Mindi,
Mwalimu Nyerere alipata kusema watafutwe wazalendo waliojiunga na TANU
kati ya 1954 - 1958 kwa maneno yake alisema kuwa kile kilikuwa kipindi kigumu.
Maneno haya aliyasema Tabora mkutanoni katika sherehe za kuadhimisha miaka
20 ya Azimio la Busara.
Kisa cha
Mwalimu kusema maneno yale katika hotuba yake ilikuwa kutokana na
swali alililoulizwa na
Ramadhani Singo.
Huyu
Ramadhani Singo alikuwa mlinzi wa
Nyerere Tabora wakati wa mkutano
ule wa Kura Tatu, akiwa na
Mwalimu mchana na usiku akikesha nje ya nyumba
ambayo
Nyerere alifikia.
Mwalimu Nyerere alipokutana na wana TANU wa Tabora kundi lile la akina
Singo,
Singo alimkabili
Nyerere akamwambia, ''
Mwalimu mbona umetusahau wenzio?
Angalia hali zetu zilivyokuwa...''
Kundi zima lile la TANU waasisi pale Tabora waliokuwa hai walikuwa mbele yake na
kwa hakika wote walikuwa hali zao taaban kwa kuwaangalia tu.
Singo katika ujana wake alikuwa na sifa ya kupigana na ujasiri na hii ndiyo sababu
ya yeye kupewa kazi ya ulinzi wa
Mwalimu Nyerere na bila shaka ndiyo huu ujasiri
wa kumkabili
Nyerere na maneno yale.
Ndipo
Nyerere alipopanda jukwaani kulihutubia taifa akasema maneno yale.
Shariff Abdallah Attas alikuwa na mengi katika historia ya TANU siku zile za mwanzo.
Kuna kisa cha Mzungu Town Clerk ambalo Kariakoo Market ilikuwa chimi yake na huyu
Mzungu ndiye alikuwa ''boss,'' wa
Abdul Sykes na
Shariff Attas.
Kisa hiki ametuhadithia
Shariff Attas siku ile ya Eid.
Anasema Mzungu zimemfikia taarifa kuwa
Abdul anauza kadi za TANU ofisini kwake.
Mwingireza akamvamia
Abdul ofisini kwake na akazikuta kadi tena
Abdul kazitoa
mwenyewe katika mtoto wa meza akaziweka juu ya meza yake huku maneno yakimtoka
kuwa asimtishe TANU ni chama halali na mtu yeyote anaweza kuwa na kadi za TANU
popote.
Abdul anamjibu Muingereza Town Clerk ''boss,'' wake kwa ile ''perfect English,'' yake.
Sifa moja kubwa ya
Abdul Sykes ilikuwa kuzungumza Kiingereza vizuri.
Mawazo Shomvi, huyu alikuwa mchezaji mpira wa Yanga katika miaka ya 1960 ananambia,
''Mimi iko siku nilikwenda ofisini kwa
Abdul Sykes nikamkuta anazungumza Kiingereza na
mtu, nilipigwa na butwaa jinsi alivyokuwa anazunguza vizuri lugha ile.''
Muingereza na
Abdul wakabwatizana hadi nje ya ofisi watu wakajazana kumtazama
Abdul
anavyopimana ubavu na Muingereza.
Shariff Attas akamgeukia
Kleist akamwambia, ''Baba yako alikuwa jeuri wakati mwingine.''
Wafanyabiashara wa Kariakoo
Mshume Kiyate,
Shariff Mbaya Mtu na wenzao wakakutana
ghafla kufanya kisomo cha kuchinja ili Muingereza asije kusababisha
Abdul afukuzwe kazi kwa
ajili ya TANU.
Kisa hiki pia alipata kunihadithia
George Kissaka mtoto wa
Mzee Kissaka ambae alikuwa
akifanya kazi pale sokoni chini ya
Abdul Sykes.
George anasema baba yake alipata kumuhadithia kisa hiki.
Stori za TANU miaka ile ya mwanzo zinasisimua sana na kama alivyosema
Baba wa Taifa, kile kilikuwa kipindi kigumu sana.
Soko la Kariakoo kama lilivyokuwa katika miaka ya 1950
Kwa taarifa zaidi za historia ya Soko la Kariakoo wakati wa kuaisisi TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika ingia hapo chini:
Mohamed Said: KARIAKOO MARKET 1949 MOJA YA KITUO CHA HARAKATI ZA SIASA DAR ES SALAAM