Kisa cha Mwitore na bi mdogo kimenikumbusha mkasa wa swahiba wangu

Kisa cha Mwitore na bi mdogo kimenikumbusha mkasa wa swahiba wangu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Swaiba alialikwa kwenye kikaocha harusi, amefika kule alikutana na binti mzuri sana, kinda bado changa kabisa. Alikuja mjini kwa mwaliko wa dada ambae wanatoka kijiji kimoja, ilkua mara yake ya kwanza kufika Dar huyu dada alimpeleka binti kwenye kikao kile kama sehemu ya utalii wake mjini. We may call her Joy.

Joy alimaliza kidato cha sita lakini hakupata chuo, hivyo katika muda wa kutafuta fursa ndiyo aliamua kulitembelea jiiji

Swaiba alimuelewa sana Joy, walibadilishana namba za simu. Baada way wiki mbili ugeni wa Joy ulifikia ukomo, swaiba alimbembeleza asiondoke. Alimchukulia chumba Guest House.

Swaiba ana mke na watoto wawili. Alianza kupitia Guest kumuona Joy akitoka kazini na alikaa nae mpaka saa mbili usiku ndiyo alikwenda kwake. Asubuhi alimpitia Joy kabla ya kwenda kazini. Baada ya wiki mbili pale Guest House, swaiba aliamua kumtafutia Joy chumba na sebule. Aliweka furniture na maisha yakaendelea.

Swaiba alishajiwekea kanuni ya kutokulala nje. Alimpa Joy mahitaji yote, na akitoka nae ni lazima arudi nyumbani. Akipata safari za kikazi anakwenda na Joy. Anasema hajawahi kuwa na raha katika maisha yake kama kipindi yuko na Joy. Alikua mcheshi, mwenye akili na hekima.

Siku moja akiwa nyumbani kwake, alipigiwa simu na jirani wa Joy kuwa Joy amepata maradhi ya ghafla. Aliwaambia wampeleke hospitali, yeye alishindwa kutoka kwake usiku ule. Alipanga kwenda hospitali alfajiri. Asubuhi na mapema anafika hospitali anafahamishwa kuwa Joy alifariki usiku ule.

Anasema kipindi kigumu alichopitia ni kuomboleza msiba wa siri. Mke wake hakufahamu kuwa amefiwa na mtu aliyekua wa karibu sana na yeye. Nilipiga picha jinsi wanaume wanavyoweza kuishi maisha ya aina mbili kwa wakati mmoja.

Swaiba alishiriki na yule dada aliyemleta Joy mjini kusafirisha mwili wa marehemu mpaka kijijini kwao. Huu ulikua mwisho wa maisha way Joy.
 
Daaah, ila ndoa ya mke mmoja inapaswa kutizamwa tena
Hili jambo lilishanishinda tangu zamani, siwezi kukaa na mke mmoja.

Watu wanapata hii mikasa kwa malipo ya machumo ya mikono yao, kama imani yako haikuruhusu kuwa na wake wengi jikaze, kwani jimai siyo chakuli, ila kama sisi huku tunaoa mpaka wanne na tutakamilisha tu hii idadi.
 
Back
Top Bottom