Kirusi kipya cha HIV kimegunduliwa Uholanzi

Kirusi kipya cha HIV kimegunduliwa Uholanzi

Nimeikuta hii habari kwenye ukurasa wa Millard Ayo. Kirusi hicho ni hatari zaidi ya kile cha mwanzo.

Kinashambulia kinga za mwili mara mbili zaidi ya kile cha awali. Mpaka sasa hakuna dawa wala chanjo ya hicho kirusi.

Corona inasuasua, hapa tusipokuwa makini tutapatikana.View attachment 2107848View attachment 2107849
Huu uzushi wa virusi utaisha lini?
Ulikua uemshamiri kwenye COVID19 sasa naona umehamia kwenye UKIMWI.
 
Sawa waulize kilikuwa kinaishi wapi before kama wamekigundua hivi karibuni ??
Kilikuwa kimetulia tu kilivyoona korona anatamba kikaona wivu! Sasa kimeamua Kama mbwai iwe mbwai..😂
 
Kumbe hata huyo Milard Ayo huwa hajiongezi kabla ya kutoa habari? Na kwanini haweki “source” ya habari zake? Kwasababu hiyo “variant” ya HIV inatibika.

“The new variant has been found mainly in The Netherlands and it is more infectious, but it can be detected with existing tests and responds to treatment”

Sawasawa mkuu....
 
Kwahiyo kwa hapa bongo kitafikia kule kwa akina Nshomile au


Serikali haikuleta tetemeko



Seri
 
Wasalaam Wakuu.

Wakati dunia ikipambana usiku na mchana katika kuhakikisha kinapata uvumbuzi wa kutibu kirusi kinachosababisha UKIMWI, nchini Uholanzi kirusi cha aina nyingine chagundulika.

Kirusi hicho kilichopewa jina la 'VB Variant' kwa maana ya Virulent Subtype B kinasadikika kuwa na nguvu za kushambulia kinga mara mbili ya Virusi vya kawaida vilivyozoeleka.

Katika utafiti uliochapishwa hivi majuzi katika jarida la 'Journal Science' watalaam wanasema kuwa kirusi hicho kina uwezo wa kujizalisha kwa haraka zaidi hivyo kufanya mashambulizi ya kinga za mwili kuwa mara dufu.

Pia, wametanabaisha kwamba uwezo wake wa kuambukiza baina ya mtu na mtu ni mwepesi zaidi.

Kirusi hicho ambacho mpaka sasa hakina kinga wala tiba, kimeshashambulia zaidi ya watu 109 huko Uholanzi.

Kirusi hicho kinajulikana kwa kupima kwa vipimo vya kawaida vya kupima maambukizi ya virusi vya UKIMWI vya kawaida.

Nawasihi Watanzania wenzangu, tuzidishe uaminifu na kuchukua tahadhari zaidi kuepukana na kirusi hicho hatari.

Tutumie kinga pale inapobidi na tukapime ili tujue hali zetu. Kama utapatikana na ugonjwa, utaanza dozi mapema na kupunguza kasi ya mashambulizi ya virusi hivyo.

TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA.

Mtaarifu na mwenzako.
 
Huu was sasa unaambukizwaje au na wenyw kwa hewa
Maana wamesema kirusi kipya au ndio tukitazamana tu tayari mmh tuleteeni elmenti
 
Nyingine ni propaganda, nafikiri covid imekuwa wimbo sasa wanataka kuhamisha watu mind zao waone covid ni kawaida maana kuna hatari zaidi ya covid. Hakuna kirusi kigeni duniani na hakuna kirusi kisichokuwa na madhara tushazoea. Mm naona wanataka kupunguza homa ya dunia ya covid.
 
Back
Top Bottom