pepoMgalatia
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
pepoMgalatia
Bukyanagandi,Hivi akina Chiota si walikuwa wakimbizi kutoka Zimbabwe mtu na mdogo wake, mmoja wao alikuwa anakimbia sana mbio za mita 100, walikuwa wanachuana sana na Balozi Hamis S. Kagasheki nafikiri mwana riadha alikuwa ni Norman huyu mwingine Raymond alifanya kazi Tazara alioa Mrusi sijui alisoma Urusi. Au siyo wao?
Nkuba25,Mzee wangu Mohamed nimekunyooshea mikono.
Ila changamoto iliyoko Sasa, kadiri unavyojitahidi kuwaelewesha vijana juu ya Historia ya Tanzania na vijana wa wakati huo, hawataki kabisa kukuelewa.
Unatoa hadi ushahidi wa picha lakini hawataki kuelewa.
Lakini siku moja mzee wangu utakumbukwa sana sana.
Mungu akujalie mapenzi yake na rehema zake.
Window7,Mzee Mohamed Said umenifunza mengi juu ya historia yetu. Labda sijapekua sana lakini ningependa kujua historia yako pia.
Mnoel,Maneno meeengi...hayana maana...nyie waandishi ndio magufuli hawataki...
Mnoel,
Mtu wa maana nitakuwa mie kaka?
Mbona unauliza jibu?
Shukuru Mungu wewe kakupa akili pevu ukawa na uwezo wa kusoma kitu
ukakichambua ukajua kama hiki cha maana na huu upuuzi.
Si kila mtu kajaaliwa kama wewe ndugu yangu.
Nistahamile ndugu yangu hivyo hivyo,
Umejua kuitumia vyema lugha kiswahili![]()
Shariff Abdalla Attas
(Picha kwa hisani ya Bwana Shomari)
Sie wengine tumekuja kumjua Shariff Abdallah Attas katika utu uzima wake akikaa Mtaa wa Twiga na Sikukuu nyumba yake mkabala na Msikiti wa Shadhili Dar es Salaam.Katika miaka ya 1950 Shariff Attas alikuwa akifanyakazi Soko la Karikaoo kama dalali wa soko. Market Master akiwa Abdulwahid Sykes. Sifa kubwa ya Shariff Attas ni ubingwa wake katika hesabu. Yeye alikuwa na uwezo wa kukokotoa hesabu ndefu kichwani bila ya kutumia ‘’calculator.’’
Kisa chake hiki ninachokieleza nimekisikia kwa masikio yangu mwenyewe miaka kadhaa nyuma takriban zaidi ya 25 hivi sasa..
Ilikuwa siku ya Eid El Fitr mimi na Kleist, mtoto wa Abdul Sykes tumekwenda kusali Eid Msikiti wa Kitumbini. Kleist ana uhusiano mkubwa sana na msikiti huu kwani hapo katika miaka ya 1930 babu yake alikuwa akienda kuswali hapo huku kafatana wa wanae Abdul, Ali na Abbas.
Habari hii kanihadithia Ali Mwinyi Tambwe. Mzee Ali Mwinyi alikuwa kaniita nyumbani kwake Kinondoni Block 41 ili asahihishe baadhi ya mambo ambayo alikuwa kasoma katika mswada wa kitabu cha Abdul Sykes, mswada ambao mwane mmoja Abdulrahman Mbamba alikuwa kamwonyesha. Kabla ya kuanza mazungumzo yetu akanambia, ‘’Mimi Abdul hanipati kabisa mimi nikimuona akija kuswali na baba yake pale Kitumbini mtoto mdogo kashikwa mkono. Si huu msikiti unaouna hii leo, msikiti ule wa zamani.’’
Msikiti huu ndipo baba yake Kleist, Abdulwahid Sykes alipofanyiwa sala ya jeneza kabla hajakwenda kuzikwa Mkaburi ya Kisutu. Kwa hiyo sikushangaa Kleist aliponiambia tukasali Eid Kitumbini. Nakumbuka wakati ule Kleist alikuwa na Mercedes Benz nyekundu, gari ya kupendeza sana. Nami nikawa sishi kumtia tashtiti kuwa kafuata nyayo za baba yake kwa kuwa baba yake amekufa gari yake ikiwa Mercedes Benz. Nikimpiga vijembe hivi yeye kazi ilikuwa kucheka tu.
Baada ya kumaliza kuswali na kupena mikono na wazee wetu…Kleist hapo yeye ndipo alikuwa anakutana na rafiki wa maehemu baba yake na sasa ni watu wazima sana yeye akawa kila akitoa mkono anaufumba anamwachia kitu mzee wake. Tulipomaliza akanambia, ‘’Mohamed sasa twende kwa Shariff Attas.’’ Tulipofika kwa Shariff Attas tukakuta veranda yake imejaa ‘’who’s who’’ katika wazee maarufu wa Dar es Salaam, mmoja wapo marehemu Bwana Hamida Tuli, muungwana wa Kizaramo kutoka Masaki. Bwana Tuli akiishi Mtaa wa Matumbi hapo jirani. Mikeka ya rangi nzuri nzuri imetandikwa na udi unatoa riha nzuri, Sinia zimejaa maakuli - kaimati, maandazi, visheti, vitumbua, tambi, katlesi, kababu, sambusa nk. Tumewakuta wazee wetu wanafuturu. Shariff kumuona Kleist kafurahi sana kupita kiasi anamwashiria aje akae ubavuni kwake. Mara tumeletewa sahani na vikombe tunakaribishwa chai.
Mara Bwana Hamida Tuli kasimama anaomba ruksa kwa niaba ya wenzake anasema, ‘’Shariff tunaomba ruksa tuondoke kwa kuwa tumelaikwa chai Ikulu kwa Rais Ali Hassan Mwinyi.’’
Basi ikapigwa fatha ikaombwa dua wazee wakapeana mikono na Shariff Attas hao wakatimka kwenda Ikulu kunywa chai na rais. Ukumbi ukabaki mtupu tuko sie watatu tu - Shariff Attas, Klesit na mimi. Kleist akaangua kicheko kile cha kejeli. Shariff Attas yeye ni babu yake anamtania na kumuogelea atakavyo. Hizi ndizo mila zetu watu wa pwani.
‘’Duu, Shariff wenzako wote wanaalikwa Ikulu kwa rais, wewe uko hapa huna akujuaye!’’ Kleist anaangua kicheko. Shariff Attas hakuwa mdogo hivyo ni mtu maarufu kwa watu maarufu wa mjini na wenye majina ya kutajika.
Shariff Attas yuko kimya kaagemea ukuta anamtazama kwa jicho la deko hasemi kitu. Kleist kamaliza kumcheka Shariff. Mkono unakwenda kwenye sambusa, kababu, kaimati.
‘’Kleist sikiza bwana. Mimi kama kuingia Ikulu ningeliingia enzi za Nyerere yeye ndiye alikuwa mwenzangu. Mimi Mwinyi atanijulia wapi?’’ Shariff Attas akaanza.
Mimi masikio yangu yashakuwa walu namtazama Shariff usoni. Picha naniyoiona siyo ile ya dakika mbili zilizopita. Namuona Shariff ghafla amebadilika anaacha maskhara anataka kusema jambo.
‘’Sikiza Kleist, hiyo ni 1954 Nyerere anakaa kwa baba yako pale Stanley ndiyo TANU inakuja juu. Nyerere kesha acha ualimu. Anakuja ofisini kwa baba yako pale Kariakoo Market. Ikifika mchana Abdul ananiita ananiambia nifatane na Nyerere nyumbani kwa ajili ya chakula cha mchana. Mimi na Nyerere mguu kwa mguu, tunaingia Swahili, Narung’ombe, Gogo, Mchikichi, Sikukuu hadi Stanley kwa mama yako Mama Daisy. Njia nzima mimi na Nyerere tunazungunza. Wkati ule hakuna anaemjua. Tunafika nyumbani kwa baba yako chakula kipo mezani tunakula tukimaliza tunarudi ofisini pale kwa baba yako pale sokoni. Yeye alikuwa hatoki anaendelea na kazi. Nyerere alikuwa mwenzangu na mzungumzaji wangu sana wakati ule.
Basi miaka ikenda hadi tukapata uhuru na Nyerere akawa Waziri Mkuu.
Siku hiyo mimi niko ofisi ya TANU ghafla Nyerere anaingia watu hamkani wamesimama na Nyerere anaanza kupeana mikono na watu walioko pale hadi akafika kwangu nami nikampa mkono. Nyerere akanitazama nami nikamtazama tukawa sote tunatazamana usoni. Nyerere akasema,‘’Mzee tumepata kukutana?’’ Mimi nikamjibu, ‘’Hapana hatufahamiani.’’
Basi akapita kusalimiana na watu wengine. Sasa Kleist mimi ilikuwa niingie Ikulu enzi za Nyerere rafiki yangu lakini bahati mbaya kanisahau.’’
Shariff Attas alikuwa mtu wa tasnifa sana.
Akajinyoosha kaegemea ukuta anamtazama Kleist kwa mtazamo wa jicho la pemebeni huku uso umejaa tabasamu kama vile anamwambia mjukuu wake Kleist, ‘’Nimekukomesha kwa kutaka kwako kunicheka ati sijaalikwa Ikulu.''
Mimi nilishusha pumzi kwani nilikuwa nimechoka kwa kisa kile kilichokuwa kimetokea kwa wakati ule zaidi ya miaka arobaini nyuma.
Kleist akaomba ruksa na Shariff akaturuhusu baada ya kupiga fatha. Kleist wakati tunatoka akaingia jikoni kwa mke wa Shariff Attas kwenda kuaga.
Tulipokuwa sasa tunatoka nje Shariff Attas akampigai kelele Kleist, ‘’Kleist bibi yako umempa shilingi ngapi?’’
Kleist akacheka akamjibu Shairff, ‘’Nenda kamuulize mwenyewe.’’
Shariff akawa anacheka kwa ndani ya nyumba na sisi tunacheka hapo nje.
![]()
Gazeti hili ndilo lililochapa kisa cha Shariff Attas na Nyerere mwaka wa 2006
Nakala ya gazeti hili nimekuta katika Nyaraka za Ally Sykes miaka mitatu baada ya kifo chake
![]()
Hiyo hapo juu kulia katika gazeti ndiyo ilikuwa nyumba ya Abdul Sykes aliyosihi na Nyerere 1954
Nyumba hii ilikuwa Mtaa wa Stanley na Sikukuu
Enzi za akina STALIN,wewe ungeishia Siberia
Nashindwa kuelewa,kujua kwote huku,you seems to be in the know in many aspects-kitu ambacho Tazania ina lack sana, how come you never hit the heights katika nchi hii. AU from the word go walikustukia utageuza ofisi kuwa place of worship??
Tatizo ni hizi admission tunazisikia kwako tu,nowhere else
kwahiyo ulivyofundishwa shule hutaki kuamini,but porojo za huyu mzee kwako ndo unaona ukweli?
Mindi,
Mwalimu Nyerere alipata kusema watafutwe wazalendo waliojiunga na TANU
kati ya 1954 - 1958 kwa maneno yake alisema kuwa kile kilikuwa kipindi kigumu.
Maneno haya aliyasema Tabora mkutanoni katika sherehe za kuadhimisha miaka
20 ya Azimio la Busara.
Kisa cha Mwalimu kusema maneno yale katika hotuba yake ilikuwa kutokana na
swali alililoulizwa na Ramadhani Singo.
Huyu Ramadhani Singo alikuwa mlinzi wa Nyerere Tabora wakati wa mkutano
ule wa Kura Tatu, akiwa na Mwalimu mchana na usiku akikesha nje ya nyumba
ambayo Nyerere alifikia.
Mwalimu Nyerere alipokutana na wana TANU wa Tabora kundi lile la akina Singo,
Singo alimkabili Nyerere akamwambia, ''Mwalimu mbona umetusahau wenzio?
Angalia hali zetu zilivyokuwa...''
Kundi zima lile la TANU waasisi pale Tabora waliokuwa hai walikuwa mbele yake na
kwa hakika wote walikuwa hali zao taaban kwa kuwaangalia tu.
Singo katika ujana wake alikuwa na sifa ya kupigana na ujasiri na hii ndiyo sababu
ya yeye kupewa kazi ya ulinzi wa Mwalimu Nyerere na bila shaka ndiyo huu ujasiri
wa kumkabili Nyerere na maneno yale.
Ndipo Nyerere alipopanda jukwaani kulihutubia taifa akasema maneno yale.
Shariff Abdallah Attas alikuwa na mengi katika historia ya TANU siku zile za mwanzo.
Kuna kisa cha Mzungu Town Clerk ambalo Kariakoo Market ilikuwa chimi yake na huyu
Mzungu ndiye alikuwa ''boss,'' wa Abdul Sykes na Shariff Attas.
Kisa hiki ametuhadithia Shariff Attas siku ile ya Eid.
Anasema Mzungu zimemfikia taarifa kuwa Abdul anauza kadi za TANU ofisini kwake.
Mwingireza akamvamia Abdul ofisini kwake na akazikuta kadi tena Abdul kazitoa
mwenyewe katika mtoto wa meza akaziweka juu ya meza yake huku maneno yakimtoka
kuwa asimtishe TANU ni chama halali na mtu yeyote anaweza kuwa na kadi za TANU
popote.
Abdul anamjibu Muingereza Town Clerk ''boss,'' wake kwa ile ''perfect English,'' yake.
Sifa moja kubwa ya Abdul Sykes ilikuwa kuzungumza Kiingereza vizuri.
Mawazo Shomvi, huyu alikuwa mchezaji mpira wa Yanga katika miaka ya 1960 ananambia,
''Mimi iko siku nilikwenda ofisini kwa Abdul Sykes nikamkuta anazungumza Kiingereza na
mtu, nilipigwa na butwaa jinsi alivyokuwa anazunguza vizuri lugha ile.''
Muingereza na Abdul wakabwatizana hadi nje ya ofisi watu wakajazana kumtazama Abdul
anavyopimana ubavu na Muingereza.
Shariff Attas akamgeukia Kleist akamwambia, ''Baba yako alikuwa jeuri wakati mwingine.''
Wafanyabiashara wa Kariakoo Mshume Kiyate, Shariff Mbaya Mtu na wenzao wakakutana
ghafla kufanya kisomo cha kuchinja ili Muingereza asije kusababisha Abdul afukuzwe kazi kwa
ajili ya TANU.
Kisa hiki pia alipata kunihadithia George Kissaka mtoto wa Mzee Kissaka ambae alikuwa
akifanya kazi pale sokoni chini ya Abdul Sykes.
George anasema baba yake alipata kumuhadithia kisa hiki.
Stori za TANU miaka ile ya mwanzo zinasisimua sana na kama alivyosema
Baba wa Taifa, kile kilikuwa kipindi kigumu sana.
![]()
Soko la Kariakoo kama lilivyokuwa katika miaka ya 1950
Kwa taarifa zaidi za historia ya Soko la Kariakoo wakati wa kuaisisi TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika ingia hapo chini:
Mohamed Said: KARIAKOO MARKET 1949 MOJA YA KITUO CHA HARAKATI ZA SIASA DAR ES SALAAM
vip mbona hicho kivazi chako kila ukipiga uko kweny vyuo vya makafir na sio madrasa?Mtanganyika...
Hunijui ndiyo maana.
Mbona suti ndiyo kivazi changu?
![]()
Lincoln Memorial Washington DC
Tunakushukuru sana,umetupa mwangaza mkubwa sana wa harakati zilivyoenda,umetujulisha mengi sana tuliyokuwa hatuyajui-na tumeweza kuchambua nakala zako kila mtu kwa kadri ya uwezo wetu but one thing no matter what Dr Julius Kambarage Nyerere was the epitomy of the struggle-contribution yake was 80%,the rest 20%-this is the grim reality. Erasing this,and rewriting history will need gigantic efforts of biblical proportions
Maneno meeengi...hayana maana...nyie waandishi ndio magufuli hawataki...
weka hapa watu waisome;sasa ukizaliwa dar ndo unakosa historia???Window7,
Mie nitakuwa na historia gani ya maana hadi mtu atake kuisoma kaka.
Mimi ni mtu wa Dar es Salaam ndiko nilikozaliwa.
Sina mambo muhimu kaka tupo tupo tu.
Nikifanya kazi bandarini sasa nimestaafu naishi Magomeni Mapipa.