Kisa cha Shariff Abdallah Attas na mwalimu Julius Nyerere ofisi ya TANU baada ya uhuru

Niah,
Kitabu kipo Tanzania Publishing House Samora Avenue,
Elite Bookshop Mbezi Samaki, Soma Bookshop Mikocheni,
Ibn Hazm Bookshop Msikiti wa Mtoro na Manyema na
Rubawa Investment Shariff Shamba, Ilala.
Mzee nashukuru saana nitajaribu kuomba mtu aninunulie. Wakati wa uhuru wengine tulikuwa watoto wadogo hivyo tulichokisoma shuleni ndo tuliamini sababu unajua hali ilivyokuwa miaka ya 60s mpaka 80s.
 
Shukrani Mzee wangu. Allah akujaze hekma na subra kubwa.
 
Bado nasubiria kile kisa cha yule bwana somo yangu.
 
Kuna watu hawajaumbwa na Haya,tabia mbaya za namna hiyo ndio watu wengine wanaanzisha mada eti ni "kuwazidi ujanja" hao waliompokea na kumkirimu
Ujue Babu hakuwazidi ujanja Waswahili peke yao, hata Mangi Mareale alipigwa kekundu na akapotezwa kwenye siasa...
 
Bado nasubiria kile kisa cha yule bwana somo yangu.
Slim5,
Vuta subira.

Unajua ''art,'' ya uandishi wa jambo unatafuta tukio muafaka
kisha unatumbukiza chuma.

Somo yako alikuwa ''man about town,'' mtoto wa mjini khasa,
mjanja maneno mengi, ''sharp,'' ''philosopher'' ''all rolled into one.''

In Shaallah nitakupa michapo yake.

Kulikuwa na guitarist mkali sana anaitwa Slim Pezin akipiga na
Manu Dibango.

Nyie akina Slim matata sana nyie.
 
I salute you. Wewe ni mwanahistoria wa kweli. Naomba utengeneze documentary ya historia ya kweli ya Tanganyika.

Muslims have played a major role in the struggle for independence in Tanganyika.
 
I salute you. Wewe ni mwanahistoria wa kweli. Naomba utengeneze documentary ya historia ya kweli ya Tanganyika.

Muslims have played a major role in the struggle for independence in Tanganyika.
Wigo,
In Shaallah...
 
Mzee Mohamed Said.

Kwanza shikamoo mzee wangu.

Mimi ni mpenzi mkubwa wa historia hasa ya nchi yetu. Swali linakuja ni wapi naweza kusoma au kupata hizi historia maana mfumo uliopo historia hazitunzwi kabisa.

Asante.
 
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
Ngoja nifanye subira Mzee wangu.
 
Mara baada ya kutoka chuo, kuna pahala nilijiweka nikiwa kama Mwl pale. Katika sisi alikuwepo Mzee mmoja ambae tulifundisha nae. Siku 1 kulikuwa na ufunguzi rasmi wa ofisi ile na mgeni alikuwa Mh wa awamu ya 4.

Basi kama ada, wafanyakazi tukafanya "line up" ili kusalimiana na Mgeni. Mimi nilisimama jirani na yule Mzee. Mgeni wetu akafika na kuanza kutoa mkono wa salamu huku tukijitambulisha.

Mara alipofika kwa yule Mzee, Mh hakumuachia mkono mapema, aliendelea kumshikilia mkono huku wakisemezana mambo ya hapa na pale.

Mh alionyesha kushtuka kumuona yule Mzee pale. Na akamuuliza: KUMBE UPO HAPA SIKU HIZI? Na maswali mengine.
Binafsi kiroho kilikuwa kikinidunda kwa kucheleweshwa kushikana mkono na Mh, huku Mzee akitumia muda mwingi kusalimiana nae. Yule Mzee alikuwa ni mwenye furaha siku nzima. Kuna raha yake ukikumbukwa na mtu mliefahamiana kitambo!
 
Kuna watu hawajaumbwa na Haya,tabia mbaya za namna hiyo ndio watu wengine wanaanzisha mada eti ni "kuwazidi ujanja" hao waliompokea na kumkirimu
Mkuu Mumba Daly heshima kwako!

Ni mimi ndio nilianzisha ile mada,sikudhani kama ingekukwaza,lkn niliuliza tu ni wapi huyu Mzee wa Butiama aliwazidi "Ujanja" wazee wa K'koo??

Hata hiyo Ujanja,niliiweka kwenye alama hizi " "...Leo kwa kusoma mada hii,naona kama Mzee wangu nayemuheshimu sana Mohamed Said kanijibu "kinamna" lile swali langu.Nimecheka sana kwa kweli...Julius alikuwa machachari sana.

Kwamba mchana anaenda Kkoo,anagongea msosi kwa Sykes,anarudi tena pale Sokoni anakabidhiwa misosi ya kwenda nayo Magomeni nyumbani,halafu msindikizaji anamsahau?Ha ha ha ha ha ha!
 
Na inasemekana hata huyo Abdulwahid Sykes alipofariki huyo bwana mkubwa hakuwa na mpango wa kuhudhuria mazishi lakini mkewe alimsihi aende kwani isingeleta picha nzuri ndio ikabidi aende tu kama kujitoa kimasomaso.
Mkuu ni bahati mbaya au nzuri tunapata ya upande mmoja,huyu wa upande wa pili watu wake hawatoi sana maelezo ya kutosha!!

Ila palikuwa na kitu katikaki!!Julius anajuwa walichotaka kumfanya huyu jamaa kwa kutaka "kumuondoa"...Yeye aliwajibu kwa "ukimya mkuu"!!Kuna siri zinahitaji miaka 50 ili ziweze "kufunguliwa"...Itafika siku kila kitu kitajulikana
 
Na inasemekana hata huyo Abdulwahid Sykes alipofariki huyo bwana mkubwa hakuwa na mpango wa kuhudhuria mazishi lakini mkewe alimsihi aende kwani isingeleta picha nzuri ndio ikabidi aende tu kama kujitoa kimasomaso.
Mumba...
Haikuwa hivyo.

Wakati Abdul Sykes anafariki Tanzania ilikuwa imegubikwa na mgogoro
wa East Africa Muslim Welfare Society.

Hiki ni kisa kirefu ukitaka kukijua ingia hapo chini:
Mohamed Said: BAKWATA SEHEMU YA SITA

Kwa ajili ya mgogoro huu kati ya serikali na Waislam hali Dar es Salaam
kwa taarifa za vyombo vya usalama haikuwa nzuri kwa Mwalimu Nyerere
kuhudhuria maziko yale ambayo toka asubuhi umma ulimiminika nyumbani
kwa mama yake Bi. Mruguru biti Mussa wa Mtaa wa Lindi yalipokuwa mazishi.

Wakashauri kuwa ni bora Mwalimu kwa ajili ya usalama asihudhurie maziko
yale.

Rashid Kawawa akamwambia Nyerere kuwa asingefahamika Dar es Salaam
kama si kwa Abdul Sykes na akiacha kwenda mazikoni hatoeleweka.

Kawawa akaamrisha kuwa ulinzi uimarishwe na Mwalimu Nyerere ahudhurie
maziko yale.

Mwalimu Nyerere alipeleka ngo'mbe mzima kwa Mama Abdul kwa ajili ya
msiba ule.

Mwalimu Nyerere alihudhuria maziko yale ambayo kwa wakati ule yaliweka
rekodi.

Hapajapatapo kutokea mazishi yaliyohudhuriwa na watu wengi kama maziko
ya Abdul Sykes.

Mzee Ahmed Rashad Ali amenihadithia kuwa yeye alikaa jamvi moja na
Nyerere pale mazikoni na walikula pilau sinia moja mkono kwa mkono.

Abdul Sykes na Ahmed Rashad walikuwa marafiki toka wako wadogo 1939
walipojulishwa na wazee wao katika ofisi ya Arab Association wakati wa Bank
Holiday na wakawa kama ndugu.
 
Barafu,
Nimesoma kila kitabu, kila jalada katika majalada ya Nyaraka za Sykes
kutafuta labda kuna mahali ambapo palikuwa na mkuruzano sikuweza
kupata kitu.

Nimefanya mazungumzo mengi na Ally Sykes, Ahmed Rashad Ally,
Hamza Aziz, Zuberi Mtemvu, Ally
na Mwinyi Tambwe.

Sijapata kitu kuwa kulikuwa na uadui wowote baina ya wazalendo hawa.

Nimezungumza na wazee wengi wa Dar es Salaam kuhusu siasa baada
ya uhuru.

Sikupata kitu ila tatizo la kuvunjwa kwa Baraza la Wazee wa TANU 1963
na kukamatwa na kuwekwa kuzuizini masheikh kuanzia 1964 baada ya
maasi ya jeshi na kuvunjwa kwa East African Muslim Welfare Society na
Nyerere kuunda BAKWATA na kukamatwa kwa Mufti Sheikh Hassan
bin Amir
.

Haya ndiyo mambo yaliyotia dosari mapenzi ya Waislam kwa Nyerere.

Lakini haya niliyoeleza hapo juu mimi binafsi niliyajumuisha kuwa ni uoga
wa Nyerere kuwa Waislam katika Tanganyika kutaka kujenga Chuo Kikuu
na kwa hakika jiwe la msingi aliliweka yeye.

Hili la Waislam kupata elimu ya juu ilijaza hofu Kanisa.

Picha ilianza kujitokeza kwa kitabu cha Bergen mwaka wa 1981, ''Religion
and Development in Tanzania.''

Sasa mwaka wa 1992 Sivalon alipokuja kuandika kitabu, ''Kanisa Katoliki
na Siasa ya Tanzania Bara 1952 - 1985,'' (Ndanda 1992) kitendawili hiki
kikateguka.

Sijakuta popote kuwa palikuwa na njama za Waislam kumwendea Nyerere
kinyume.



Hivi karibuni waandishi wa kitabu cha maisha ya Mwalimu Nyerere walinitafuta
niwapatie kitabu cha Bergen.

Inaelekea na wao wanataka kujua ukweli wa yale aliyoandika Bergen kuhusu
Nyerere kuwa aliahidi kulipa nguvu kanisa lake katika nchi ya kisekula na yeye
akiwa kiongozi mkuu.

Historia hii inataka utulivu wa akili.
Haitaki hamaki wala kuifunga akili ukawa unapenda kusikia kinachokufurahisha.

Barafu,
Nyerere hakutaka ''kufanywa,'' lolote na wazee wetu.
Wala hakuna jipya la kufunguliwa.

Abdul Mtemvu akiandika gazeti la ''Change,'' katika miaka ya 1990
alimfanyia mahojiano Dossa Aziz nyumbani kwake Mlandizi.

Alimuuliza Dossa, ''Baada ya haya yote kutokea baina yenu ikiwa leo
mtarudi Arnautoglo kufanya uchaguzi kati ya Abdul Sykes na Julius
Nyerere
, utamchagua nani?''

Jibu nakuachieni nyie mkisie nini alisema Dossa Aziz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…