Kisa cha Maiti ya mtu isiyotambulika iliyookotwa kwenye ufukwe wa bahari na Mvuvi wa Dagaa

Kisa cha Maiti ya mtu isiyotambulika iliyookotwa kwenye ufukwe wa bahari na Mvuvi wa Dagaa

Wakati fulani nikiwa Dodoma mwaka 2022, siku moja msafara wa Rais Samia (presidential motorcade) ulikuwa ukitokea Airport Dodoma kuelekea ikulu chamwino. Nadhani na yeye alikuwa anarejea kutokea nje ya nchi).

Sasa nakumbuka siku hii Mimi nilikuwa nimetumwanatokea benki ya Nmb tawi la Bunge pale kuweka floti ya mpesa .
Sasa siku hii nilipokuwa karibia na Malaika Pub nikitembea pembeni ya barabara kuna jambo nilishuhudia maeneo hayo ambalo limenifanya nikupe kisa hiki kimoja ambacho nataka kushare hapa.

Siku hiyo wakati msafara ukipita, yupo bwana mmoja akiwa na gari yake akijaribu kupenya penya huku pembeni mwa Barabara na gari yake, alijikuta amekanyaga kitu kama rundo la taka . Sasa Ghafla zikasikika kelele za Watu waliokuwa pembeni pale kama kumshtua huyu jamaa akiwa na gari yake.

Kumbe huyu mdau alichokuwa amekanyaga Kama taka ,haikuwa ni takataka bali ni kichaa aliyekuwa amejikunja pembeni ya barabara amelala huku amejifunika na nguo chakavu.🥺🥺

Kichaa huyu nakumbuka alikuwa ni mmama fulani hivi mfupi mweusi na alikanyagwa nadhani mguu. Sasa katika hekaheka za hapa na pale na umati wa watu , yule bwana akiwa amepaniki alijitolea kumpeleka yule kichaa hospitali hapo Dodoma (nimesahau jina ila ndio hospitali kubwa Dodoma).

Baada ya kushuhudia hiki kizaazaa nikaacha umati hapo ukipiga gumzo huyooo Mimi nikaondoka zangu kwa masikitiko kuja huku maeneo ya duka kubwa la pombe kali la Takawedo liquor store. Wakaaji wa Dodoma haswa maeneo ya Area c wanayapata haya Maeneo.

Anyway sasa zikapita kama wiki moja au mbili hivi , mitaa ya pale nikasikia kwenye vijiwe vya boda kwamba yule mama kichaa ni kama alikuja kufariki japo sikuwa na uhakika sana . Sasa binafsi nikajisemea moyoni kama alifariki kweli, basi mwili wake ungekaa mochwari siku kadhaa au wiki kadhaa kusubiria ndugu na jamaa wajitokeze kuja kuuchukua mwili wao. Na kama pasingejitokeza mtu mwenye uhusiano na huyu kichaa basi ungezikwa tu na serikali... Ikawa imeisha hivyo .

Lakini kama tungerudisha wakati kama miaka 70 au 80 nyuma , maiti ya mtu kama huyu halafu iwe ni ya mwanaume ikose ndugu wa kumzika na haijulikani, basi ingefuatwa na na watu MAALUM na kuuchukua na kuuvalisha vizuri kabisa kisha kupewa ujumbe Maalum na mzito wa kuusafirisha hadi sehemu fulani mbali sana. Pia hawa watu wangeipa hii maiti passport ya kusafiria pamoja na fedha ya matumizi wakati wa safari njiani ikiwa inapeleka ujumbe .😁😁. ....

Hii ina sound kama stori za abunuwasi na bhangi ee🤣🤣🤣. Lakini amini nachokwenda kukusimulia hapa......
View attachment 3546961
Tafuta popcorn 🍿 kabisa nikupe kisa hiki cha kijasusi cha aina yake
Nimeikubali hii intro
 
"Operation Mincemeat" na "Dial M for Murder" ni movie zangu pendwa za kizamani.
mcTobby , nisamehe
Hii naijua nje ndani

Operesheni Mincemeat,
Ulikuwa ni mpango wa siri wa Uingereza mwaka 1943 wakati wa Vita vya Pili vya Dunia uliolenga kuwapotosha Wajerumani kuhusu mipango ya uvamizi wa Washirika.
Maafisa wa ujasusi wa Uingereza walitengeneza mpango wa ajabu: waliweka nyaraka za uongo kwenye mwili wa mtu aliyekufa na kuuacha baharini karibu na Hispania ili Wajerumani waamini kuwa Washirika walikuwa wanapanga kuvamia Ugiriki badala ya Sicily. Mpango huo ulifanikiwa kwani Adolf Hitler aliamini taarifa hizo na kuhamisha majeshi kwenda kulinda Ugiriki na maeneo mengine, hivyo uvamizi halisi wa Sicily ulipofanyika Wajerumani walikamatwa bila maandalizi.

Ili kufanya mpango huo uonekane halisi, maafisa Ewen Montagu na Charles Cholmondeley walimpa marehemu utambulisho mpya kama afisa wa jeshi aitwaye William Martin. Walitengeneza historia kamili ya maisha yake, ikiwa ni pamoja na barua za mapenzi, stakabadhi za benki, na hata mchumba wa kubuniwa.

Mpango huo ulivutiwa na mawazo ya waandishi na hata ulihusishwa na mwandishi wa James Bond, Ian Fleming, ambaye alichangia mawazo ya mbinu za udanganyifu wa kivita.
Mwili uliotumika ulikuwa wa Glyndwr Michael, mtu maskini kutoka Wales ambaye hakuwa na familia, na maisha yake yalitumiwa kama chombo cha vita. Hili lilizua mjadala kuhusu maadili ya kutumia mwili wa mtu kwa madhumuni ya kijeshi.

Hii ilikuwa ni mojawapo ya mbinu za ajabu zaidi za udanganyifu katika historia ya vita na mpango wa siri wa Uingereza uliolenga kumpotosha kiongozi wa Nazi, Adolf Hitler, wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.
Mwaka 1943, mataifa ya Washirika yalikuwa yanajiandaa kuivamia Ulaya kupitia kisiwa cha Sicily. Tatizo lilikuwa wazi: Wajerumani walitarajia uvamizi huo. Ili kufanikiwa, Waingereza walihitaji kuwafanya Wajerumani waamini kuwa uvamizi ungefanyika sehemu nyingine na hasa Greece, Hapo ndipo mpango wa ajabu ulipozaliwa.

Wazo la kutumia maiti kama mjumbe wa siri
Maafisa wa ujasusi wa Uingereza walibuni mpango wa kuweka nyaraka za siri za uongo kwenye mwili wa mtu aliyekufa na kuufanya uonekane kama askari aliyekufa ajalini baharini.

Mwili huo ungeonekana kama umebeba nyaraka muhimu za kijeshi kuhusu mipango ya uvamizi. Walitarajia kwamba maafisa wa Kihispania wangepata mwili huo na, kwa siri, kuwapa Wajerumani taarifa zilizopatikana.
Mpango huo ulihitaji mambo mengi yaonekane ya kweli kabisa na si nyaraka tu, bali maisha kamili ya mtu huyo wa kubuni.

Kuundwa kwa utambulisho wa “Major William Martin”
Mtu aliyekufa alipewa utambulisho mpya: afisa wa Jeshi la Wanamaji wa Uingereza aitwaye Major William Martin.
Maafisa wa ujasusi walitengeneza maisha yake kwa undani mkubwa, wakijumuisha:
  • Barua za mapenzi kutoka kwa mchumba wa kubuniwa
  • Picha ya mwanamke aliyedaiwa kuwa mpenzi wake
  • Risiti za matumizi ya kila siku
  • Tiketi na stakabadhi za benki
  • Barua binafsi za kawaida za maisha ya kila siku
Lengo lilikuwa kuonyesha kwamba alikuwa mtu halisi mwenye maisha ya kawaida, si sehemu ya mpango wa kijeshi.
Hii inaonyesha jinsi ujasusi wa kivita ulivyohusisha pia saikolojia — kuwafanya wapinzani waamini hadithi nzima bila shaka.
Mwili unatupwa baharini karibu na Hispania
Mwili huo uliwekwa baharini karibu na pwani ya Hispania, nchi ambayo ilikuwa haina msimamo rasmi vitani lakini ilikuwa na mawasiliano ya karibu na Ujerumani wa Nazi.
Kama ilivyotarajiwa:
  • Mwili ulipatikana na mamlaka za Hispania
  • Nyaraka zilichunguzwa kwa siri
  • Taarifa zilifikishwa kwa Wajerumani
  • Hatimaye, uongo huo uliaminika.
  • Mafanikio ya mpango dhidi ya Ujerumani
  • Matokeo yake yalikuwa makubwa sana kijeshi.
  • Adolf Hitler aliamini kuwa uvamizi mkubwa ungefanyika Ugiriki badala ya Sicily. Kutokana na hilo:
  • Majeshi ya Ujerumani yalihamishwa kutoka Sicily
  • Ulinzi wa Sicily ulidhoofika
  • Washirika walifanikiwa kuivamia Sicily kwa urahisi zaidi
  • Tukio hili lilisaidia kubadilisha mwelekeo wa vita Ulaya.
Chanzo cha mawazo na mchango wa waandishi
Mpango huu ulichangiwa na mawazo ya ubunifu na hata fasihi.
Ian Fleming — ambaye baadaye aliandika hadithi za James Bond — alikuwa sehemu ya idara ya ujasusi ya Uingereza wakati huo na alichangia mawazo kuhusu mbinu za udanganyifu wa kivita.
Mpango huo unaonyesha jinsi ubunifu, hadithi na saikolojia zilivyotumika kama silaha za vita.
 
SEHEMU YA NANE
Sasa kamati hii ya Twenty Committee ikawa ipo kwenye maandalizi ya mwisho kabisa katika kumuandaa huyu mtu mfu yaani mincemeat aliyebatizwa jina la Major William Martin kwa ajili ya kuanza safari, Kipengele muhimu cha kumuandaa huyu mfu ilikuwa ni kutafuta mtu anaedhaniwa anaweza kufanana naye kwa sura ya uso ili picha yake itumike kwenye I. D. Card ya major William Martin. Ikumbukwe maiti hii iliokotwa na haikuwa na picha yoyote ambayo ingeweza kutumika kumtambua huyu bwana akiwa hai alifanana aje.

Hivyo ilipofika mwezi march Ewen Montagu alikutana na afisa usalama kitengo cha ujasusi jeshi la maji aliyeitwa Ronnie Reed ambaye kitaaluma alikuwa mfanyakazi wa shirika la BBC akiwa mhandisi kwenye maswala ya mawasiliano Hususani kwenye mitambo ya radio.
Huyu bwana Ronnie alikuwa na uso mwembamba na kidevu kilichochongoka, ambapo Ewen Montagu aliamini huyu afisa picha yake ingeweza kutumika katika kitambulisho cha huyu major William Martin.

Baada ya zoezi hili la kupata picha ya kitambulisho cha mincemeat, zoezi lililobaki ilikuwa ni kuvalishwa nguo ambazo ni sare rasmi zilizoandaliwa kwa ajili yake.

Na kweli Ewen Montagu na Cholmondeley pamoja na timu iliyokuwa ikishughulikia zoezi hili walifika hospital ya St. Pancras kwa ajili ya kuivalisha maiti hii nguo ikiwemo na chupi😁😁🤣🤣🤣🤣🤣. Zoezi ambalo huyu Ewen Montagu alikuja kukiri baadaye yaani mwaka 1991 kwamba namnukuu. " A task that I heartly disliked........ on seeing the corpse lying stiff on the mortuary slab, gradually being transformed into someone i almost knew by the clothes, and the personality,........ ".

Sasa katika zoezi la kuuvalisha huu mwili nguo hizo za uniform yaani Battle dress kwenye mochwari hii, ni kwamba mwili wa huyu mtu kutokana na kukaa kwenye friji kwa muda mrefu , viatu viligoma kuingia mguuni kutokana na hali mbaya ya mwili huo yaani "Rigor Mortis" na kukakamaa sana kutokana na baridi hivyo ikaamuliwa kuivalisha maiti viatu liwe zoezi la mwisho kabisa, hivyo ikarudishwa kwenye friji za mochwari ikiwa Sasa maiti hiyo imevalia sare za jeshi kama Marine officer.


Ukiachana na zoezi hili la kuivalisha maiti nguo , ni kwamba maiti hii ilipaswa kusafirishwa kwa njia ya nyambizi yaani submarine. Na hapo mwanzo nikudokezea nyambizi iliyopaswa kufanya zoezi hili la kuubeba mwili ilikuwa inaongozwa na captain Bill Jewell iliyoitwa HMS Seraph na ilitarajiwa kuanza safari lakini huyu Captain baada ya kuusishwa katika operation hii ya siri na Ewen Montagu, alipaswa kuichelewesha kuanza safari kwa wiki moja ili maandalizi ya maiti hii ya Major William Martin ifanyiwe maandalizi ya mwisho mwisho.

Hii delay ya karibia wiki moja ilitosha kuwataarifu maafisa wengine waliokuwa wanahusika na operation hii akiwemo Alan Hillgarth afisa wa ubalozi yaani Naval Attachè aliyepo uhispania na afisa mwingine anayeitwa Dudley Clarke aliyepo Algeria wawe ATTENTION❗❗❗❗.
Na kweli ukatumwa ujumbe wa siri kwa njia ya Telegram kwenda kwa Clarke na Hillgarth uliosomeka : MINCEMEAT SAILS 19TH APRIL, AND OPERATION PROBABLY TAKES PLACE 28TH APRIL "

Hiyo tarehe iliyotajwa hapo juu kwenye ujumbe huo wa siri wa telegram yaani tarehe 28 ulikuwa na maana mbili. maana ya kwanza ilipaswa mincemeat afikishwe majira ya usiku wa manane kati ya tarehe 28 na 29 wakati hakuna mwanga wa mwezi unaondama usiku ili usije kugundulika ni nini kilikuwa kinaendelea na wavuvi wale wanaovua majira ya usiku pale nyambizi itakapouachia mwili wa mincemeat baharini karibu na ufukwe........

Pili ni kwamba operation hii ingeweza kuanza hata mapema yaani tarehe 26 April ili kama maiti hiyo ingeachiwa baharini , wangeipa muda wa siku mbili ielee baharini hadi kwenye fukwe za Hispania kisha huyu Allan Hillgarth akiwa uhispania ajitayarishe kupata Taarifa zozote zutakazotolewa na mamlaka za uhispania kuhusiana na kupatikana kwa maiti ya mtu ambaye wao watadhania alipata ajali huko katikati baharini............ Nadhani umeelewa hapo ....




Sasa kwa upande wa Cholmondeley na Ewen Montagu, zoezi lililobaki ni kufanyia maandalizi ya mwisho mwili wa marehemu ikiwemo kuivalisha viatu pamoja na mkanda maalum wa ngozi kiunoni.. mkanda huu ungetumika kuifunga na na kuishikilia brifecase iliyo na barua zile maalum pamoja na nyaraka zote muhimu. Hii ina maana kwamba endapo Huyu Mincemeat akiachwa baharini aelee hadi kwenye fukwe za Hispania, aleee pamoja na briefcase hiyo .

Baada ya hapo mwili wa mincemeat ulipaswa kusafirishwa kutoka hospital ya St Pancras iliyopo London kwa gari maalum ya mochwari hadi Scotland kwenye bandari ambapo nyambizi ya HMS Seraph . Hivyo baada ya mwili huu kuwekwa kwenye kifaa maalum kama thermos kubwa iliyotengenezwa maalum kwa ajili ya kazi hii ulipakiwa kwa uangalifu maalum na kuwekwa kwenye gari maalum ya Van aina ya Aston Martin ikiendeshwa na afisa wa MI5 aliyeitwa Jock Harsfall.

Ewen Montagu, Charles Cholmondeley pamoja na maafisa wengine waliohusika kwenye operation hii walipaswa kusafiri kwa magari mengine kama escort hadi Scotland ..

Baada ya safari ndefu kutoka uingereza hadi Scotland hatimaye msafara huu ulifika kwenye bandari ya Greenock kwenye pwani ya magharibi ya Scotland, na walikuta maafisa kadhaa wakimsubiri ujio wao ikiwemo mzigo maalum kama pipa kubwa hivi la chuma ambapo kwa juu kuliandikwa Optical instrument SPECIFIC F. O. S SHIPMENT. HANDLE WITH CARE.
Baada ya hafla fupi ya mapokezi Bill Jewell ambaye alikuwa anajua mzigo huo ulikuwa ni kitu gani alikuwa akifuatilia kwa karibu mzigo huu ukishushwa na kuhifadhiwa kwenye cargo bay ya nyambizi ya HMS Seraph.

Baada ya zoezi hili kukamilika , Ewen Montagu na Cholmondeley walimpa bill Jewell maelezo na kumkabidhi briefcase yenye nyaraka za Siri (zile Barua )ambazo zilipaswa kuambatana na huyu marehemu ambazo zingekuwa attached pale maiti hii itakapofikishwa kwenye eneo husika kisha kuachwa zielee baharini hadi ufukweni.

Ikawa rasmi Sasa baada ya miezi mitatu ya maandalizi ya huyu marehemu imekamilika na maiti hii ikawa imekabidhiwa kundi lingine la majasusi (yaani bill Jewell na maafisa wengine) kwa ajili ya kuusafirisha hadi kwenye fukwe za Hispania kwa safari ya karibia siku 10 baharini.
Nikukumbushe tu kitu hapa . Hii nyambizi ya HMS Seraph sio kwamba ilikuwa inaubeba mzigo huu maalum peke yake , bali ilikuwa na jukumu lingine la kubeba mizigo na zana zingine za kivita kwa ajili ya kusafirishwa hadi Afrika kaskazini. Nyambizi hii ilikuwa kama ni cover up ili isijulikane ni nini haswa kinaendelea kwa wasio husika. Na ikizingatiwa nyambizi hupita chini ndani ya bahari.

Sasa Ndani ya nyambizi hii wafanyakazi wake yaani Crewmen walikuwa hawajui ni kifaa gani hiki kama pipa lenye urefu wa futi sita walikuwa wamebeba ila walikuwa wanapewa maelezo ya mara kwa mara kwamba ni kifaa maalum cha kijasusi chenye umuhimu mkubwa cha utafiti wa Hali ya hewa baharini, wasijue ndani yake kulikuwa na maiti ya mtu na wangekaa nayo humo kwa zaidi ya siku kumi Safarini.😎😎😎🤣 Na tena wengine wangelala pembeni ya kifaa hiki kama pipa na kukifanaya kama mto wa kuegemezea kichwa.


Na kweli ilipofika saa 10 kamili jioni siku ya tarehe 19 mwezi april mwaka 1943 baada ya kila kitu kuwa clear , Nyambizi ya HMS Seraph iling'oa nanga kwenye bandari ya Holy loch magharibi mwa Scotland na kuingia bahari kuu na kufanya "Trim dive" kwa ajili ya safari ndefu kuelekea bahari ya Mediterranean ikiongozwa na kapteni Bill Jewell akisaidiana na first lieutenant David Scott kama msaidizi wake.

Kwanza ngoja nigusie kidogo maana ya trim dive..


Iko hivi Kwa namna nyambizi ilivyotengenezwa na ikiwa imebeba mzigo lazima Captain anayeiongoza aizamishe kidogo kidogo hadi chini ya maji na kuibuka tena juu ya uso wa maji ili kuhakikisha ipo balanced...
Ndio maana kama umewahi kushuhudia kwenye movie au documentary zinazoonyesha hizi nyambizi Kuna kitu umewahi kuona.... Nyambizi inaibuka Ghafla na kurudi tena ndani ya bahari... Pale unakuta inafanyiwa TRIM DIVE ili iwe balance... Anyway waliosoma concept za Archimedes principle kwenye physics wataelewa hapa hii concept anyway tuendelee......😎



Huyu Bill Jewell alituma ujumbe Maalum makao makuu ya "Admirality" uliosomeka kwamba operation imeanza huku maafisa waliobaki akiwemo Montagu na Cholmondeley wakiwaza je huu mpango wa kuwadanganya wajerumani utafanya kazi au la? Maana WAJERUMANI NAO WALIKUWA SMART SANA KWENYE MICHEZO HII YA DECEPTION YA KIJASUSI Lilikuwa ni swala la muda kusubiria nini kitatokea. Wengi wa maafisa waliokuwa wanajua kuhusiana na hii operation walikuwa na wasiwasi swali likiwa , je, maiti itaangukia mikononi mwa wajerumani? Na je , watadanganyika (deceived) na barua ambazo watazikuta kwa huyu marehemu?

Ni kawaida kwenye medani za kijasusi pale ambapo maafisa kuwa na wasiwasi endapo plan au operation maalum iliyotarajiwa kufanyika kama itafaulu au itafeli . Na kuna Kanuni moja inasema kwamba endapo Kuna jambo litazua wasiwasi basi "ABORT THE MISSION"
Ipo nukuu moja ya afisa wa usalama aliyeitwa John Godfrey inasema kwamba "“Intelligence, like food,soon gets stale, smelly, cold, soggy and indigestible, and when it has gone bad does more harm than good. If it ever gets into one of these revolting conditions, do not try to warm it up. Withdraw the offending morsel, and start again.”
Hili jambo lilikuwa akilini mwa captain wa hii nyambizi bwana Bill Jewell. Tayari alipewa maelekezo endapo katika operation hii kukatokea jambo linalohatarisha operation hii ya siri , hana budi ku terminate mpango mzima kwa kuchoma nyaraka za Siri na mwili wa huyu mincemeat kuharibiwa ili kufuta ushahidi wowote ule.

Baada ya safari ya siku kadhaa baharini, ilipowadia Tarehe 28 April ndani ya nyambizi ya HMS Seraph ikizunguka rasi ya st. Vincent na kuchukua uelekeo kwenda Huelva Spain, captain Bill Jewell aliwaita maafisa wake wachache akiwemo msaidizi wake na kutoa briefings kuhusiana na operation hii na mzigo walioubeba . Kwa mara ya kwanza wengine miongoni wa maafisa hao ndio walijua kwamba walikuwa wanasafirisha Maiti ya mtu kwa siri kubwa aliyehifadhiwa kwenye kifaa maalum kama pipa kubwa zito la chuma lenye urefu wa futi 6 na upana wa mita 2.

Ilipofika usiku wa kuamkia Tarehe 29 April , Captain bill Jewell alitoa amri nyambizi izame chini ya maji karibia na pwani ya Punta Umbria kusini mwa Hispania
na kufanya kitu kinaitwa close range reconnaissance ya eneo hilo lote ili kuelewa mazingira yake kwa kutumia binoculars.
Zaidi waliona tu boti ndogo mbao za wavuvi pamoja na vinyumba vya msonge waliyokuwa wanakamati wavuvi na familia zao.

Sasa ilipofika tarehe 30 April , majira ya saa Saba kamili usiku, nyambizi hii ilianza kukaribia taratibu fukwe yenye kina cha maji mafupi kwenye eneo hili la punta Umbria .
Wafanyakazi wa nyambizi hii yaani Crewmen walitaarifiwa kwamba mzigo walioubeba ndani yake Kuna kifaa maalum cha Siri kimewekwa kwa ajili ya kuachwa hapo Huelva kwa ajili ya kumtega mtu ambaye anasemekana ni jasusi wa ujerumani aliyekuwa Hispania 🤣🤣🤣.
Baada ya muda wa kama masaa mawili yaani majira ya 10 na robo asubuhi nyambizi iliibuka kwenye maji na bill Jewell alitoa amri kifaa hicho kibebwe kwa uangalifu mkubwa hadi kwenye mlango wa nyambizi wa kufyatulia kombora aina ya torpedo yaani Torpedo Hatch , kisha kuachwa hapo na wakaamriwa warudi ndani ya nyambizi . Hivyo maafisa wawili kwa amri na maelekezo ya captain Bill Jewell walifungua NATI za mlango wa kifaa hiki kama pipa kubwa la chuma na kuutoa mwili wa mincemeat au Major William Martin .
Kwa uangalifu mkubwa brifecase aliyokuwa amefungwa nayo
Briefcase hiyo ya ngozi yenye nembo ya kifalme (Royal coart of arm), ilifunguliwa na kuwekwa nyaraka za Siri na barua alizokuwa amekabidhiwa captain Bill Jewell na Ewen Montagu kisha alaziweka kwa uangalifu ndani ya briefcase hiyo na kuifunga.. baada ya hapo funguo za brifecase hiyo zikawekwa kwenye mfuko wa nguo alizovaa huyu marehemu pamoja na kadi ya kitambulisho yenye picha yake... na baadhi ya vitu vingine ikiwemo life jacket litakalowezesha hii maiti kuelea baharini. Zoezi lililochukua karibu nusu saa. Baada ya kukamilika hili zoezi, Bill Jewell akawaamuru maafisa wake watatu waibebe hiyo maiti na kuiweka baharini taratibu kisha ielee ikiwa na brifecase yenye document za Siri...

Huyu bwana Jewell baada ya kushuhudia mincemeat ameachwa baharini , mbele ya Maafisa wenzake kabla ya kurudi ndani ya nyambizi alitamka Maneno kadhaa kama sala ambayo yalikuwa ni ZABURI YA 39🤣🤣🤣 kama ishara ya kuuaga huu mwili wa Mincemeat 🤣😂😂😂😂.
Nyambizi ikarudi baharini katikati na kuharibu na kukizamisha kifaa kilichokuwa kimebeba maiti ya mincemeat au Major William Martin.
Ilipofika majira ya asubuhi ya saa moja na robo hivi, Captain bill Jewell alituma jumbe za siri kwenda makao makuu ya Admirality yaliyopo London uingereza , uliosomeka *"Mincemeat Completed" * na *"parcel delivered safely" *
Safari ya nyambizi hii kuelekea Afrika kaskazini ikaendelea kama ratiba yake ilivyopangwa📍📌🔨📌💢🔨📌📍






..



ACHA SASA TUKATEMBEE UHISPANIA 😎😎😎😎
 
Screenshot_20260125-135515~2.jpg

Kifaa hiki mfano wa pipa kilichoandikwa FOS . Kilikuwa na urefu wa kama futi sita na upana wa mita mbili. Ndicho kilichohifadhi mwili wa Major William Martin au Mincemeat kwa ajili ya kusafirishwa kwa kutumia nyambizi Ya H.M.S SERAPH kutoka bandari ya Scotland hadi bahari ya Mediterranean. Sadati iliyochukua takribani wiki na siku kadhaa
 
Kitambulisho cha major William Martin.
Screenshot_20260111-175451~2.jpg

Kiuhalisia kitambulisho hiki kilikuwa ni feki karibia kila kitu.. kwa mfano jina , lilikuwa ni la afisa mwingine kabisa,namba ya kitambulisho yaani naval identity card no.148228 ilikuwa ni Namba ya utambulisho wa Ewen Montagu na picha hii ilikuwa ni ya afisa wa MI6 ambaye alikuwa ni fundi mitambo ya redio ya BBC aliyeitwa Ronnie Reed
 
SEHEMU YA TISA

ASUBUHI NA MAPEMA KUSINI MWA HISPANIA
Baada ya Jose Antonio Rey Maria pamoja na wavuvi wengine kuendelea na mishe zao za uvuvi kama kawaida , asubuhi yote ya siku hii maiti iliyookotwa baharini iliachwa imelala mchangani kwenye kivuli . Nzi nao wakiruka huku na kule kuizunguka.

Sasa kadiri kulivyokuwa kukikucha na jua kuanza kuwa Kali, nao mchanga ule wa ufukweni ulikuwa ukipata joto na hii ikasababisha maiti hii kuendelea kutoa Harufu Kali sana .

Sasa maiti hii ikiwa imelala hapo mchangani , Kuna baadhi ya watu kadhaa ikiwemo maafisa wa serikalini na wa mtaa wa Punta Umbria walikuja kuona na kushuhudia hii maiti baada ya wambea wa hapo mtaani kusambaza Taarifa kuhusiana na kupatikana kwa maiti ya mwanajeshi baharini. Hii haikuwa big deal sana maana wambea wapo kila mahali (hata hapa Jf wambea wapo tu 🤣🤣) Na ilitarajiwa hali hii.

Sasa moja ya watu waliokuja kushuhudia hii maiti alikuwa ni afisa wa kijeshi aliyeitwa Mariano Pascual del pobil ambaye alikuwa ni kamanda wa kikosi Maalum cha kijeshi mahsusi kilichokuwa kikifanya doria ya miguu kwenye pwani ya huelva kilichojulikana kama 2nd battalion of seventy-second battalion infantry regiment . Afisa huyu akatoa Taarifa kwa mamlaka ya kipolisi kwenye mji mdogo wa Punta Umbria kuhusiana na kupatikana kwa maiti hii ya mwanajeshi kwenye fukwe za La bota. Baada ya polisi kupokea Taarifa hizi , nao polisi wakawasilisha Taarifa kwenye mamlaka ya bandari ya Port Huelva kuhusiana na tukio hili. Sasa ikaonekana kwamba kwa kuwa maiti iliyopatikana alikuwa ni mwanajeshi, basi jukumu la kiupelelezi na taratibu zingine likaachiwa maafisa wa kijeshi(under military jurisdiction) wa deal nalo. .

Kabla ya kuondoka huyu afisa mwenye cheo kikubwa eneo hilo, aliamua kufanyia upekuzi kiasi maiti hii . Kwanza aliitambua briefcase hii iliyokuwa na nembo ya kifalme yaani "Royal crown" ambayo ilikuwa imefungamanishwa na chain kwenye mwili wa mtu huyu.

Pia afisa huyu Pascual del pobil aliweza kupekua maiti hii kwenye mfuko wa suruali na kukutana na pochi ambapo aliweza kutoa kitambulisho cha maiti hii na kusoma jina lake likiwa linamtambulisha kama Major William Martin.
Baada ya hapo aliifungua cheni iliyokuwa imefungwa brifecase pamoja na maiti na kuitoa briefcase hiyo kwa ajili ya kuondoka nayo.. huyu afisa Kuna kitu alisahau kutoa kwenye mfuko wa maiti hii;FUNGUO ZA HII BRIEFCASE . Anyway haikuwa big deal sana... Hivyo huyu afisa akatoa amri maiti hii isafirishwe na kupelekwa hadi kwenye mji wa Huelva kwa ajili ya kwenda kuhifadhiwa na kusubiria taratibu zingine.

Kabla ya maiti hii kuondolewa , daktari wa Eneo hili aliitwa na kutakiwa kudhibitisha kwamba mwili huu tayari umeshakufa ili taratibu zingine zifuatwe.

Sasa maiti ilitakiwa kubebwa na kuondolewa Eneo hili.
Ikumbukwe kwamba kutoka eneo hili hadi kwenye bandari ndogo ya punta Umbria kulikuwa hakuna barabara zaidi ya njia iliyokuwa mchanga ambapo gari isingeweza kupita , hivyo maiti hii ikapakiwa kwenye punda vizuri kisha kachalii kadogo kakawa kanaongoza huyu punda hadi eneo la Punta Umbria huku nyuma akifuatwa na wanajeshi wawili kwa mguu kuisindikiza kwa ajili ya kusafirishwa na boti hadi mji wa Huelva asubuhi inayofuata.

Afisa huyu bwana Pascual del pobil alitoa Taarifa kwenye ubalozi wa uingereza mjini Madrid kuhusiana na kupatikana kwa afisa wa jeshi wa kiingereza kwenye fukwe za La bota mapema asubuhi baada ya kuokotwa na mvuvi aliyekuwa akivua samaki asubuhi.

Taarifa hii ya kupatikana kwa maiti ilimpa ahueni naibu balozi wa uingereza aliyekuwa anahudumu kwenye ubalozi wa Madrid aliyeitwa Francis haselden. Afisa huyu wa ubalozi alikuwa akiisubiria taarifa hii kwa hamu kubwa kwakuwa alikuwa akiitegemea muda wowote kwakuwa naye alikuwa amepewa Taarifa hapo kabla na kamati ya Twenty Committee kwamba atarajie kusikia Taarifa za kupatikana kwa maiti.

Huyu Haselden Kuna maagizo maalum aliachiwa endapo maiti hii itapatikana na Gomez-beare ambaye nilikutaarifu awali alikuwa ni naval attachê wa maswala ya jeshi Hususani kwenye maswala ya jeshi la majini ambaye alikuwa akifanya kazi ubalozi wa uingereza mjini Madrid .

Maagizo haya ilikuwa kama ifuatavyo: endapo Huyu Haselden atapata Taarifa za kupatikana kwa maiti ya mwanajeshi wa uingereza pamoja na vitu alivyopatikana navyo(brifecase) kwenye fukwe za Hispania,basi ilimpasa apige simu kwenda kwa huyu Gomez beare kumjulisha. Kisha huyu Gomez atoe maelekezo ya namna ya kuzikwa kwa huyu mtu aliyekufa huku akisubiri Taarifa zingine kutoka makao makuu uingereza.
Baada ya hapo huyu Haselden ataulizwa kwa njia ya simu kama huyu mtu mfu Kuna nyaraka amepatikana nazo zikiwa kwenye briefcase, kisha haselden atasema zimepatikana ila "hawawezi kuziongelea kwenye simu ni nyaraka za aina gani ". Zingatia hapa kwenye mabano.

Nataka nikueleweshe kitu hapa ili uelewe kwa makini.
Huyu Gomez-beare alikuwa anajua fika kabisa simu karibia zote zilizokuwa zinapigwa kwenye ubalozi wa uingereza mjini Madrid tayari zilikuwa zimedukuliwa kwa maana kwamba zilikuwa zinasikilizwa kwa Siri (bugged) na mtandao wa majasusi wa jeshi la Ujerumani la Nazi.

Hivyo mazungumzo na maelekezo haya kwa njia ya simu kati ya haselden na Gomez-beare yalitarajiwa kusikilizwa na mtandao wa kijasusi wa ujerumani uliokuwa ukiendesha operesheni zake za kukusanya Taarifa za kijasusi hapo Hispania ambao baadhi yao walikuwa wamepandikizwa kwa Siri sana hadi ndani ya ubalozi wa uingereza hapo Madrid Hispania. Huyu Gomez-beare alikuwa na hakika mazungumzo haya yangewafikia wajerumani baada kudukua simu. Na ilikusudiwa iwe hivyo😎😎.

Sasa kabla hatujaenda deep nataka nikujulishe jambo hapa.
Mbali na nchi ya uhispania kipindi hicho cha vita kuu ya pili ya dunia kuwa neutral yaani haifungamani na upande wowote ule, hii ilitoa nafasi kwa majasusi wa pande zote kwa maana ya ujerumani na Alliance (uingereza, Ufaransa marekani) kuendesha shughuli zao za Siri pasipo usumbufu kutoka kwenye mamlaka ya nchi ya uhispania, wakati huo ikiongozwa na Jenerali Franco.

Sasa wajerumani walikuwa na mtandao wao mpana wa kijasusi uliokuwa ukikusanya kila aina ya Taarifa iliyofaa ndani ya uhispania na kuziripoti makao makuu huko Berlin ukilinganisha na(allied nations) . Mtandao huu wa kijasusi ndani ya uhispania ulikuwa ukiongozwa na Spymaster aliyejulikana kama Adolf Claus. Huyu jamaa alikuwa kama Sniffing dog yaani mbwa anayenusa . Hii ilikuwa ina maana kwamba Taarifa yoyote ile ya kweli au ya umbea alikuwa anaichukulia kwa uzito na kuituma makao makuu Berlin.

Sasa huyu naibu balozi au vice -consul Haselden aliachiwa jukumu la kuhakikisha kila maelekezo aliyopewa anayafanyia kazi kwa uangalifu kwakuwa majasusi wa ujerumani nao walikuwa wapo "Vigilant".
Kwa kifupi huyu Haselden hakuwa na taaluma ya maswala ya Sanaa ya ujasusi hivyo ilibidi awe makini .
Haselden ilimpasa ajifanye ni afisa ambaye anaharakishwa na wakubwa wake huko London katika kuhakikisha nyaraka zilizokuwa na huyu marehemu mincemeat zinapatikana na kurudishwa kwenye ubalozi wa uingereza..

Hii hali ya kujifanya kuharikishwa ,kungetengeneza "Attention" kwa majasusi wa ujerumani. Hii ingefanya mtandao wa majasusi wa ujerumani ukiongozwa na Adolf Claus kutaka kujua haswa na ikiwezekana kuzipata nyaraka hizo na kujua zilikuwa zinahusiana na nini. Anyway.....

Sasa baada ya maiti hii kuwasili asubuhi na Feri hadi kwenye bandari ya huelva ikitokea punta Umbria ilikuja kupokelewa na mtu maalum ambaye alikuwa akihusika na kutoa huduma za kuzika watu yaani "undertaker" aliyeitwa Emilio Morales Candela.
Kwa maelekezo ya vice consul Francis Haselden, huyu bwana candela aliamriwa aisafirishe maiti hii hadi kwenye eneo la kuzikia.

Na kweli huyu bwana candela baada ya maiti hiyo kuwasili hapo huelva aliiweka kwenye geneza la mbao kisha akaipakia kwenye gari la mkokoteni uliokuwa unavutwa na farasi lililokuwa linamilikiwa na La Magdalena Funeral services of Huelva.

Kila hatua iliyokuwa ikifanyika ilikuwa inafuatiliwa kwa karibu na huyu Haselden. Na kweli safari ya kuelekea makaburini ilianza huku farasi aliyebeba geneza la huyu marehemu akiongozwa na huyu Candela huku Haselden akifuatilia kila hatua kwa karibu akiwa na gari lake .
Sasa mkokoteni huu uliobeba hii maiti ulikatiza kwenye mitaa kadhaa ndani ya huu mji wa huelva , ikiwemo Concepçion.
Watu wa eneo hili walikuwa wamepata habari kwamba kuna mwili wa mwanajeshi wa uingereza uliookotwa baharini unapita ukiwa unakokotwa na farasi 😎😎.Wambea wambea nao walijitokeza pembezoni mwa njia kushuhudia.
Watu kadhaa walikusanyika nje ya kanisa la katoliki la Nuestra Señora de Lourdes lililokaribu na uwanja wa kuzikia watu wakishuhudia maiti hii ikipitishwa. Wengine wakifanya ishara ya msalaba na kusali kimyakimya kuiombea maiti hii mmojawapo akiwa padri wa kanisa hilo Father Josè Manuel Romero Bernal.
Maiti hii ikiwa imebeba kwenye mkokoteni wa farasi iliendelea kukatiza mitaa kadhaa hadi kwenye uwanja wa Makaburi wa Nuetra Senora del la Soledad ambalo eneo hili kijiografia lipo kama kwenye kilima hivi kiasi nje ya mji wa huelva kidogo.
Sasa kwenye malango haya ya kuingia eneo hili la cemetery , kulikuwa na mtu anasubiri hapo. Hakuwa mwingine bali ni luteni Pascual del pobil ambaye nilikutaarifu awali ndio aliyeichukua briefcase ambayo iliambatana na huyu marehemu kule ufukweni na tayari alikuwa nayo ameishikilia mkononi.

Luteni huyu hakuwa peke yake hapo kwenye lango la kuingia Makaburini ,bali alikuwa ameambatana na watu wawili ambao kitaaluma walikuwa ni madaktari na waliotarajia kufanya upasuaji wa maiti hii pindi itakapofika. Madaktari hawa walitambulika kama Eduardo Fernàndez del Torno pamoja na mwanaye daktari aliyeitwa Eduardo Fernàndez Contioso. Na mtu mwingine ambaye alikuwepo katika jopo hili la watu wakisubiri hii maiti kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji alikuwa ni raia wa kimarekani aliyeitwa Willie Watkins....... Ngoja nikudokezee jambo hapa kidogo kuhusu huyu raia wa marekani.


Ipo hivi siku tatu nyuma kabla ya maiti hij haijapatikana ikielea ufukweni kule punta Umbria ni kwamba Kuna ndege ndogo aina P-39 aircobra ilitua kwa dharura(crash landing ) kwenye mojawapo ya shamba eneo la punta Umbria na rubani wa ndege hii alikuwa huyu Watkins ila bahati nzuri hakupata majeraha baada ya ndege yake iliyokuwa ikitoka Afrika kaskazini kuelekea ureno kuishiwa mafuta na kuanguka mashambani. Huyu bwana alikamatwa na wanajeshi waliokuwa wakifanya patrol eneo la Punta Umbria na kusekwa rumande. Baadaye huyu Watkins alitolewa na kuhifadhiwa nyumbani kwa Francis Haselden kwakuwa hakukuwa na ubalozi wa marekani hapo kwenye mji wa huelva.

Hivyo basi luteni Pascual del pobil alitoa maelekezo huyu Watkins awepo eneo hili la cemetery aweze kuutambua mwili wa huyu mwanajeshi aliyeokotwa kama anamfahamu na ina connection ya namna yoyote ile na ndege iliyoanguka...

Maiti hii ilipowasili ikiwa ndani ya geneza la mbao , ilibebwa hadi kwenye nyumba moja ambayo ilikuwa ikitumika kama mochwari na eneo la kuandalia maiti kabla ya kuzikwa.

Maiti ya huyu mtu ilinyanyuliwa juu na kuwekwa kwenye meza ya sementi hivi Kwa ajili ya taratibu za kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu (body autopsy) 🔎🔎.

HAPA KIMBEMBE NDIO KINAANZIA. 🤔









Sasa mwili wa huyu mwanajeshi aliyeokotwa, yaani Major William Martin au jina lake halisi Glyndwr Michael baada ya kulazwa juu ya meza maalum zile za mochwari, ilifanyiwa upekuzi kwanza mfukoni. Na ikakutwa ikiwa na vitu kadhaa binafsi ambavyo mtu yoyote yule anaweza kuwa navyo mfukoni mwake; pesa kiasi cash, pakti ya sigara, funguo,kiberiti, saa, risiti, kadi ya kitambulisho, wallet , stampu pamoja na karatasi za tiketi .

Vitu hivi vilitolewa na kuwekwa juu ya meza pamoja na brifecase ambayo awali ilikuwa imechukuliwa na Pascual del pobil.
Huyu luteni de pobil hakuvitilia maanani vitu hivi vilivyokuwa mfukoni mwa hii maiti, zaidi alichukua funguo kwa ajili ya kufungua hii briefcase kujua nini kilichomo ndani..
Haya yote yakiendelea Francis Haselden alikuwa yupo pembeni akiangalia kila kitu kilichokuwa kikiendelea kwa umakini wa hali ya juu sana ila akizuga kama hakuwa anatilia maanani sana.

Baada ya huyu afisa Pascual pobil kufungua briefcase hii ,kila kilichomo humo ndani kilikuwa kimelowa na maji . Bahasha zilizokuwa na barua ndani zilolowana lakini majina yaliyokuwa yameandikwa juu yake pamoja na mihuri yalikuwa yanasomeka vizuri kabisa.

Haselden aliitwa aje aziangalie na kwa namna vilivyokuwa zimefungwa ilimaanisha kwamba barua hizi zilikuwa ni za umuhimu wa Hali ya juu bena zimetoka kwenye mikono ya mtu au watu wenye vyeo vizito sana ndani ya jeshi la uingereza.

Kumbuka huyu Haselden alikuwa akijua barua hizi zilikuwa zinahusiana na nini kwakuwa tayari alikuwa amepewa briefs kuhusiana na operation mincemeat.

Sasa huyu luteni Pascual del pobil baada ya kuziangalia hizi bahasha na kujiridhisha zilikuwa ni za uingereza alitaka kumkabidhi huyu Haselden (kitu ambacho hakikuwa kinatarajiwa) .
Haselden alikataa kuondoka na nyaraka hizi kwa kutoa sababu moja ya kipekee sana. Alimwambia huyu pobil asingeweza kuondoka nazo pasipo Nyaraka hizi kupitia kwa mkubwa wake ambaye alikuwa ni Naval commander wa bandari kwenye mji wa huelva kisha ndio ataweza kuzichukua na kuzirudisha uingereza kwa kufuata protokali.😎😎😎😁.


Kumbuka mpaka hapa barua hizo hazijafunguliwa kujua nini kilichokuwa kimeandikwa humo.

Baada ya huyu Haselden kukataa kuondoka na hii brifecase na vitu vingine vya huyu marehemu, afisa Pascual del pobil alivichukua na kuondoka navyo akimwacha Haselden hapo akiendelea kushuhudia zoezi la upasuaji wa hii maiti ukiendelea.

Kiitifaki ni kwamba , maiti hii ilipaswa kufanyiwa upasuaji na daktari maalum wa kijeshi yaani military pathologist lakini kwakuwa hakuwa karibu ,zoezi hili alikabidhiwa daktari Fernàndez na kijana wake .
Huyu Watkins, rubani wa kimarekani aliamua kutoka nje na kwenda kuvuta sigara. Hakutaka kushuhudia huu mwili uliooza ukikatwakatwa kwa ajili ya zoeZi la upasuaji kutokana na Harufu ya muozo uliokuwa mle ndani .


Sasa basi Licha ya kusemekana kwamba nchi ya uhispania haikuwa na madaktari bingwa wa upasuaji kipindi hicho, lakini huyu Dr. Fernàndez alikuwa na uzoefu sana kuhusiana na taaluma hii ya upasuaji wa miili ya watu kwa miaka kadhaa lakini hii haikumfanya kuwa daktari bingwa wa upasuaji.

Zoezi la upasuaji likaanza , ngozi ya nje ya mwili huu haikuwa imeharibika sana lakini kisu kilipopitishwa kuukata mwili huu haswa sehemu ya kifuani, viungo vya ndani vilikuwa vimeharibika kiasi kwamba chumba hiki kilijaa Harufu moja mbaya sana . Sehemu ya mapafu ya hii maiti ilikuwa imejaa maji na daktari Fernàndez asingeweza kudhibitisha moja kwa moja kwamba maiti hii ilikufa maji kutokana na mapafu kuharibika sana.

Baada ya hapo daktari huyu aliangalia(minor examination ) sehemu kadhaa za mwili huu Ikiwemo masikio, nywele za kichwa pamoja na rangi ya ngozi ya huu mwili iliyoanza kupotea kabisa kutokana na kuharibika.
Kumbuka hapa huyu Haselden alikuwa akifuatilia kila hatua ya upasuaji aliyokuwa akiifanya huyu daktari Fernàndez pamoja na kijana wake .
Haselden alipoona kama huyu daktari anataka kwenda deep sana kwenye kutaka kujua chanzo cha kifo cha huyu mtu , alimwambia huyu daktari haina haja ya kuichunguza sana hii maiti kwakuwa imeharibika sana kutokana na joto kali.
Hivyo daktari Fernàndez alijaza fomu maalum na kutoa remarks zake kama daktari iliyoandikwa hivi :.nanukuu.
" young British officer fell in the water while still alive, showed no evidence of bruising, and drowned through asphyxia caused by submersion. The body had been in the water between eight and ten days".

Hii ina maana daktari Fernàndez alihitimisha kifo cha mtu huyu kilitokana na kukosa hewa (asphyxia) baada ya kuanguka majini ,na mwili wake haukuwa na dalili za mchubuko wa aina yoyote ile na ulikaa kwenye maji kwa karibia siku nane hadi kumi 🤔🤔🤔🔎.
Baada ya hapo mwili ukarudishwa vizuri kwenye sanduku na kwenda kuhifadhiwa, kusubiri taratibu zingine kufuatwa za maziko.


Sasa hapa nataka nikudokezee jambo kidogo uelewe.. Huyu daktari Fernàndez nilikueleza hapo kabla alikuwa mzoefu katika taaluma hii ya upasuaji lakini hakuwa amekidhi vigezo ambavyo tunaweza sema ni daktari bingwa wa upasuaji. Kwanini?
Ipo hivi kama huyu daktari angekuwa makini na taaluma yake ya upasuaji Kuna vitu kadhaa angebaini kwenye hii maiti ya major William Martin aliyoifanyia upasuaji na kubaini haikuwa imekufa kwa sababu ya kuzama majini.🤔🤔👁️.

Kwanza angejiuliza swali hili, kama maiti hii ilikaa kwenye maji kwa takribani siku nane hadi kumi mbona nywele za kichwa hazikuwa zimenyonyoka na bado zilikuwa na rangi ile nyeusi ya asili? Kikawaida maiti iliyokaa kwenye maji muda mrefu nywele za kichwa hunyofoka na pia hubadilika rangi kutokana na kemikali na madini ya chumvi chumvi yaliyopo kwenye maji ya bahari.

Pili angejiuliza pia mbona ngozi ya hii maiti ilibadilika rangi na kuwa kama na weusi? Kama angekuwa makini kuchunguza sampuli za ngozi ya hii maiti , angebaini mtu huyu alikufa kwa sumu aina ya phosphorus ambayo baada ya muda fulani hubadilisha rangi ya ngozi na kuwa na weusi kama side effects na sio kufa maji.

Pia huyu daktari angejiuliza pia akilini mwake kama kweli maiti hii ilikaa kwenye maji kwa karibia siku kumi mbona sehemu za masikio na sehemu nyingine laini za mwili huu hazikuwa zimeliwa au kutafunwa na samaki wadogo au baharini ?🤔🤔🔎. Angetambua hili angekuwa na mashaka juu ya kisababishi cha kifo cha huyu mtu .
Na la zaidi daktari huyu angetambua pia nguo za hii maiti zilikuwa zimeloa kwa kukaa kwenye maji lakini zilionekana bado zina ile hali ya kutojikunja sana ukilinganisha na nguo iliyokaa kwenye maji kwa muda mrefu. Hii ingekuwa red flag .

Na la zaidi huyu daktari Kuna kitu hakuweza kukitambua au kuking'amua kwa haraka kuhusiana na kiwango cha kuharibika kwa hii maiti ya major William Martin au Mincemeat. Daktari huyu aliamini maiti hii Ilikaa kwenye maji kwa karibia siku nane hadi kumi.

Lakini Kwa mujibu wa ushahidi wa baadhi ya vitu alivyokuwa navyo mfukoni huyu marehemu baada ya kufanyiwa upekuzi ilionekana tiketi alizokuwa amebeba ilionekana Major William Martin aliondoka LONDON tarehe 24 April ,lakini maiti yake iliokotwa majira ya asubuhi tarehe 30 April .🤔🤔🤔
Maana yake maiti hii ilikaa kwenye maji kwa karibia siku 5 hivi. Lakini Kwa muda wote huu ilivyokaa baharini na kiwango cha kuharibika vilikuwa haviendani hata kidogo .👁️👃👁️. 🔎 🤔. Kwa kifupi daktari Fernàndez alishindwa kutambua ni lini hii maiti ilikufa haswa.

Hatuwezi mlaumu daktari huyu sana kwa sababu moja nataka nikupe hapa.

Kiuhalisia nchi ya uhispania ni nchi ambayo dini ya Roman Catholic imekita mizizi sana. Hivyo kwa imani ya dini ya katoliki hairuhusiwi na ni mwiko kuifanyia maiti uchunguzi wa kitabibu kutaka kujua sababu za kifo cha mtu.. Ni kama tu kwenye dini ya kiislamu mtu akifa, ndani ya masaa 24 au 48 awe ameshazikwa😐😐😐🔎🔎🔎🔎🔎🔎📍📍🔨📍🔨📍.




Anyway tuendelee.......



Ilipofika majira ya usiku wa saa mbili huyu vice consul Francis Haselden alituma ujumbe Maalum kwa simu kwenda kwenye ubalozi uingereza huko Madrid na kuwasiliana na Naval attachê bwana Don Gomez-bearre . Ujumbe huu nanukuu:

"With reference to my phone message26 today body is identified as Major W. Martin R.M. identity card 148228 dated 2nd Feb. 1943 Cardiff. Naval judge has taken possession of all papers. Death due to drowning probably 8 to 10 days at sea. I am having funeral Sunday noon.”

Ndivyo ujumbe huu ulivyobainisha . Ukiisoma hii meseji Kuna mahali imetajawa Naval judge. Huyo jaji ni Pascual del pobil kitaaluma alikuwa ni mwanasheria.

Sasa nataka nikudokezee jambo hapa. Huu ujumbe uliotumwa kwenda kwa naval Attachè aliyeko Madrid uhispania ulitarajiwa kumfikia Gomez bearre , lakini nilikujulisha simu au jumbe za telegram zilizokuwa zinatoka na kuingia ndani ya ubalozi huu wa uingereza tayari kwa namna yoyote zilikuwa zinasikilizwa au kusomwa kwa Siri baada ya kuwa "intercepted" na baadhi ya watu fulani fulani ambao kiuhalisia walikuwa mapandikizi ya mtandao wa kijasusi wa Ujerumani uliokuwa ukisimamiwa na mtu mmoja ndani ya mji wa huelva ambaye nilikudokezea anaitwa "Adolf Clauss.
Huu mtandao wa siri wa kijasusi haikumaanisha ni wajerumani,la hasha kwa mfano gavana wa jimbo hili la huelva pamoja na msimamizi mkuu wa bandari hii ya huelva na maafisa kadhaa wa ngazi za juu wa kiutawala wa jimbo hili la huelva,wote hao walikuwa kwenye Payroll ya huyu Adolf Clauss. Watu hawa kiuhalisia walikuwa na acces ya Taarifa zozote zile ambazo zingekuwa interested kwa wajerumani.

Sasa ni wazi kwamba nyaraka hizi za Siri zilipaswa kuangukia mikononi mwa wajerumani, lakini kama isivyo bahati zikawa mikononi mwa mamlaka za Hispania.. shida iliyojitokeza ni kwa namna gani nyaraka hizo zitaangukia mikononi mwa wajerumani?.


Anyway....


Sasa siku ya Tarehe 2 mwezi mei 1943, ndio ilikuwa siku rasmi ya kumzika huyu Afisa William Martin 😎 kama ratiba ilivyopangwa na ubalozi wa uingereza huko Hispania. Kwa kifupi huyu bwana alikuwa anazikwa ndani ya nchi ya uhispania.

Viongozi na maafisa kadhaa wa ngazi mbalimbali walitarajiwa kuhudhuria mazishi ya huyu Mwanajeshi aliyekufa maji🤣😎.
Baadhi ya Maafisa na viongozi hawa waliohudhuria mazishi haya ni pamoja na naibu balozi wa uingereza nchini Hispania bwana Francis Haselden mwenyewe, Pascual del pobil pamoja na kamanda Elvira, msimamizi wa bandari ya mji wa Huelva.
Gavana wa jimbo hili la Huelva hakuhudhuria kutoa heshima zake za mwisho ila aliweza kutuma mwakilishi.

Kwa kifupi huyu major William Martin au Mincemeat alitarajiwa kuzikwa kwa taratibu na heshima zote za kijeshi kutokana na aina ya wahudhuriaji walipofika kutoa heshima zao za mwisho.

Cheti cha kifo cha major William Martin kilisainiwa rasmi na msimamizi wa mazishi bwana Candela kwa maelezo yafuatayo:

W. Martin, aged between 35 and 40, native of Cardiff (England) , officer of the British marines, found on the beach known as ‘La Bota’ at half past nine on April 30th, 1943. Death by drowning.”

Baada ya taratibu za kuuaga mwili huu Ikiwemo na risala fupi kusomwa , geneza la Major William Martin lilibebwa kwa ajili ya kwenda kupumzishwa kwenye eneo la Makaburi ya San Marco. Eneo hili huzikwa watu wenye kipato cha chini . Haselden aligharamia eneo hili la kuzikia kwa kukodi kwa pasetas 250.

Eneo hili la Makaburi ya San Marco hulipiwa kuzika mtu wako na kulipa gharama za kutunza kaburi (mfano kufyeka nyasi,n.k). Na endapo ukashindwa kulipa gharama za kila mwezi basi mwili hufukuliwa na kwenda kuzikwa sehemu nyingine . Hivyo Haselden alilipia gharama zote hizi kwa niaba ya ubalozi wa uingereza mjini Madrid.

Sasa ilipofika saa sita na nusu mchana , geneza la Major William Martin lilishushwa kaburini huku Haselden akijua fika kwenye akili yake anayezikwa hakuwa afisa wa jeshi maji la uingereza na wala jina la William Martin halikuwa jina lake halisi⚠️⚠️⚠️📍📍.

Kwa kifupi ni kwamba major William Martin au Glandyr Michael raia maskini kabisa mwenye asili ya Wales alizikwa kama raia wa uingereza na kuzikwa kwenye nchi ya ugenini ya uhispania kama afisa wa jeshi la maji mwenye cheo cha umeja. 😑😑😑😑🥺🥺🥺.

Kwenye kaburi la huyu major William Martin au Glandyr Michael kuliandikwa maandishi ya kilatini yaliyosomeka kama ifuatavyo "DULCE ET DECORUM EST PRO PATRIA MORI" . Msemo huu ni kutoka kwenye kitabu cha mashairi kinachoitwa Odes kutoka kwa mwandishi wa kiitaliano aliyeitwa HORACE wa Karne ya 23B.C.
Tafsiri ya msemo huu usio rasmi unamaanisha "Ni Raha sana na inafaa kabisa kufa kwa ajili ya nchi yako"

Baada ya taratibu za kuushusha kaburini mwili wa marehemu , mzikaji akiendelea kufukia kaburi nao maafisa waliohudhuria akiwemo Haselden walipanda magari yao na kuondoka.

Lakini katika shughuli hii ya kumzika huyu marehemu,yupo mtu MMOJA alikuwa akifuatilia shughuli nzima kwa ukaribu na umakini wa hali ya juu sana . Hakuwa mwingine bali ni Adolf Clauss ambaye hapo awali nilikujulisha awali alikuwa ni afisa wa kijasusi wa Ujerumani ambaye alikuwa akifanya kazi ya kukusanya Taarifa zozote zile za kijasusi kwa niaba ya jeshi la Nazi la ujerumani kupitia kitengo cha kijasusi cha jeshi la Nazi kilichojulikana kama ABHWEIR.
Huyu bwana alikuwa anafuatilia kila kitu kuhusiana na shughuli hii nzima ya mazishi ya huyu Mwanajeshi aliyekufa maji wa uingereza.

Kwa kifupi huyu bwana alikuwa anajaribu kwa kila njia namna ya kupata briefcase hii iliyokuwa na barua zile za Siri alizokuwa nazo huyu mtu aliyezikwa.........

Zipo na na nani na atazipataje. Lilikuwa ni swali ambalo Adolf Clauss pengine alijiuliza.
 
Screenshot_20260112-165349~2 (1).jpg

Kaburi la Major William Martin alikozikwa huko Hispania kwenye eneo la Makaburi ya San Marco....inadaiwa mpaka Sasa kaburi hili hutembelewa kwa ajili ya kufanyiwa kumbukumbu na sala fupi kila mwaka katika kumuenzi huyu Glandyr Michael
 
mcTobby , nisamehe
Hii naijua nje ndani

Operesheni Mincemeat,
Ulikuwa ni mpango wa siri wa Uingereza mwaka 1943 wakati wa Vita vya Pili vya Dunia uliolenga kuwapotosha Wajerumani kuhusu mipango ya uvamizi wa Washirika.
Maafisa wa ujasusi wa Uingereza walitengeneza mpango wa ajabu: waliweka nyaraka za uongo kwenye mwili wa mtu aliyekufa na kuuacha baharini karibu na Hispania ili Wajerumani waamini kuwa Washirika walikuwa wanapanga kuvamia Ugiriki badala ya Sicily. Mpango huo ulifanikiwa kwani Adolf Hitler aliamini taarifa hizo na kuhamisha majeshi kwenda kulinda Ugiriki na maeneo mengine, hivyo uvamizi halisi wa Sicily ulipofanyika Wajerumani walikamatwa bila maandalizi.

Ili kufanya mpango huo uonekane halisi, maafisa Ewen Montagu na Charles Cholmondeley walimpa marehemu utambulisho mpya kama afisa wa jeshi aitwaye William Martin. Walitengeneza historia kamili ya maisha yake, ikiwa ni pamoja na barua za mapenzi, stakabadhi za benki, na hata mchumba wa kubuniwa.

Mpango huo ulivutiwa na mawazo ya waandishi na hata ulihusishwa na mwandishi wa James Bond, Ian Fleming, ambaye alichangia mawazo ya mbinu za udanganyifu wa kivita.
Mwili uliotumika ulikuwa wa Glyndwr Michael, mtu maskini kutoka Wales ambaye hakuwa na familia, na maisha yake yalitumiwa kama chombo cha vita. Hili lilizua mjadala kuhusu maadili ya kutumia mwili wa mtu kwa madhumuni ya kijeshi.

Hii ilikuwa ni mojawapo ya mbinu za ajabu zaidi za udanganyifu katika historia ya vita na mpango wa siri wa Uingereza uliolenga kumpotosha kiongozi wa Nazi, Adolf Hitler, wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.
Mwaka 1943, mataifa ya Washirika yalikuwa yanajiandaa kuivamia Ulaya kupitia kisiwa cha Sicily. Tatizo lilikuwa wazi: Wajerumani walitarajia uvamizi huo. Ili kufanikiwa, Waingereza walihitaji kuwafanya Wajerumani waamini kuwa uvamizi ungefanyika sehemu nyingine na hasa Greece, Hapo ndipo mpango wa ajabu ulipozaliwa.

Wazo la kutumia maiti kama mjumbe wa siri
Maafisa wa ujasusi wa Uingereza walibuni mpango wa kuweka nyaraka za siri za uongo kwenye mwili wa mtu aliyekufa na kuufanya uonekane kama askari aliyekufa ajalini baharini.

Mwili huo ungeonekana kama umebeba nyaraka muhimu za kijeshi kuhusu mipango ya uvamizi. Walitarajia kwamba maafisa wa Kihispania wangepata mwili huo na, kwa siri, kuwapa Wajerumani taarifa zilizopatikana.
Mpango huo ulihitaji mambo mengi yaonekane ya kweli kabisa na si nyaraka tu, bali maisha kamili ya mtu huyo wa kubuni.

Kuundwa kwa utambulisho wa “Major William Martin”
Mtu aliyekufa alipewa utambulisho mpya: afisa wa Jeshi la Wanamaji wa Uingereza aitwaye Major William Martin.
Maafisa wa ujasusi walitengeneza maisha yake kwa undani mkubwa, wakijumuisha:
  • Barua za mapenzi kutoka kwa mchumba wa kubuniwa
  • Picha ya mwanamke aliyedaiwa kuwa mpenzi wake
  • Risiti za matumizi ya kila siku
  • Tiketi na stakabadhi za benki
  • Barua binafsi za kawaida za maisha ya kila siku
Lengo lilikuwa kuonyesha kwamba alikuwa mtu halisi mwenye maisha ya kawaida, si sehemu ya mpango wa kijeshi.
Hii inaonyesha jinsi ujasusi wa kivita ulivyohusisha pia saikolojia — kuwafanya wapinzani waamini hadithi nzima bila shaka.
Mwili unatupwa baharini karibu na Hispania
Mwili huo uliwekwa baharini karibu na pwani ya Hispania, nchi ambayo ilikuwa haina msimamo rasmi vitani lakini ilikuwa na mawasiliano ya karibu na Ujerumani wa Nazi.
Kama ilivyotarajiwa:
  • Mwili ulipatikana na mamlaka za Hispania
  • Nyaraka zilichunguzwa kwa siri
  • Taarifa zilifikishwa kwa Wajerumani
  • Hatimaye, uongo huo uliaminika.
  • Mafanikio ya mpango dhidi ya Ujerumani
  • Matokeo yake yalikuwa makubwa sana kijeshi.
  • Adolf Hitler aliamini kuwa uvamizi mkubwa ungefanyika Ugiriki badala ya Sicily. Kutokana na hilo:
  • Majeshi ya Ujerumani yalihamishwa kutoka Sicily
  • Ulinzi wa Sicily ulidhoofika
  • Washirika walifanikiwa kuivamia Sicily kwa urahisi zaidi
  • Tukio hili lilisaidia kubadilisha mwelekeo wa vita Ulaya.
Chanzo cha mawazo na mchango wa waandishi
Mpango huu ulichangiwa na mawazo ya ubunifu na hata fasihi.
Ian Fleming — ambaye baadaye aliandika hadithi za James Bond — alikuwa sehemu ya idara ya ujasusi ya Uingereza wakati huo na alichangia mawazo kuhusu mbinu za udanganyifu wa kivita.
Mpango huo unaonyesha jinsi ubunifu, hadithi na saikolojia zilivyotumika kama silaha za vita.
Yeap hii ni nzuri....😄 Utawasaidia wale ambao hawapendi kusoma stori ndefu sana. Lakini kwa wale wanaopenda Kwenda deep zaidi kuhusu hiki kisa bado huu Uzi utawafaa ili wapate ile picha Kamili haswa kuhusiana na hii operesheni..
 
SEHEMU YA TISA

ASUBUHI NA MAPEMA KUSINI MWA HISPANIA









Sasa mwili wa huyu mwanajeshi aliyeokotwa, yaani Major William Martin au jina lake halisi Glyndwr Michael baada ya kulazwa juu ya meza maalum zile za mochwari, ilifanyiwa upekuzi kwanza mfukoni. Na ikakutwa ikiwa na vitu kadhaa binafsi ambavyo mtu yoyote yule anaweza kuwa navyo mfukoni mwake; pesa kiasi cash, pakti ya sigara, funguo,kiberiti, saa, risiti, kadi ya kitambulisho, wallet , stampu pamoja na karatasi za tiketi .

Vitu hivi vilitolewa na kuwekwa juu ya meza pamoja na brifecase ambayo awali ilikuwa imechukuliwa na Pascual del pobil.
Huyu luteni de pobil hakuvitilia maanani vitu hivi vilivyokuwa mfukoni mwa hii maiti, zaidi alichukua funguo kwa ajili ya kufungua hii briefcase kujua nini kilichomo ndani..
Haya yote yakiendelea Francis Haselden alikuwa yupo pembeni akiangalia kila kitu kilichokuwa kikiendelea kwa umakini wa hali ya juu sana ila akizuga kama hakuwa anatilia maanani sana.

Baada ya huyu afisa Pascual pobil kufungua briefcase hii ,kila kilichomo humo ndani kilikuwa kimelowa na maji . Bahasha zilizokuwa na barua ndani zilolowana lakini majina yaliyokuwa yameandikwa juu yake pamoja na mihuri yalikuwa yanasomeka vizuri kabisa.

Haselden aliitwa aje aziangalie na kwa namna vilivyokuwa zimefungwa ilimaanisha kwamba barua hizi zilikuwa ni za umuhimu wa Hali ya juu bena zimetoka kwenye mikono ya mtu au watu wenye vyeo vizito sana ndani ya jeshi la uingereza.

Kumbuka huyu Haselden alikuwa akijua barua hizi zilikuwa zinahusiana na nini kwakuwa tayari alikuwa amepewa briefs kuhusiana na operation mincemeat.

Sasa huyu luteni Pascual del pobil baada ya kuziangalia hizi bahasha na kujiridhisha zilikuwa ni za uingereza alitaka kumkabidhi huyu Haselden (kitu ambacho hakikuwa kinatarajiwa) .
Haselden alikataa kuondoka na nyaraka hizi kwa kutoa sababu moja ya kipekee sana. Alimwambia huyu pobil asingeweza kuondoka nazo pasipo Nyaraka hizi kupitia kwa mkubwa wake ambaye alikuwa ni Naval commander wa bandari kwenye mji wa huelva kisha ndio ataweza kuzichukua na kuzirudisha uingereza kwa kufuata protokali.😎😎😎😁.


Kumbuka mpaka hapa barua hizo hazijafunguliwa kujua nini kilichokuwa kimeandikwa humo.

Baada ya huyu Haselden kukataa kuondoka na hii brifecase na vitu vingine vya huyu marehemu, afisa Pascual del pobil alivichukua na kuondoka navyo akimwacha Haselden hapo akiendelea kushuhudia zoezi la upasuaji wa hii maiti ukiendelea.

Kiitifaki ni kwamba , maiti hii ilipaswa kufanyiwa upasuaji na daktari maalum wa kijeshi yaani military pathologist lakini kwakuwa hakuwa karibu ,zoezi hili alikabidhiwa daktari Fernàndez na kijana wake .
Huyu Watkins, rubani wa kimarekani aliamua kutoka nje na kwenda kuvuta sigara. Hakutaka kushuhudia huu mwili uliooza ukikatwakatwa kwa ajili ya zoeZi la upasuaji kutokana na Harufu ya muozo uliokuwa mle ndani .


Sasa basi Licha ya kusemekana kwamba nchi ya uhispania haikuwa na madaktari bingwa wa upasuaji kipindi hicho, lakini huyu Dr. Fernàndez alikuwa na uzoefu sana kuhusiana na taaluma hii ya upasuaji wa miili ya watu kwa miaka kadhaa lakini hii haikumfanya kuwa daktari bingwa wa upasuaji.

Zoezi la upasuaji likaanza , ngozi ya nje ya mwili huu haikuwa imeharibika sana lakini kisu kilipopitishwa kuukata mwili huu haswa sehemu ya kifuani, viungo vya ndani vilikuwa vimeharibika kiasi kwamba chumba hiki kilijaa Harufu moja mbaya sana . Sehemu ya mapafu ya hii maiti ilikuwa imejaa maji na daktari Fernàndez asingeweza kudhibitisha moja kwa moja kwamba maiti hii ilikufa maji kutokana na mapafu kuharibika sana.

Baada ya hapo daktari huyu aliangalia(minor examination ) sehemu kadhaa za mwili huu Ikiwemo masikio, nywele za kichwa pamoja na rangi ya ngozi ya huu mwili iliyoanza kupotea kabisa kutokana na kuharibika.
Kumbuka hapa huyu Haselden alikuwa akifuatilia kila hatua ya upasuaji aliyokuwa akiifanya huyu daktari Fernàndez pamoja na kijana wake .
Haselden alipoona kama huyu daktari anataka kwenda deep sana kwenye kutaka kujua chanzo cha kifo cha huyu mtu , alimwambia huyu daktari haina haja ya kuichunguza sana hii maiti kwakuwa imeharibika sana kutokana na joto kali.
Hivyo daktari Fernàndez alijaza fomu maalum na kutoa remarks zake kama daktari iliyoandikwa hivi :.nanukuu.
" young British officer fell in the water while still alive, showed no evidence of bruising, and drowned through asphyxia caused by submersion. The body had been in the water between eight and ten days".

Hii ina maana daktari Fernàndez alihitimisha kifo cha mtu huyu kilitokana na kukosa hewa (asphyxia) baada ya kuanguka majini ,na mwili wake haukuwa na dalili za mchubuko wa aina yoyote ile na ulikaa kwenye maji kwa karibia siku nane hadi kumi 🤔🤔🤔🔎.
Baada ya hapo mwili ukarudishwa vizuri kwenye sanduku na kwenda kuhifadhiwa, kusubiri taratibu zingine kufuatwa za maziko.


Sasa hapa nataka nikudokezee jambo kidogo uelewe.. Huyu daktari Fernàndez nilikueleza hapo kabla alikuwa mzoefu katika taaluma hii ya upasuaji lakini hakuwa amekidhi vigezo ambavyo tunaweza sema ni daktari bingwa wa upasuaji. Kwanini?
Ipo hivi kama huyu daktari angekuwa makini na taaluma yake ya upasuaji Kuna vitu kadhaa angebaini kwenye hii maiti ya major William Martin aliyoifanyia upasuaji na kubaini haikuwa imekufa kwa sababu ya kuzama majini.🤔🤔👁️.

Kwanza angejiuliza swali hili, kama maiti hii ilikaa kwenye maji kwa takribani siku nane hadi kumi mbona nywele za kichwa hazikuwa zimenyonyoka na bado zilikuwa na rangi ile nyeusi ya asili? Kikawaida maiti iliyokaa kwenye maji muda mrefu nywele za kichwa hunyofoka na pia hubadilika rangi kutokana na kemikali na madini ya chumvi chumvi yaliyopo kwenye maji ya bahari.

Pili angejiuliza pia mbona ngozi ya hii maiti ilibadilika rangi na kuwa kama na weusi? Kama angekuwa makini kuchunguza sampuli za ngozi ya hii maiti , angebaini mtu huyu alikufa kwa sumu aina ya phosphorus ambayo baada ya muda fulani hubadilisha rangi ya ngozi na kuwa na weusi kama side effects na sio kufa maji.

Pia huyu daktari angejiuliza pia akilini mwake kama kweli maiti hii ilikaa kwenye maji kwa karibia siku kumi mbona sehemu za masikio na sehemu nyingine laini za mwili huu hazikuwa zimeliwa au kutafunwa na samaki wadogo au baharini ?🤔🤔🔎. Angetambua hili angekuwa na mashaka juu ya kisababishi cha kifo cha huyu mtu .
Na la zaidi daktari huyu angetambua pia nguo za hii maiti zilikuwa zimeloa kwa kukaa kwenye maji lakini zilionekana bado zina ile hali ya kutojikunja sana ukilinganisha na nguo iliyokaa kwenye maji kwa muda mrefu. Hii ingekuwa red flag .

Na la zaidi huyu daktari Kuna kitu hakuweza kukitambua au kuking'amua kwa haraka kuhusiana na kiwango cha kuharibika kwa hii maiti ya major William Martin au Mincemeat. Daktari huyu aliamini maiti hii Ilikaa kwenye maji kwa karibia siku nane hadi kumi.

Lakini Kwa mujibu wa ushahidi wa baadhi ya vitu alivyokuwa navyo mfukoni huyu marehemu baada ya kufanyiwa upekuzi ilionekana tiketi alizokuwa amebeba ilionekana Major William Martin aliondoka LONDON tarehe 24 April ,lakini maiti yake iliokotwa majira ya asubuhi tarehe 30 April .🤔🤔🤔
Maana yake maiti hii ilikaa kwenye maji kwa karibia siku 5 hivi. Lakini Kwa muda wote huu ilivyokaa baharini na kiwango cha kuharibika vilikuwa haviendani hata kidogo .👁️👃👁️. 🔎 🤔. Kwa kifupi daktari Fernàndez alishindwa kutambua ni lini hii maiti ilikufa haswa.

Hatuwezi mlaumu daktari huyu sana kwa sababu moja nataka nikupe hapa.

Kiuhalisia nchi ya uhispania ni nchi ambayo dini ya Roman Catholic imekita mizizi sana. Hivyo kwa imani ya dini ya katoliki hairuhusiwi na ni mwiko kuifanyia maiti uchunguzi wa kitabibu kutaka kujua sababu za kifo cha mtu.. Ni kama tu kwenye dini ya kiislamu mtu akifa, ndani ya masaa 24 au 48 awe ameshazikwa😐😐😐🔎🔎🔎🔎🔎🔎📍📍🔨📍🔨📍.




Anyway tuendelee.......



Ilipofika majira ya usiku wa saa mbili huyu vice consul Francis Haselden alituma ujumbe Maalum kwa simu kwenda kwenye ubalozi uingereza huko Madrid na kuwasiliana na Naval attachê bwana Don Gomez-bearre . Ujumbe huu nanukuu:

"With reference to my phone message26 today body is identified as Major W. Martin R.M. identity card 148228 dated 2nd Feb. 1943 Cardiff. Naval judge has taken possession of all papers. Death due to drowning probably 8 to 10 days at sea. I am having funeral Sunday noon.”

Ndivyo ujumbe huu ulivyobainisha . Ukiisoma hii meseji Kuna mahali imetajawa Naval judge. Huyo jaji ni Pascual del pobil kitaaluma alikuwa ni mwanasheria.

Sasa nataka nikudokezee jambo hapa. Huu ujumbe uliotumwa kwenda kwa naval Attachè aliyeko Madrid uhispania ulitarajiwa kumfikia Gomez bearre , lakini nilikujulisha simu au jumbe za telegram zilizokuwa zinatoka na kuingia ndani ya ubalozi huu wa uingereza tayari kwa namna yoyote zilikuwa zinasikilizwa au kusomwa kwa Siri baada ya kuwa "intercepted" na baadhi ya watu fulani fulani ambao kiuhalisia walikuwa mapandikizi ya mtandao wa kijasusi wa Ujerumani uliokuwa ukisimamiwa na mtu mmoja ndani ya mji wa huelva ambaye nilikudokezea anaitwa "Adolf Clauss.
Huu mtandao wa siri wa kijasusi haikumaanisha ni wajerumani,la hasha kwa mfano gavana wa jimbo hili la huelva pamoja na msimamizi mkuu wa bandari hii ya huelva na maafisa kadhaa wa ngazi za juu wa kiutawala wa jimbo hili la huelva,wote hao walikuwa kwenye Payroll ya huyu Adolf Clauss. Watu hawa kiuhalisia walikuwa na acces ya Taarifa zozote zile ambazo zingekuwa interested kwa wajerumani.

Sasa ni wazi kwamba nyaraka hizi za Siri zilipaswa kuangukia mikononi mwa wajerumani, lakini kama isivyo bahati zikawa mikononi mwa mamlaka za Hispania.. shida iliyojitokeza ni kwa namna gani nyaraka hizo zitaangukia mikononi mwa wajerumani?.


Anyway....


Sasa siku ya Tarehe 2 mwezi mei 1943, ndio ilikuwa siku rasmi ya kumzika huyu Afisa William Martin 😎 kama ratiba ilivyopangwa na ubalozi wa uingereza huko Hispania. Kwa kifupi huyu bwana alikuwa anazikwa ndani ya nchi ya uhispania.

Viongozi na maafisa kadhaa wa ngazi mbalimbali walitarajiwa kuhudhuria mazishi ya huyu Mwanajeshi aliyekufa maji🤣😎.
Baadhi ya Maafisa na viongozi hawa waliohudhuria mazishi haya ni pamoja na naibu balozi wa uingereza nchini Hispania bwana Francis Haselden mwenyewe, Pascual del pobil pamoja na kamanda Elvira, msimamizi wa bandari ya mji wa Huelva.
Gavana wa jimbo hili la Huelva hakuhudhuria kutoa heshima zake za mwisho ila aliweza kutuma mwakilishi.

Kwa kifupi huyu major William Martin au Mincemeat alitarajiwa kuzikwa kwa taratibu na heshima zote za kijeshi kutokana na aina ya wahudhuriaji walipofika kutoa heshima zao za mwisho.

Cheti cha kifo cha major William Martin kilisainiwa rasmi na msimamizi wa mazishi bwana Candela kwa maelezo yafuatayo:

W. Martin, aged between 35 and 40, native of Cardiff (England) , officer of the British marines, found on the beach known as ‘La Bota’ at half past nine on April 30th, 1943. Death by drowning.”

Baada ya taratibu za kuuaga mwili huu Ikiwemo na risala fupi kusomwa , geneza la Major William Martin lilibebwa kwa ajili ya kwenda kupumzishwa kwenye eneo la Makaburi ya San Marco. Eneo hili huzikwa watu wenye kipato cha chini . Haselden aligharamia eneo hili la kuzikia kwa kukodi kwa pasetas 250.

Eneo hili la Makaburi ya San Marco hulipiwa kuzika mtu wako na kulipa gharama za kutunza kaburi (mfano kufyeka nyasi,n.k). Na endapo ukashindwa kulipa gharama za kila mwezi basi mwili hufukuliwa na kwenda kuzikwa sehemu nyingine . Hivyo Haselden alilipia gharama zote hizi kwa niaba ya ubalozi wa uingereza mjini Madrid.

Sasa ilipofika saa sita na nusu mchana , geneza la Major William Martin lilishushwa kaburini huku Haselden akijua fika kwenye akili yake anayezikwa hakuwa afisa wa jeshi maji la uingereza na wala jina la William Martin halikuwa jina lake halisi⚠️⚠️⚠️📍📍.

Kwa kifupi ni kwamba major William Martin au Glandyr Michael raia maskini kabisa mwenye asili ya Wales alizikwa kama raia wa uingereza na kuzikwa kwenye nchi ya ugenini ya uhispania kama afisa wa jeshi la maji mwenye cheo cha umeja. 😑😑😑😑🥺🥺🥺.

Kwenye kaburi la huyu major William Martin au Glandyr Michael kuliandikwa maandishi ya kilatini yaliyosomeka kama ifuatavyo "DULCE ET DECORUM EST PRO PATRIA MORI" . Msemo huu ni kutoka kwenye kitabu cha mashairi kinachoitwa Odes kutoka kwa mwandishi wa kiitaliano aliyeitwa HORACE wa Karne ya 23B.C.
Tafsiri ya msemo huu usio rasmi unamaanisha "Ni Raha sana na inafaa kabisa kufa kwa ajili ya nchi yako"

Baada ya taratibu za kuushusha kaburini mwili wa marehemu , mzikaji akiendelea kufukia kaburi nao maafisa waliohudhuria akiwemo Haselden walipanda magari yao na kuondoka.

Lakini katika shughuli hii ya kumzika huyu marehemu,yupo mtu MMOJA alikuwa akifuatilia shughuli nzima kwa ukaribu na umakini wa hali ya juu sana . Hakuwa mwingine bali ni Adolf Clauss ambaye hapo awali nilikujulisha awali alikuwa ni afisa wa kijasusi wa Ujerumani ambaye alikuwa akifanya kazi ya kukusanya Taarifa zozote zile za kijasusi kwa niaba ya jeshi la Nazi la ujerumani kupitia kitengo cha kijasusi cha jeshi la Nazi kilichojulikana kama ABHWEIR.
Huyu bwana alikuwa anafuatilia kila kitu kuhusiana na shughuli hii nzima ya mazishi ya huyu Mwanajeshi aliyekufa maji wa uingereza.

Kwa kifupi huyu bwana alikuwa anajaribu kwa kila njia namna ya kupata briefcase hii iliyokuwa na barua zile za Siri alizokuwa nazo huyu mtu aliyezikwa.........

Zipo na na nani na atazipataje. Lilikuwa ni swali ambalo Adolf Clauss pengine alijiuliza.
.....
 
Back
Top Bottom