SEHEMU YA 10
Huyu Adolf Clauss ambaye nilikujuza alikuwa ni afisa wa kijasusi wa kijerumani chini ya kitengo maalum cha kijasusi cha jeshi la Nazi ABHWEIR, alikuwa akipambana kwa kila namna kupata nyaraka hizo zilizokuwa zimebebwa na huyu afisa Major William Martin lakini juhudi zake ziliambulia patupu. Maafisa wa serikali ya uhispania ambao baadhi yao walikuwa kwenye Payroll ya huyu mtu waligoma kutoa ushirikiano wa kumkabidhi kujua zinahusiana na nini hizi nyaraka kuepuka mgogoro wa kidiplomasia kati ya uingereza na Hispania.
Sasa aliamua kujaribu njia nyingine ya kuweza kupata hizi nyaraka. Alimtafuta afisa mwingine wa hapo Hispania aliye kwenye payroll za wajerumani ili aweze kupata access ya hizo nyaraka.
Afisa huyu alikuwa ni luteni kanali wa kikosi Maalum cha polisi kwenye mji wa huelva aliyeitwa Santiago Garrigós afanye juu chini aweze kumshawishi Pascual del pobil amuonyeshe hizo nyaraka alizokuwa amebeba major William Martin. Huyu Garrigós alitumia mbinu zote alizozijua na kupata baadhi ya info kuhusiana na brifecase na nyaraka zake japo hakuweza kusoma.
Baada ya kupata baadhi ya Taarifa kuhusiana na nyaraka hizo , alimtonya huyu Clauss kwamba brifecase hiyo ilikuwa na barua mbili maalum za maelekezo na mipango ,picha zaidi ya 23 pamoja na
Bahasha zenye anwani ya general Eisenhower, Cunningham pamoja na general Alexander ambao hawa wote walikuwa makamanda wa vikosi vya allied vilivyokuwa huko Afrika kaskazini. Clauss bado hakuridhika na Taarifa hizi kutoka kwa Garrigós japo zilimpa mwanga fulani kuhusiana na namna gani hizi nyaraka zilikuwa na umuhimu mkubwa.
Clauss akaamua kutafuta njia nyingine tena. Mara hii aliamua kutumia ushawishi wa baba yake ambaye alikuwa balozi wa ujerumani nchini uhispania aliyeitwa Ludwig Clauss aweze kumtumia gavana wa kiraia wa jimbo la huelva bwana Joaquìn Miranda Gonzalez aweze kutumia ushawishi wake kama gavana ili nyaraka hizo apate kuziona na vilevile kupigwa picha kwa Siri kisha zitumwe hadi kwa wajerumani. 🤔 Lakini bado ilishindikana. ......
Sasa tukirudi hadi huko London, uingereza Ewen Montagu na Charles Cholmondeley walikuwa wanajua tayari nyaraka hizi alizokuwa nazo major William Martin zimefika sehemu iliyokusudiwa salama ila wasiwasi waliokuwa nao ni kwamba nyaraka hizo ziliangukia kwenye mikono ya Maafisa wa Hispania ambao kwa jicho la kijasusi ni kama walikuwa wanachewelesha "Taarifa nyeti" zilizokuwa ndani ya barua hizo kufika kwenye mikono ya wajerumani wenyewe.
Sasa ikaamuliwa waweze kuingia tena Kazini kuhakikisha nyaraka hizo zinafika kwenye mikono ya wajerumani. Kitengo cha ujasusi wa jeshi la maji la uingereza waliamua kuchukua jukumu hili kupitia Alan Hillgarth ambaye ni mjumbe maalum kwenye ubalozi wa uingereza mjini Madrid wa jeshi la maji la uingereza yaani Naval Attachè.
Huyu bwana Hillgarth alituma ujumbe Maalum kwa simu ya ubalozi hadi uingereza kwenda makao makuu ya Admirality kitengo cha Naval Intelligence kuhusiana na mazishi ya major William Martin pamoja na wageni waliohudhuria na taratibu zingine hadi kukamilika.
Simu hii aliyopiga (cable) kutoa ujumbe kwenda uingereza alitumia simu rasmi ya ubalozi akijua fika simu hii itasikilizwa na Wajerumani .
Nao makao makuu walirudisha ujumbe kwa njia hii hi ya simu wenye namba 04132 kama feedback kwa Hillgarth ukitamka afanye juu chini kupata briefcase pamoja na nyaraka zake haraka iwezekanavyo kwa sababu ni za Siri na za umuhimu mkubwa🔨🔨📍.
Ujumbe huu aliotumiwa Hillgarth ulitarajiwa kuwa intercepted na majasusi wajerumani. Ujumbe huu ulisomeka kama ifuatavyo :
"
Some of papers Major Martin had in his possession are of Great importance and secrecy. Make formal demand for all papers and notify me by my personal signal immediately of addressees of any official letters recovered.
Such letters should be returned addressed to commodore Lashbrooke , personal by fastest route and should not repetition not be opened tampered with in any way. If no official letters are recovered make searching but discreet inquires at Huelva and Madrid where they were washed ashore and if so what happened to them"
Hii ina maana kama wajerumani wangedukua ujumbe huu wa simu nao wangeongeza bidii ya kupata hizi nyaraka haraka iwezekanavyo kabla hazijarudi mikononi mwa Uingereza.
Baada ya ujumbe huu kwenda kwa Hillgarth, Ewen Montagu alimtumia ujumbe mwingine tofauti na huu kwa njia salama ya kijasusi ya Cipher uliosomeka kama ifuatavyo
: "Carry out instructions in my Naval Signal as this is necessary cover but lack of success is desirable." Hii ilikuwa na maana ujumbe wa kwanza aliotumiwa Hillgarth kwa njia ya simu ya ubalozi ilikuwa ni cover na ulitarajiwa kusikilizwa na Wajerumani kwa vyovyote vile.
Ujumbe huu alioupokea Hillgarth aliweza kumjulisha Naibu balozi wa uingereza Francis Haselden aweze kuzitafuatilia na kuzitafuta hizi nyaraka
(kiuhalisia Haselden alikuwa anajua nyaraka zipo wapi na nani ,lakini hii ilikuwa ni kuwazuga wajerumani waweze kujua umuhimu wa hizo nyaraka).
Sasa kabla hatujaenda mbali nataka nikujuze jambo moja kuhusiana na hii taaluma ya ujasusi / unjagu au ushushu.
Katika Dunia ya ujasusi UMBEA ni kama sarafu. Na kawaida umbea una tabia ya kusambaa kama utando wa buibui kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Na kawaida umbea una tabia ya kubadilika kadiri unavyozidi kusambaa kutoka sehemu moja au kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine.
Hata hapa Jeiefu usione tunafungua nyuzi za umbea umbea kuhusiana na serikali au viongozi wa serikalini ,huku tunachangia kwa mbwembwe. Kuna watu humu na ID zao umbea wowote wa humu kazi yao ni kuuchukua kwa uzito wake na kupelekwa huko
UTIISINI kwa ajili ya kuchakatwa haijalishi umbea huo una ukweli au la... Anyway acha tusiongee sana lakini kaa ukijua na kufahamu kwamba
"In intelligence, Gossip is a currency where spies are traded with it , government officials saturated with it and ordinary people indulged with it" 😎😎😎
Hivyo huyu Hillgarth aliamua kutumia sarafu hii ya umbea . Kwenye Maeneo ya migahawa na mitaani alipokuwa akipiga stori na baadhi ya watu alianza kutoa fununu za umbea umbea kwamba Waingereza Kuna nyaraka zimepotea ndani ya mji wa huelva na wanazitafuta.📍📍🔨 .
Alifanya hivi makusudi kabisa akijua kwamba umbea huu alioropoka utawafikia wajerumani. Hii ni kwa sababu hata huko mtaani majasusi wajerumani (yaani Adolf Clauss) walikuwa wameweka wambea na walikuwa kwenye Payroll kwa ajili ya kukusanya Taarifa zozote zile ambazo zingekuwa interested na majasusi wa ujerumani waliokuwa wametapakaa uhispania yote Hususani kwenye mji huu wa huelva haijalishi ni za umbea au la.
Huyu Hillgarth pia alijaribu njia nyingine ambayo kwa vyovyote vile alijua ingetoa "Alert" au red flag kwa wajerumani.
Huyu bwana Hillgarth aliamua kutaka kuwasiliana admiral wa jeshi la maji la uhispania aliyeitwa Moreno ambaye pia alikuwa ni waziri aliyesimamia shughuli za majeshi ya majini. Huyu bwana Moreno licha ya kuwa ni rafiki wa Hillgarth, pia alikuwa ni pro-german.
Lengo la Hillgarth kuwasiliana na huyu bwana ilikuwa ni kumtaka amsaidie kupata hizo nyaraka.
Kwa upande wa Adolf Clauss, Taarifa alizokuwa akuzipata na kuzituma kwa wakubwa zake huko Ujerumani, kuhusiana na hizi nyaraka na Anwani za wakuu wa kijeshi zilizokuwa juu ya bahasha kulimuongezea presha maradufu kuhakikisha anazioata kabla hazijaingia mikononi mwa Uingereza.
Nataka uelewe hapa jambo moja. Kiuhalisia sio kwamba Waingereza walikuwa wanataka hizi nyaraka zirudi mikononi mwao bali huu ulikuwa ni mchezo uliopangwa kwa ustadi wa Hali ya juu wa kuwafanya Wajerumani wapate kiwewe na mshawasha wa kuzipata hizo nyaraka na ujumbe wa hizo barua .
Walichokuwa wanakifanya uingereza hapa ni kuongeza grease kwenye tairi za Mjerumani zizunguke kwa haraka ili kutaka kuzifikia hizi nyaraka 🔨📍📍. Nafikiri unapata picha kwa hiki nachokielezea hapa.
Sasa simu zikawa hazikauki kati ya ubalozi wa uingereza ndani ya uhispania na makao makuu nchini uingereza. Na simu zote hizi kwa namna moja au nyingine zilikuwa zikisikilizwa na Wajerumani kwa Siri.
Simu hizi kiuhalisia zilikuwa zikipigwa kwa ajili ya kuwashinikiza maafisa wa operation hii waliopo HISPANIA kuzi secure hizo nyaraka.📍🔨📍
Sasa huyu Adolf Clauss alifanya juu chini kupata content ya hizi nyaraka lakini bado hakufua dafu na hata mawakala wake aliowaweka kwenye kila idara ya jeshi la maji la uhispania bado hawakuweza kumsaidia kupata Taarifa rasmi ya hizo nyaraka.
Sasa ikatolewa amri kutoka kwa admiral Moreno
IKASEMEKANA kwamba brifecase hii ya Major William Martin pamoja na nyaraka zake zipelekwe makao makuu ya Admirality huko Madrid pasipo kufunguliwa kwa namna yoyote ile.
Hii ilimuongezea uzito Adolf Clauss namna ya kuzi secure hizi nyaraka. Ameshindwa huku huelva, je zikienda huko Madrid makao makuu ataweza?
Ugumu wa kuzipata hizo nyaraka ni kwamba baada ya kufika Madrid Sasa IKASEMEKANA zipo chini ya uangalizi wa jeshi la Navy la uhispania hivyo ilihitajika pia huyu Adolf Clauss aweze kumtumia pandikizi lake aliyekwepo ndani ya jeshi hilo kuweza kupata hizo infosandani ya jeshi kuhusiana na nyaraka hizo .
Lakini baadaye huyu pandikizi ndani ya jeshi kufanya Enquires kuhusiana na nyaraka hizo bado majibu yalikuwa Negative kwa maana ya kwamba nyaraka hizo jazijafika huko.
Adolf Clauss hakukata tamaa , akajaribu kutumia assets zake yaani mapandikizi wake kwenye idara ya usalama wa nchi ya Hispania ya Dirección General de Seguridad yaani DGS lakini napo hakukuwa na msaada wa kuzipata hizo nyaraka .
Kwa kifupi ni kwamba Adolf Clauss alikuwa anajua mtu wa mwisho kuwa na hiii briefcase yenye hizi nyaraka alikuwa ni Admiral Moreno ambaye awali nilikujulisha ni waziri aliyekuwa akisimamia idara ya jeshi kitengo cha navy.
Sasa katika dakika za tisini Adolf Clauss aliamua kumtumia pandikizi wake wa muhimu na wa mwisho ndani ya jeshi la anga aliyejulikana kama afisa Groizar ambaye alikuwa na umuhimu kwa wajerumani katika kumtumia kutokana na huyu bwana kuwa na connection na kila mkubwa ndani ya jeshi la Hispania... Huyu bwana atleast alionyesha matumaini ya nyaraka hizi feki kuwafikia wajerumani ndani ya siku tisa Baadaye.📍📍🔨🔨🔨✍️
Kitambulisho chenye picha ya cha Adolf Clauss. Huyu jamaa hakukata tamaa katika kuzipata hizi nyaraka feki za siri