Basi sawa ila naamini unamfahamu huyu bwana Abu Ubaidah Al Banshiri ambaye alikufa kwenye MV Bukoba.
Sio mara ya kwanza tanzania kuhusishwa na ugaidi. Shambulio la 1998 magaidi wa kitanzania walihusika. Na kama watu wa al qaeda wanaweza kuja kujificha hapa lazima wana watu wanaowakaribisha na kuwahifadhi. Sasa ukionekana una misimamo mikali na unafundisha radicalism kwa vijana, watu watakuja kukutembelea ili wajiridhishe ni nini lengo lako. Mahakama kuweza kuthibitisha au kutothibitisha haimaanishi kuwa eti sio magaidi. Kuna majambazi na wezi huwa wanakamatwa na kesi wanashinda na mwisho wao huwa wanauliwa mitaani kwa sababu huwa wanashinda mahakamani kwa sababu ya loop holes za kisheria.
Watu walijaribu kuutingisha mbuyu hapa tanzania, circa 2014-16. Na wakashughulikiwa vizuri tu.