Kirusi kinachotisha kuliko Corona ni uoga/ hofu

Kirusi kinachotisha kuliko Corona ni uoga/ hofu

1584465073003.png
 
Watu wamejaa raia wa nje na wa ndani wananunua bidhaa kwa foleni isiyo ya kawaida, watu wamejaza vyakula, pedi, na vitu vingine vingi kwa pamoja na si kawaida, wafanyakazi wamevaa mask gloves. Mashelf yana magepu daah

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo Corona imekuja na hela nini? Unapata wapi ujasiri wa kwenda kununua stock ya vyakula kwenye supermarket usawa huu kama sio ulongo??
 
  • Thanks
Reactions: rr4
Wabongo hatujambo!

Toka Corona ianze imeshapata wasemaji na wataalamu wengi.

Sasa hivi kila mtu anajifanya msemaji mzuri wa Corona.

Kuna hadi wengine wameshapata hadi dawa tayari. Wabongo noma. Yaani Corona imeshakuwa dili tayari.

Kazi za kitaalam na sayansi tuwaachie wataalamu. Huko vijijini watu wamejawa na hofu

Hakuna wanachojua zaidi ya kwamba Corona ni hatari sana itamaliza watu wote.

Hii imepelekea na itapelekea unyanyapaa.
Imefika mahali ukikohoa tu! Tayari una Corona.

Yaani hata ukipaliwa na pilipili masikini ya Mungu utaambiwa Corona.

Natoa wito kwa mamlaka kueneza elimu sana hasa vijijini ambako mtandao hasa wa internet si mpana.

Hofu ya kufa ni kubwa
Hofu imetamalaki kuliko elemu ya kujikinga.
 
Back
Top Bottom