bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 1,213
- 2,938
Mwaka 2022, nchini Brazil (mji wa Mineiros), binti mmoja wa miaka 19 alijifungua watoto wawili wa kiume waliotazamiwa kuwa mapacha wa kawaida. Watoto hao walikua kwa amani hadi walipofikisha umri wa miezi minane.
Lakini kutokana na sura za watoto hao kuanza kutofautiana sana, mama huyo aliamua kufanya kipimo cha DNA na mwanamume aliyedhaniwa kuwa baba wa wote wawili.
Majibu yalirudi na majanga: Mwanamume huyo alikuwa baba wa mtoto mmoja tu! Mtoto wa pili hakuwa wake kabisa!
Siku majibu ya kipimo cha DNA yalipotoka, sio tu kwamba yaliacha familia katika mshtuko mkubwa... bali ulimwengu mzima wa sayansi ulibaki unashika mdomo kwa kutoliamini jambo hilo!
Akiwa kwenye mshtuko, mama huyo alikumbuka kuwa siku hiyo hiyo alikuwa na uhusiano wa kimwili na mwanamume mwingine.
Wazazi walipomtafuta mwanamume huyo wa pili na kumfanyia kipimo cha DNA... majibu yakathibitisha rasmi kuwa yeye ndiye baba wa kibiolojia wa mtoto yule wa pili!
Kesi hii nadra mno duniani kitaalamu inaitwa Heteropaternal Superfecundation.
Inatokea wakati mwanamke anapotoa mayai mawili kwa wakati mmoja (ovulation), kisha mayai hayo yakarutubishwa na mbegu za wanaume wawili tofauti ndani ya masaa au siku chache. Kwa kuwa mbegu za kiume zinaweza kuishi hadi siku 5 ndani ya mfumo wa uzazi, miujiza hii ya chumbani hutokea!
Daktari aliyesimamia kesi hii, Tulio Jorge Franco, alithibitisha kuwa hii ni moja ya kesi chache mno kuwahi kurekodiwa katika historia ya binadamu.
Mbali na mshangao huo wa kisayansi, kilichofuata kilikuwa cha kipekee zaidi:
Mwanamume yule aliyekuwa baba wa mtoto mmoja aliamua kumpiga stop ibilisi wa ubinafsi! Alikubali kuwalea watoto wote wawili kama wake wa damu, bila kuweka ubaguzi wowote ili wakue pamoja kwa amani.
Kama ingekuwa ni wewe ndiye huyo mwanamume, ungekuwa na ujasiri wa kumpokea na kumlea mtoto huyo mwingine kama wako, au ungepanga mikoba yako na kuondoka?