Mimi binafsi daima nitakushukuru-kuna majina nilikuwa nayasikia nikidhani hawa wanajulikana sababu ni malwatan wa mjini,kumbe it was more then that-hapo nakushukuru wewe na management ya JF-otherwise mengi tusingeyajua-Mimi nime major katika history-but believe me nilikuwa mweupe kabisa katika aspects nyingi za taifa hili
Azam TV Saba Saba Day 2015
Jackline,
Abdul Sykes na
Dr. Kleruu walianza kuandika historia ya TANU 1962/63
baada ya mazungumzo kati ya
Abdul Sykes,
Mwalimu Kihere na
Dossa
Aziz.
Aliyekuja na fikra hii alikuwa
Mwalimu Kihere na
Nyerere akaunga mkono
na yeye ndiye aliyesema
Abdul aandike kwa kuwa yeye anajuwa mengi
kutokana na historia ya baba yake
Kleist Sykes, kuwa muasisi wa African
Association.
Abdul Sykes akajitoa baada ya kumdhihirikia kuwa kilichokuwa kinatafutwa si
historia ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Dr. Klerruu alikamilisha ule mswada lakini kitabu hakikuchapwa hadi hii leo.
Inasemekana huu mswada na baadhi ya yale ambayo
Abdul aliyoandika upo
katika maktaba ya CCM mahali fulani hakuna ajuaye wapi.
Hata hivyo kuna mwana TANU mmoja katika vijana wa Youth League aliuiba
huu mswada akabadilisha hapa na pale na kuchapa kitabu kwa jina lake alichokiita
historia ya TANU.
TANU walimuonya asichape tena kitabu kile.
Kitabu hiki mimi alinipa baba yangu na naamini kilimvunja moyo sana kwa yale
aliyokuta mle kwani yeye aliiona TANU ilivyoanza toka ile siku ya kwanza kwani
Abdul Sykes alikuwa rafiki yake wa karibu sana toto utoto wao.
Kitabu hiki hakina tofauti kubwa sana na kile kitabu cha Kivukoni College, ''Historia
ya TANU.''
Ikawa sasa kama imewekwa sheria fulani kuwa ni marufuku mtu kuja na historia
ambayo haitaanza na
Mwalimu Nyerere.
Ikawa hata inaposemwa kuwa
Nyerere alichukua uongozi wa TAA mwaka wa 1953
haielezwi kachukua vipi na kachukua kutoka kwa nani.
Ikawa kwa njia hii jina la
Abdul Sykes halitajwi.
Ikawa vilevile ni mwiko mkubwa kueleza historia ya Waislam katika kuunda TANU na
kupigania uhuru wa Tanganyika kiasi mwaka wa 1988 gazeti la Africa Events (London)
toleo zima lilikusanywa kwa mimi kule kumtaja
Abdul na
Ally Sykes,
Saadan Abdul
Kandoro,
John Rupia na mchango wa Waislam katika kuasisi TANU.
Lakini jambo la kustaajabisha sana ni mfano wa
Earle Seaton na
Japhet Kirilo.
Hawa waliandika kitabu maarufu, ''The Meru Land Case,'' kuhusu mgogoro wa ardhi
iliyoporwa na Wazungu kule Meru.
Hii ilikuwa mwaka wa 1952 na wakati ule
Abdul alikuwa Kaimu rais wa TAA na secretary.
Abdul alishughulika sana na kesi hii na yeye ndiye aliyemtaka
Seaton aichukue kesi ile
na kuandika ''petition,'' kwenda UNO.
Ilipofika wakati wa
Kirilo kwenda New York UNO Waingereza wakakataa kumpa pasi ya
kusafiria.
Abdul akahangaika kama rais wa TAA kusimama kidete hadi Waingereza wakasalimu amri
wakampa
Kirilo pasi.
Kirilo na
Seaton walipokuja kuandika kitabu chao, hakuna popote
Abdul ametajwa.
Hili mimi linanistaajabisha hadi leo.
Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa kila mwandishi aliyekuja kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika
ukimtoa
Judith Listowel, ''The Making of Tanganyika.''
Lakini kubwa kabisa ambalo mimi linanishangaza ni kuwa katika ''review'' ya
John Iliffe na ya
Jonathon Glassman kuhusu kitabu cha
Abdul wote hawakubali kuwa
Abdul ndiye muasisi wa TANU.
''Review,'' zote hizi zipo katika Cambridge Journal of African History.
Glassman yeye alinialika kuzungumza chuoni kwake Northwestern University, Evanston Chicago
na nilizungumza katika ukumbi wa
Eduardo Mondlane.
Mjadala ulikuwa mkali.
Lakini aliniambia kitu kimoja kuwa wao kabla yangu hawakujua kuwa katika kupigania uhuru
wa Tanganyika kulikuwa, na kwa kutumia maneno yake, ''strong Muslim movement.''