Kirusi kinachotisha kuliko Corona ni uoga/ hofu

Kwahiyo Corona imekuja na hela nini? Unapata wapi ujasiri wa kwenda kununua stock ya vyakula kwenye supermarket usawa huu kama sio ulongo??
 
Reactions: rr4
Kesho naenda na mimi kuzoa toilet paper za kutosha super market kama mabeberu walivyofanya.
 
Wabongo hatujambo!

Toka Corona ianze imeshapata wasemaji na wataalamu wengi.

Sasa hivi kila mtu anajifanya msemaji mzuri wa Corona.

Kuna hadi wengine wameshapata hadi dawa tayari. Wabongo noma. Yaani Corona imeshakuwa dili tayari.

Kazi za kitaalam na sayansi tuwaachie wataalamu. Huko vijijini watu wamejawa na hofu

Hakuna wanachojua zaidi ya kwamba Corona ni hatari sana itamaliza watu wote.

Hii imepelekea na itapelekea unyanyapaa.
Imefika mahali ukikohoa tu! Tayari una Corona.

Yaani hata ukipaliwa na pilipili masikini ya Mungu utaambiwa Corona.

Natoa wito kwa mamlaka kueneza elimu sana hasa vijijini ambako mtandao hasa wa internet si mpana.

Hofu ya kufa ni kubwa
Hofu imetamalaki kuliko elemu ya kujikinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…