Mkuu kubali ukatae ni kwasababu tu kuna sheria za nchi la sivyo ungeshuhudia mambo ya ajabu sana. Angalia mfano jihadists mafundisho yao ambayo wanafundisha vijana.
Reference ya karibu kabisa angalia lile tukio la West Gate Nairobi. Wale jamaa walikuwa wakikukuta wanakuambia recite shahadah (kwamba unamkiri Allah na unamtambua Mohamed kuwa ni mtume wa Allah) na kama hujui ulikuwa unakula risasi.
Sasa imagine kungekuwa hakuna hizo sheria za nchi zinazozuia mauaji unadhani watu ambao hawaamini Islam wangepona?
Unaona unapofeli hapo?! Kwahiyo Al Shabaab kusema waliyosema kwako ndo reference ya kufanya conclusion?!
Hebu twende taratibu! Kwanza kabisa neno Jihad ambako umewatoa hao uliowaita Jihadists, ni neno ambalo limekuwa corrupted sana kiasi kwamba wengi mnaamini Jihad is nothing but war! Lakini hata tukichukua hiyo tafsiri yenu mnayoipenda sana, hebu tuangalie aya zinazotumiwa sana na hao mnaowaita Jihadists!!
QURAN 2:190 inasema:-
Na piganeni katika njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaowapigeni, wala msiruke mipaka. Kwa yakini Mwenyezi Mungu hawapendi warukao mipaka.
Na 191 Inasema:-
Na wauweni po pote mwakutapo, na kuwatoa po pote walipokutoweni; kwani mateso ni mabaya zaidi kuliko kuua. Wala msipigane nao karibu na Msikiti Mtakatifu mpaka wawapigeni ndani yake. Na wakiwapigeni basi nanyi pia wapigeni: kama hivyo ndiyo malipo ya makafiri.
Na 192 inasema:-
Lakini kama wakiacha, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mrehemevu.
Na mwisho inasema:-
Na wapigeni mpaka pasiwe mateso, na dini iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu; na kama wakiacha, basi usiweko uadui ila kwa wadhalimu.
Kwanza kabisa, kuzielewa hizo aya ni lazima uwe umesoma au uwe na mwanga wa theology tofauti na wengi wenu mnavyoingia tu Google na kuokoteza aya halafu eti ndo mnajiona mnaijua Quran...
...Yaani Quran ile ile ambayo watu wanatumia miaka na miaka kuisoma, watu mnaielewa ndani ya dakika 1... you guys are geniuses!
Lakini pamoja na umuhimu wa teolojia ili uweze kuelewa msingi wa aya za Quran na hata zile za Bible, lakini hebu zisome kwa makini hizo sehemu zilizo-highlight!
Piganeni na wale WANAOKUPIGENI, na wala MSIVUKE MIPAKA!
Hivi hapo unapata picha gani? Ni kwamba Waislamu wameambiwa Wabebe silaha wakaue watu wasio wa imani yao au wameambiwa WAKIWAANZA, FIGHT BACK?!
Hivi kwenye hayo mataifa ya Kikristo, WAKIANZA KUPIGWA, ina maana hawapigani? Kama hawa-fight back, unaweza ku-declare hapa kwamba Crusade ilikuwa UNHOLY War?
Na hapa wala sitaki kuwa mnafiki... Ukiacha wale Waarabu wala neema kule Gulf Countries, Waislam duniani kote akili zetu tunazijua wenyewe!! Huwa hawataki ujinga!!
Hata ukikaa chini ukapiag mahesabu tawala zilizowahi kufurumishwa madarakani just kwa watu kuingia barabarani tu... utakuta nchi zenye Waislamu wengi ndo zinaongoza!! Hata kule West Africa ambako ukizingua tu watu wanakupandia na mashine huko huko Ikulu, nyingi ni zile zenye waislamu wengi!
Hata hawa ma-CCM yanayotusumbua ni kwa sababu yanajua kuna akina Chaliifrancisco wengi ambao Mzungu ili kuhakikisha anakula neema za Afrika bila wenge, akawaambia Bwana Kasema "Mtu akikutandika kofi mkono wa kushoto, mgeuzie na la kulia..." (Don't mind, hii ni furahisha genge tu)
But look CCM Zanzibar wanavyoikumbatia bara... wale wanajua kabisa CCM Bara wakisema "sasa kila mmoja ale kwa urefu wa kamba yake katika kutafuta utawala", huo utakuwa ndio mwisho wa CCM ZNZ!
Mtasema sana... hamjasoma, vibarakashia, sijui kunywa kahawa vibarazani, lakini UJINGA KWETU, NOI!
Tuache hayo "mazungumzo baada ya habari"
Sasa ni kwanini nilisema kuzielewa hizo aya ni lazima uwe na mwanga wa teolojia!
Unlike Moses and Jesus, Muhamad aliitangaza imani yake kwa taabu kweli kweli! Yeye na wafuasi wake ilikuwa mara kwa mara wanashambuliwa na hata kuuawa! Wakati mwingine mateso waliyokuwa wanayapata yalikuwa yanatoka kwa watu wa ukoo wake mwenyewe!
Mambo yalipozidi kuwa magumu, ikabidi Muhammad na Wafuasi wake watoroke Makkha usiku usiku na kukimbilia Madina!! Lakini wakati wote huo, ilikuwa wakishambuliwa, jamaa hawajibu mapigo na wakabaki kumlilia Mwenyezi Mungu awanusuru na madhira waliyokuwa wanakutana nayo!
Kutokana na hayo, ndipo zikashuka hizo aya kuwaambia "Acheni uf'ala nyie , wakiwapiga, fight back! Wakiwaua, nanyi ueni! Kama waliwatoa sehemu zenu, fight hard kukomboa hizo sehemu"
Sasa je, hao Magaidi ambao mnapenda sana kuwatumia kama reference, ndivyo wanavyofanya?! Kule Msumbiji walikoenda kuua watu, unaamini kabisa actions zao zinaendana na hizo aya?! Wale wauaji wanaojiita Boko Haram, hivi kabla hawajaanza ule unyama wao ulishawahi kusikia Waislamu Nigeria wamepigwa na Wakristo hatimae Boko Haram wakapata uhalali wa ku-fight back
Na kabla hujaanza kulalamika kuhusu neno kafiri lililotumika hapo, nikujuze tu kwamba Kafiri sio TUSI na wala sio NENO LA KASHFA kama ambavyo mnadhanii! KAFIRI NI MTU ASIYEAMINI UNACHOKIAMINI! Hata Mwislamu ni KAFIRI mbele ya jicho la Mkristo! Hata kwenye Bible hilo neno limetumika sana!!!
Lakini hata ukija kwenye kamusi,
Hiyo ni kamusi ya Kizungu ambayo kuna 90% imeandikwa na Christians! Wao wanakuambia:-
Kwa Mkristo: Kafiri ni yule asiyeamini, especially MUSLIM, wakati kwa Waislam, Kafiri asiyeamini katika Uislamu bila kujali kama ni Mkristo, Pagan, Myahudi or anyone!!
Merriam Dictionary nao:-
Hilo nimeamua kuweka wazi mapema kwa sababu wangekuja wengine hapa wakaanza kutoa mapovu kwa sababu tu aya ya 191 imetaja Makafiri! Tena nadhani ukifahamu maana ya Kafiri basi Mkristo ataona fahari kuitwa Kafiri na Mwislamu! Kwanini asione fahari kuambiwa anaamini Yesu alikufa na kufufuka? Kwanini asione fahari kuaambiwa haamani Quran?!