Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #161
Che...Mzee anapeta hiyo😂anajifanya hajui. Uzuri wanajua sana wanachokifanya. Wakiwa in public ndo wanadownplay what they are doing.
Mjadala ili uwe na tija unahitaji adabu.
Umeweka video nzuri na inaeleweka.
Hapana haja ya kunifanyia kejeli kuwa nilikuwa nchi za nje.
Niheshimu kama ninavyokuheshimu.
Nisome ninavyoandika kwako kwa heshima.
Turejee kwenye hii video.
Ninataka sana kujua historia na mwisho wa huyu kijana.
Kwani hakika lazima atakuwa na mahali alipoanzia.
Amesoma wapi, nani waalimu wake, nani wazazi wake, anatoka mji gani nk. nk.
Tuiridhishe na ukweli isiwe ni video ya kwengine imefanyiwa "dubbing."
Tusijenge mlima kutoka kichuguu.