Kisa cha Mwitore na bi mdogo kimenikumbusha mkasa wa swahiba wangu

Kisa cha Mwitore na bi mdogo kimenikumbusha mkasa wa swahiba wangu

Swaiba alialikwa kwenye kikaocha harusi, amefika kule alikutana na binti mzuri sana, kinda bado changa kabisa. Alikuja mjini kwa mwaliko wa dada ambae wanatoka kijiji kimoja, ilkua mara yake ya kwanza kufika Dar huyu dada alimpeleka binti kwenye kikao kile kama sehemu ya utalii wake mjini. We may call her Joy.

Joy alimaliza kidato cha sita lakini hakupata chuo, hivyo katika muda wa kutafuta fursa ndiyo aliamua kulitembelea jiiji

Swaiba alimuelewa sana Joy, walibadilishana namba za simu. Baada way wiki mbili ugeni wa Joy ulifikia ukomo, swaiba alimbembeleza asiondoke. Alimchukulia chumba Guest House.

Swaiba ana mke na watoto wawili. Alianza kupitia Guest kumuona Joy akitoka kazini na alikaa nae mpaka saa mbili usiku ndiyo alikwenda kwake. Asubuhi alimpitia Joy kabla ya kwenda kazini. Baada ya wiki mbili pale Guest House, swaiba aliamua kumtafutia Joy chumba na sebule. Aliweka furniture na maisha yakaendelea.

Swaiba alishajiwekea kanuni ya kutokulala nje. Alimpa Joy mahitaji yote, na akitoka nae ni lazima arudi nyumbani. Akipata safari za kikazi anakwenda na Joy. Anasema hajawahi kuwa na raha katika maisha yake kama kipindi yuko na Joy. Alikua mcheshi, mwenye akili na hekima.

Siku moja akiwa nyumbani kwake, alipigiwa simu na jirani wa Joy kuwa Joy amepata maradhi ya ghafla. Aliwaambia wampeleke hospitali, yeye alishindwa kutoka kwake usiku ule. Alipanga kwenda hospitali alfajiri. Asubuhi na mapema anafika hospitali anafahamishwa kuwa Joy alifariki usiku ule.

Anasema kipindi kigumu alichopitia ni kuomboleza msiba wa siri. Mke wake hakufahamu kuwa amefiwa na mtu aliyekua wa karibu sana na yeye. Nilipiga picha jinsi wanaume wanavyoweza kuishi maisha ya aina mbili kwa wakati mmoja.

Swaiba alishiriki na yule dada aliyemleta Joy mjini kusafirisha mwili wa marehemu mpaka kijijini kwao. Huu ulikua mwisho wa maisha way Joy.
Dah ila wanaume tunakazi sana.
 
Inawezekana kabisa,
Daaah hatari sana.......kumbe unaweza kuwa ndoan afu usiwe na furaha
unaeza kuwa upo na mtu ambaye yupo yupo tu! Sio supportive kihisia hapo ndio shida inapoanza wala hakuchangamshi. Badala yake anakuwa source ya kero zaidi ya kukupa amani na furaha.
 
Mume anarudi nyumbani kavurugwa unajua ni mambo ya kazi, unahangaika kumfariji kumbe kavurugwa na mchepuko[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Uzuri Joy alikuwa comforter sio kivuruge 😂😂😂 yani michepuko wana package flani amazing! Anakuwa romantic katika namna flani amazing and very supportive emotionally. Raha anazokupa unaweza mjengea hata kighorofa kimoja fasta.

Mke uliemuoa kwa mamilioni ndio anakuwa source ya kero sijui kwanini yani, hawanaga emotional support esp.mkishaanza kulala na kuamka pamoja, wana ile hali ya kuchukulia poa ile bond mliyo nayo as they stop making you feel special...mambo huharibikia hapo sasa.
 
Wengi wenu hamna sababu ya msingi ya kuoa wake wengi isipokuwa tamaa tu ya ngono. Na majority kwenye suala la kuoa wake wengi ndiyo karibu kila mtu anajikuta anataka atimize dini; ila kwenye masuala mengineyo wala hamkumbuki kama dini imewaamuru.
C.c Jurjani
Hahahah shemela bana, kuoa wake wengi kuna faida yake bana japo sina hulka hio ila nachokiona ambacho ndio sababu ya michepuko huwa ni hali ya wake kuleta mazoea ya kipumbavu. Mke anakuwa unsupportive emotionally na kujifanyia vitu ilimradi kwa kuhisi anakumiliki ndio mnafikia stage mume ule uspesho unakuwa hamna tena. Mazoea yanaua emotional sparks zinazokoleza hisia za mapenzi baina yenu.

Watu wanao opt michepuko sio kwamba wote ni umalaya ila raha za mapenzi zinakuwa overshadowed na kero zaidi badala ya emotional support and comfort.
 
Ninyi mnaosema mke mmoja hatoshi hamjapenda tu! Na mke ni bora uishi jela kuliko kuishi na mume asiyekupenda!
Hahahahah mke mmoja mtamu akiwa hajaanza kukupuuza. Hata nyie mngekuwa ME lazma mngeona kero ya kupuuzwa. Unamuhitaji mke ili awe comforter awe rafiki yako ila after sometime anakuwa ha serve that purpose unafanyaje?

What do we do to broken glass? We replace them with new ones!
 
Wengi wenu hamna sababu ya msingi ya kuoa wake wengi isipokuwa tamaa tu ya ngono. Na majority kwenye suala la kuoa wake wengi ndiyo karibu kila mtu anajikuta anataka atimize dini; ila kwenye masuala mengineyo wala hamkumbuki kama dini imewaamuru.
C.c Jurjani
Sahihi binamu na sio kazi rahisi kama tunavyoandika kuoa wake wengi na wameusiwa oeni kuanzia wawili mpk wanne lakini muwe waadilifu mkishindwa uadilifu basi oa mmoja.Na wanaume wenye mathna (wake wawili)wana mtihani sana kwa Mungu maana uadilifu wengi unawashinda wanaegemea upande mmoja tu na ndo chanzo cha kurogwa na kurogana hikoo.

Hawa wa kizazi hiki jamani hawaoi kwa uadilifu bali kwa hulka na kukomoana na bimkubwa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi ningelia aisee nigedakwa tu ila ningesingizia msiba hata wa ndugu yangu aidha mzazi au ndugu yangu wa damu, bibi mlezi au babu ningezuga kumkumbuka sana mke angenibembeleza kama ni romantic

Umenikumbusha kisa cha jamaa yangu mmoja wakati tuko chuo. Jamaa siku hiyo kaenda kwa demu wake kamkuta demu analia macho yamevimba.. jamaa ndio kuanza kumbembeleza pale akamuuliza kulikoni? Demu kampa jamaa bonge la stori ya kuhuzunisha mpaka jamaa nae akaanza kulia..! Wamelia pale weee... Siku ya siku jamaa anakuja kugundua kumbe demu alikua analia kupigwa chini na mshkaji mwingine ambae nae ni mwanafunzi hapo hapo! Aisee jamaa yangu alikua mbogo balaa na ukizingatia alikua anajidai mgumu flani.. sisi saa hiyo hatuna mbavu 😆😆
 
Hahahahah hizi zipo mzee, unaumia kwa maumivu ya demu mwengine kukulamba kibuti! Nahisi ishawahi ntokea hii 😂😂😂
 
Hahahahah mke mmoja mtamu akiwa hajaanza kukupuuza. Hata nyie mngekuwa ME lazma mngeona kero ya kupuuzwa. Unamuhitaji mke ili awe comforter awe rafiki yako ila after sometime anakuwa ha serve that purpose unafanyaje?

What do we do to broken glass? We replace them with new ones!

Ila bana Extro tuseme tu ukweli.. sisi wanaume nadhani tumelaaniwa linapokuja swala la michepuko. Hata uwe na mwanamke mzuri kiasi gani, anakujali, anakupenda, yupo supportive lakini bado ukiona katoto kazuri nje huko unaanza kukamezea mimate! Na mbaya ni kwamba at that moment unapokutana na dem mzuri, hua unasahau kabisa kama una mke.... utakuja kukumbuka baadae huko mmeshamaliza mambo yenu ndio unaanza kujuta ila huachi!
 
Ni kweli mkuu ila mie huwa naishia kuwatamani tu sijui kwanini, kuchukua hatua za kuanza kumtongoza mwanamke mwengine ikiwa nina mke anayenihudumia bila usumbufu huwa inakuaga ishu.

Labda demu mwenyewe anishobokee kiasi kwamba anipe greenlight tu 😂 ila sipendagi ku waste energy kumfuatilia mwanamke.
 
Uzuri kwavile mademu wa siku hizi hua hawana haja ya kutongozwa kwahiyo najua na wewe utakua unawatafuna tu kama sisi. 😀
 
Back
Top Bottom