
Na mimi ndiyo nimeanza na Mungu huyo, na najitahidi kutokuwa general na kusisitiza kila ninapoandika Mungu naweka na sifa zake "Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote" ambaye anajumuisha hao kina Allah, Jehovah, etc.

Siwezi kuzungumzia miungu wote kwa pamoja, lazima nianze na Mungu fulani specific. Na huyu ndiye Mungu anayejulikana kwa wengi kwa kupitia dini.

Sasa, kwa kuanzia na huyu, umekubali kuwa huyu hayupo?

Maana kuna watu wanasema Beyonce ni Mungu wao, na wanasema Beyonce yupo, hao siwezi kubishana nao kusema kwamba Mungu wao Beyonce hayupo.
 
It's a free forum, jifunze kuvumilia maoni yanayokinzana na ya kwako.
Hizo imani zenu zilizotungwa na matapeli wa zamani ni hiyari yako kuziamini au kutokuziamini, ukulizwa maswali yanayohitaji sold proofs ilhali vitu vyeni ni 'hewa' kwa maana na vya kufikirika tu basi eleza ya kuwa hauna proofs au kwepa swali au jibu kitapelitapeli kama wanavyojibu masheikh na wachungaji.
 
Hapana, bado sijakubali kwa sababu hoja zako bado hazijathibitisha kuwa Mungu huyu hayupo. Kwa nini unataka mimi nithibitishe kitu ambacho wewe mwenyewe bado hujathibitisha? Endelea na hoja zako na ulete ushahidi wa moja kwa moja

Unasema unazungumzia Mungu maalum, lakini Epicurean Paradox ni hoja ya jumla dhidi ya dhana fulani ya Mungu, si dhidi ya Mungu maalum wa dini fulani. Kwa mfano, Uislamu unaeleza kuwa uovu ni sehemu ya majaribio ya imani, na Ukristo unaeleza kuwa uovu ulitokana na free will. Je, una hoja inayopingana na tafsiri hizi?
 
Epicurean paradox inamhusu Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote. Ni Mungu maalum katika muktadha huo.

Ukisema Beyonce ni Mungu wako na sifa ya uungu wake ni kujua kuimba na kucheza muziki sana, Epicurean Paradox haimgusi huyo Mungu wako Beyonce.

Nikuulize.

Uthibitisho wa aina gani utakufanya ukubali Mungu hayupo?
 
Kwenye mifano umewataja wachina na wajapan 😁, hao wazungu uliowataja wengi wanaishi ishi tu bila imani.
Mifano iendane na uhalisia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…