Tatizo ni hizi admission tunazisikia kwako tu,nowhere else
Jackline1,
Wapi utazisikia ndugu yangu habari za
Abdul Sykes ikiwa wanahistoria walimsusa?
Kwani kabla ya mimi kuandika kitabu cha
Abdul wewe ulimjua?
Kumrejesha kwangu katika historia ndiko kulikoninyanyua mimi na kitabu changu
kwani nilikuja na mambo yaliyowastaajabisha wasomi wengi duniani katika tasnia
ya African History.
Walisoma katika kitabu hicho mambo ambayo yalikuwa mapya kwao.
Hii ndiyo iliyonifanya niingizwe katika Cambridge Journal of African History na kuwa
mmoja wa waandishi katika mradi wa Dictionary of African Biography (DAB).
Huu ulikuwa mradi wa Harvard na Oxford University Press New York.
Katika kitabu cha
Abdul Sykes kuna mahali nimemlaumu
John Iliffe kwa yeye
kutumia
Nyaraka za Sykes kuandika historia ya African Association akimtumia
mwanafunzi wake
Daisy Sykes binti ya
Abdul, lakini alishindwa kuchukua juhudi
yoyote kumtafuta
Abdul Sykes kumhoji kuhusu TANU.
Hii ya Makerere ni ndogo wala isitushughulishe inafahamika na ''contemporaries,''
wake wote si ''news,'' kwangu.
Sikiliza hii.
Siku moja
Kleist Sykes, huyu ni mtoto wa
Abdul Sykes kanipigia simu ananiomba
niende ofisini kwake nikaangalie kitu.
Nilipofika akanitolea barua mbili zote za mwaka wa 1953.
Moja ni ''Admission Letter,'' ya Princeton University na ya pili ni barua kutoka kwa
Earle Seaton.
Barua hizi mbili zote zina uhusiano.
Barua ya
Earle Seaton anampongeza
Abdul Sykes kwa kupata nafasi Princeton na
katika barua ile anamwambia kuwa akiwa New Jersey asikose kwenda UNO kusikiliza
majadiliano ya Nchi Zilizokuwa Chini ya Udhamini wa UNO.
New Jersey ni jirani sana na New York ilipo UN na ndipo kilipo Chuo Cha Princeton.
Kleist kaniahidi kunipatia nakala za barua hizo na nikizitia mkononi nitaziweka hapa
sote tuzisome.
Kwa wasiomjua
Earle Seaton nitawapa kwa kifupi tu historia yake In Shaallah.
Kwanza
Seaton na
Abdul walikuwa marafiki na
Abdul alimtia katika TAA
ili asaidie katika Constitutional Development Committee ya
Gavana Edward
Twining ya 1949.
Seaton alikuwa mwanasheria akiwa na ofisi yake Moshi.
Ulipozuka Mgogoro wa Meru
Abdul akamuomba
Seaton aisaidie Meru Citizens Union ya
kina
Japhet Kirilo kuandika ''petition,'' kwenda UNO.
Kwa habari zaidi ingia:
Mohamed Said: ABDULWAHID SYKES, JAPHET KIRILO, NA EARLE SEATON, 1952
Mohamed Said: KLEIST SYKES (1894 - 1949) KATIKA DICTIONARY OF AFRICAN BIOGRAPHY (DAB) OXFORD UNIVERSITY PRESS, NEW YORK