Kisa cha Shariff Abdallah Attas na mwalimu Julius Nyerere ofisi ya TANU baada ya uhuru

Kisa cha Shariff Abdallah Attas na mwalimu Julius Nyerere ofisi ya TANU baada ya uhuru

Barafu,
Nimesoma kila kitabu, kila jalada katika majalada ya Nyaraka za Sykes
kutafuta labda kuna mahali ambapo palikuwa na mkuruzano sikuweza
kupata kitu.

Nimefanya mazungumzo mengi na Ally Sykes, Ahmed Rashad Ally,
Hamza Aziz, Zuberi Mtemvu, Ally
na Mwinyi Tambwe.

Sijapata kitu kuwa kulikuwa na uadui wowote baina ya wazalendo hawa.

Nimezungumza na wazee wengi wa Dar es Salaam kuhusu siasa baada
ya uhuru.

Sikupata kitu ila tatizo la kuvunjwa kwa Baraza la Wazee wa TANU 1963
na kukamatwa na kuwekwa kuzuizini masheikh kuanzia 1964 baada ya
maasi ya jeshi na kuvunjwa kwa East African Muslim Welfare Society na
Nyerere kuunda BAKWATA na kukamatwa kwa Mufti Sheikh Hassan
bin Amir
.

Haya ndiyo mambo yaliyotia dosari mapenzi ya Waislam kwa Nyerere.

Lakini haya niliyoeleza hapo juu mimi binafsi niliyajumuisha kuwa ni uoga
wa Nyerere kuwa Waislam katika Tanganyika kutaka kujenga Chuo Kikuu
na kwa hakika jiwe la msingi aliliweka yeye.

Hili la Waislam kupata elimu ya juu ilijaza hofu Kanisa.

Picha ilianza kujitokeza kwa kitabu cha Bergen mwaka wa 1981, ''Religion
and Development in Tanzania.''

Sasa mwaka wa 1992 Sivalon alipokuja kuandika kitabu, ''Kanisa Katoliki
na Siasa ya Tanzania Bara 1952 - 1985,'' (Ndanda 1992) kitendawili hiki
kikateguka.

Sijakuta popote kuwa palikuwa na njama za Waislam kumwendea Nyerere
kinyume.

Hivi karibuni waandishi wa kitabu cha maisha ya Mwalimu Nyerere walinitafuta
niwapatie kitabu cha Bergen.

Inaelekea na wao wanataka kujua ukweli wa yale aliyoandika Bergen kuhusu
Nyerere kuwa aliahidi kulipa nguvu kanisa lake katika nchi ya kisekula na yeye
akiwa kiongozi mkuu.

Historia hii inataka utulivu wa akili.
Haitaki hamaki wala kuifunga akili ukawa unapenda kusikia kinachokufurahisha.

Barafu,
Nyerere hakutaka ''kufanywa,'' lolote na wazee wetu.
Wala hakuna jipya la kufunguliwa.

Abdul Mtemvu akiandika gazeti la ''Change,'' katika miaka ya 1990
alimfanyia mahojiano Dossa Aziz nyumbani kwake Mlandizi.

Alimuuliza Dossa, ''Baada ya haya yote kutokea baina yenu ikiwa leo
mtarudi Arnautoglo kufanya uchaguzi kati ya Abdul Sykes na Julius
Nyerere
, utamchagua nani?''

Jibu nakuachieni nyie mkisie nini alisema Dossa Aziz.

Shukran Sana kwa facts hizi za historia Ya Tanganyika ambazo are very interesting
Tatizo lako kaka unapotea sana na najua pilika za maisha ni nyingi
Ila ujue kwamba huwa na enjoy sana kusoma michango yako hapa JF
My 2 cents
 
Kuna siku ulihadithiwa uzushi ukauleta huku na badae mhusika alipoukana ukaja kututaka radhi... Kwako lililo jema ni kumsema mwl Nyerere tu kwa mabaya... Kwanin usihangaike kwa wakati uliopo kutoa mambo mazuri, pambana viwanja vya misikiti vinavyotaka kuporwa, pambana na ugaidi na chuki ovu zinazoenezwa katika nyumba za ibada, kwani Iraq, libya na kwingine nani wanafanya mauaji kwa dini zao... Acheni kutumia uhuru wenu vibaya na kufanya JF sehemu ya chuki.
 
Na inasemekana hata huyo Abdulwahid Sykes alipofariki huyo bwana mkubwa hakuwa na mpango wa kuhudhuria mazishi lakini mkewe alimsihi aende kwani isingeleta picha nzuri ndio ikabidi aende tu kama kujitoa kimasomaso.
Na itaendelea kusemekana sana tu...wewe ndio ulikuwa mke wake? Ulikuwepo? Udini ni shida aiseee.
 
Kuna siku ulihadithiwa uzushi ukauleta huku na badae mhusika alipoukana ukaja kututaka radhi... Kwako lililo jema ni kumsema mwl Nyerere tu kwa mabaya... Kwanin usihangaike kwa wakati uliopo kutoa mambo mazuri, pambana viwanja vya misikiti vinavyotaka kuporwa, pambana na ugaidi na chuki ovu zinazoenezwa katika nyumba za ibada, kwani Iraq, libya na kwingine nani wanafanya mauaji kwa dini zao... Acheni kutumia uhuru wenu vibaya na kufanya JF sehemu ya chuki.
Dongo...
Hapana chuki katika ninayoandika hili nina hakika nalo.
Labda wewe hupendezwi tu na haya ninayoandika.

Kuhusu ugaidi nina paper niliwasilisha Chuo Kikuu Cha
Ibadan, Nigeria 2006.

Unaweza kuisoma hap chini:
Mohamed Said: ISLAM, TERRORISM AND AFRICAN DEVELOPMENT

Hayo mengine ya viwanja nk. bahati mbaya sina ujuzi wa hayo.

Ningefanya JF mahali pa kueneza chuki au kubughudhi na kutukana watu
nadhani siku nyingi ningelikuwa nishafukuzwa.

Watu wengi wanapenda kunisoma fanya uchunguzi utalitambua hili.

Pia nina blog ambayo ni maarufu sana Marekani, Ulaya na Arabuni kiasi
nastaajabu.

Hii si dalili ya mtu anaeandika chuki.
Hata hivyo mimi naelewa hisia zako.

Hakika hii ''corrective history,'' ninayoandika imewafadhaisha watu wengi
sana.

Kuhitimisha ningependa kusema kuwa ule uzushi wa yule ndugu yangu kweli
umenisikitisha mno.

Ningeliweza kukaa kimya nisikuelezeni lakini ningekuwa sina amani katika nafsi
yangu.

Allah atuepusha na watu kama wale.
 
er3bQjXjUA-gIjirvYPZ7req0Qq9Vy1t9K3kKNqRFoltAKW2HjRaPgHuGfv7enUhi6x4K7Xj5GSVjw2IZb2hYfKanrQQmgaeG5-2ABlbQohvXjPYctrAhbvqMdKRO9kp0MLlAt5vt7zFKZal73DKMUpZEILcLU_6ANrk8kQaOdROeypele2WR7vaXsOhM1iXfSCdqKiJGdVIpUXf73td0aPDHkPQPIG6oNyhxXDYIuBOJkQ_iVlNTMUbIAXPFD9QDHaJez37AjexF3uwb4MWXblYp_C0q5aKQyid3Qo8UA4kNfDrdwgRNA92bCS08qSFgLmNZ5oluK8H66I1Y4sEeajSaW0EgSyUNfcrURvEfpb2cxOygCbl5GQvf_YAiVfb6hY6Vnv59m4TVVkJupd4l_M4kL99Hur8fH0pea2fEbTTtCeTnSK_Nrg8RkvfMYmMoSqIcqTZ4CAQMv8IDCv2NTwg_YVHi827JxcUuTmQtPwcFXYCtU_OPID59dP4zIwiKyhc307YfgRy3X9pvyHMt7z6ebwsgMefyJpLIMictYmeCo12RWtCMWmYLd0Ew6YqePFyFniOi8GH_gMKLve-kLioOq3CGv2hGbK54EOlPdehcZaa=w493-h657-no

Shariff Abdalla Attas
(Picha kwa hisani ya Bwana Shomari)

Sie wengine tumekuja kumjua Shariff Abdallah Attas katika utu uzima wake akikaa Mtaa wa Twiga na Sikukuu nyumba yake mkabala na Msikiti wa Shadhili Dar es Salaam.Katika miaka ya 1950 Shariff Attas alikuwa akifanyakazi Soko la Karikaoo kama dalali wa soko. Market Master akiwa Abdulwahid Sykes. Sifa kubwa ya Shariff Attas ni ubingwa wake katika hesabu. Yeye alikuwa na uwezo wa kukokotoa hesabu ndefu kichwani bila ya kutumia ‘’calculator.’’

Kisa chake hiki ninachokieleza nimekisikia kwa masikio yangu mwenyewe miaka kadhaa nyuma takriban zaidi ya 25 hivi sasa..

Ilikuwa siku ya Eid El Fitr mimi na Kleist, mtoto wa Abdul Sykes tumekwenda kusali Eid Msikiti wa Kitumbini. Kleist ana uhusiano mkubwa sana na msikiti huu kwani hapo katika miaka ya 1930 babu yake alikuwa akienda kuswali hapo huku kafatana wa wanae Abdul, Ali na Abbas.

Habari hii kanihadithia Ali Mwinyi Tambwe. Mzee Ali Mwinyi alikuwa kaniita nyumbani kwake Kinondoni Block 41 ili asahihishe baadhi ya mambo ambayo alikuwa kasoma katika mswada wa kitabu cha Abdul Sykes, mswada ambao mwane mmoja Abdulrahman Mbamba alikuwa kamwonyesha. Kabla ya kuanza mazungumzo yetu akanambia, ‘’Mimi Abdul hanipati kabisa mimi nikimuona akija kuswali na baba yake pale Kitumbini mtoto mdogo kashikwa mkono. Si huu msikiti unaouna hii leo, msikiti ule wa zamani.’’

Msikiti huu ndipo baba yake Kleist, Abdulwahid Sykes alipofanyiwa sala ya jeneza kabla hajakwenda kuzikwa Mkaburi ya Kisutu. Kwa hiyo sikushangaa Kleist aliponiambia tukasali Eid Kitumbini. Nakumbuka wakati ule Kleist alikuwa na Mercedes Benz nyekundu, gari ya kupendeza sana. Nami nikawa sishi kumtia tashtiti kuwa kafuata nyayo za baba yake kwa kuwa baba yake amekufa gari yake ikiwa Mercedes Benz. Nikimpiga vijembe hivi yeye kazi ilikuwa kucheka tu.

Baada ya kumaliza kuswali na kupena mikono na wazee wetu…Kleist hapo yeye ndipo alikuwa anakutana na rafiki wa maehemu baba yake na sasa ni watu wazima sana yeye akawa kila akitoa mkono anaufumba anamwachia kitu mzee wake. Tulipomaliza akanambia, ‘’Mohamed sasa twende kwa Shariff Attas.’’ Tulipofika kwa Shariff Attas tukakuta veranda yake imejaa ‘’who’s who’’ katika wazee maarufu wa Dar es Salaam, mmoja wapo marehemu Bwana Hamida Tuli, muungwana wa Kizaramo kutoka Masaki. Bwana Tuli akiishi Mtaa wa Matumbi hapo jirani. Mikeka ya rangi nzuri nzuri imetandikwa na udi unatoa riha nzuri, Sinia zimejaa maakuli - kaimati, maandazi, visheti, vitumbua, tambi, katlesi, kababu, sambusa nk. Tumewakuta wazee wetu wanafuturu. Shariff kumuona Kleist kafurahi sana kupita kiasi anamwashiria aje akae ubavuni kwake. Mara tumeletewa sahani na vikombe tunakaribishwa chai.

Mara Bwana Hamida Tuli kasimama anaomba ruksa kwa niaba ya wenzake anasema, ‘’Shariff tunaomba ruksa tuondoke kwa kuwa tumelaikwa chai Ikulu kwa Rais Ali Hassan Mwinyi.’’

Basi ikapigwa fatha ikaombwa dua wazee wakapeana mikono na Shariff Attas hao wakatimka kwenda Ikulu kunywa chai na rais. Ukumbi ukabaki mtupu tuko sie watatu tu - Shariff Attas, Klesit na mimi. Kleist akaangua kicheko kile cha kejeli. Shariff Attas yeye ni babu yake anamtania na kumuogelea atakavyo. Hizi ndizo mila zetu watu wa pwani.

‘’Duu, Shariff wenzako wote wanaalikwa Ikulu kwa rais, wewe uko hapa huna akujuaye!’’ Kleist anaangua kicheko. Shariff Attas hakuwa mdogo hivyo ni mtu maarufu kwa watu maarufu wa mjini na wenye majina ya kutajika.

Shariff Attas yuko kimya kaagemea ukuta anamtazama kwa jicho la deko hasemi kitu. Kleist kamaliza kumcheka Shariff. Mkono unakwenda kwenye sambusa, kababu, kaimati.

‘’Kleist sikiza bwana. Mimi kama kuingia Ikulu ningeliingia enzi za Nyerere yeye ndiye alikuwa mwenzangu. Mimi Mwinyi atanijulia wapi?’’ Shariff Attas akaanza.

Mimi masikio yangu yashakuwa walu namtazama Shariff usoni. Picha naniyoiona siyo ile ya dakika mbili zilizopita. Namuona Shariff ghafla amebadilika anaacha maskhara anataka kusema jambo.

‘’Sikiza Kleist, hiyo ni 1954 Nyerere anakaa kwa baba yako pale Stanley ndiyo TANU inakuja juu. Nyerere kesha acha ualimu. Anakuja ofisini kwa baba yako pale Kariakoo Market. Ikifika mchana Abdul ananiita ananiambia nifatane na Nyerere nyumbani kwa ajili ya chakula cha mchana. Mimi na Nyerere mguu kwa mguu, tunaingia Swahili, Narung’ombe, Gogo, Mchikichi, Sikukuu hadi Stanley kwa mama yako Mama Daisy. Njia nzima mimi na Nyerere tunazungunza. Wkati ule hakuna anaemjua. Tunafika nyumbani kwa baba yako chakula kipo mezani tunakula tukimaliza tunarudi ofisini pale kwa baba yako pale sokoni. Yeye alikuwa hatoki anaendelea na kazi. Nyerere alikuwa mwenzangu na mzungumzaji wangu sana wakati ule.

Basi miaka ikenda hadi tukapata uhuru na Nyerere akawa Waziri Mkuu.


Siku hiyo mimi niko ofisi ya TANU ghafla Nyerere anaingia watu hamkani wamesimama na Nyerere anaanza kupeana mikono na watu walioko pale hadi akafika kwangu nami nikampa mkono. Nyerere akanitazama nami nikamtazama tukawa sote tunatazamana usoni. Nyerere akasema,‘’Mzee tumepata kukutana?’’ Mimi nikamjibu, ‘’Hapana hatufahamiani.’’

Basi akapita kusalimiana na watu wengine. Sasa Kleist mimi ilikuwa niingie Ikulu enzi za Nyerere rafiki yangu lakini bahati mbaya kanisahau.’’

Shariff Attas alikuwa mtu wa tasnifa sana.

Akajinyoosha kaegemea ukuta anamtazama Kleist kwa mtazamo wa jicho la pemebeni huku uso umejaa tabasamu kama vile anamwambia mjukuu wake Kleist, ‘’NImekukomesha kwa kutaka kwako kunicheka ati sijaalikwa Ikulu.''

Mimi nilishusha pumzi kwani nilikuwa nimechoka kwa kisa kile kilichokuwa kimetokea kwa wakati ule zaidi ya miaka arobaini nyuma.

Kleist akaomba ruksa na Shariff akaturuhusu baada ya kupiga fatha. Kleis wakati tunatoka akaingia jikoni kwa mke wa Shariff Attas kwenda kuaga.

Tulipokuwa sasa tunatoka nje Shariff Attas akampigai kelele Kleist, ‘’Kleist bibi yako umempa shilingi ngapi?’’

Kleist akacheka akamjibu Shairff, ‘’Nenda kamuulize mwenyewe.’’

Shariff akawa anacheka kwa ndani ya nyumba na sisi tunacheka hapo nje.



iQl-N4u7N12cUVPdLGb_jw_LjTkiTjxz9DJ7wHC6LjOzHWmEPeflA3S8U20FOZFzuCwEV8lcuEQ=w469-h657-no

Gazeti hili ndilo lililochapa kisa cha Shariff Attas na Nyerere mwaka wa 2006
Nakala ya gazeti hili nimekuta katika Nyaraka za Ally Sykes miaka mitatu baada ya kifo chake

2016%2B-%2B1

Hiyo hapo juu kulia katika gazeti ndiyo ilikuwa nyumba ya Abdul Sykes aliyosihi na Nyerere 1954
Nyumba hii ilikuwa Mtaa wa Stanley na Sikukuu
Ahsante sana Mohamed kwani umenikumbusha mbali sana.
 
Ni nani hasa anayeficha historia na ni nani anayetakiwa kuandika historia??
 
Sooth,
Katika miaka ya 1960 kulikuwa na kundi la vijana wakijiita, ''Chipukizi Club,''
wakipiga muziki wa ''pop.''

Alikuwapo Hussein Shebe, Raymond Chihota, Cuthbert Sabuni, Chico,
Nanji, Badrin, Henin Seif, Mariam, Sauda
na wengineo wakiungana na
vijana wa Kigoa na band yao, ''The Blue Diamonds.''

Walikuwa na kipindi Radio Tanzania kila Jumamosi mchana kikiitwa ''Chipukizi
Club.''

Kipindi hiki walikuwa wakikifungua na nyimbo inaitwa, ''Here We Go Luubiluu.''

Hii ndiyo ilikuwa ''signature tune'' ya kipindi hicho.

ewpqn4-FaFMKjGmhSafT_UMcz8t-FyKsVV-2-Gg-QAc38mavJQyD20ScvJZkaqjLwP4vrt1VS0H-ElKU5V0uQyasw5BXoXFnRRJoReaWRTHmFmtgBKBRwlz7LThkgWqYS2KKC_B0Uc_6D6MGknvogomi8Ul9MU7obw406TfhOX1NA7Zg90DoAPyOMYt7qWb_OzAnc_Lin9Qzr7jrYNx0dZTrzGO7EaeulcnIGP_Id5eEy1Abvjq8_kw2N-HHUuUDlxi6w5NXpOIYNLxuUptE94kO4WptOJrzbjg0alqNmLBP8rBZDt7BtkRFN7sdgGHuZXrsU-Xtg4blOiEDtzp7R33S_Q327ywJvJP0TNssrb9rOt2iryFXL3CuCxhBwD8BBIWHBRQgCypnJJXHmb0f8NnfdFYTn4-R76I3vWKwRJctndYu20yMAP70HOtMSeh4dCqdzMsj1UQSxhS298cXfUiQffQwRu0i0wnrChRkc7nTc0hDP-1zaZIrz7dCVNE017hU0WOo8-FYvBYrbVMTaE_Rk8ktHdw3VNAdg_CwlLj8vN1DDu-NPcWVz9jfExkl4eRbU9u23jfz6eb2sLAyS1RCRnk6CxalgpmafqkpiODigqScLQ=w670-h526-no

Miaka hiyo mimi ndiye huyo hapo Mnazi Mmoja na nyuma yangu ni barabara
ambayo baadae ikajapewa jina Titi Street na hizo nyumba ni Soko la Kisutu.
Usisahau 'The Drifters wakifanya show show zao goan club na avalon na baadaye wakaja The Rifters[Kina Kingui???]
 
Enzi za akina STALIN,wewe ungeishia Siberia
Jackline1,
Kabla ya kupelekwa Siberia kwanza nimgepitishwa Lubyanka.

Kweli usemayo kalamu yangu ni kali na mimi ni mtu huru sina
ufungamano na upande wowote.

Stalin alipokufa daktari wake akaambiwa athibitishe kifo.

Daktari aliogopa akasema wasubiri kwanza asije Stalin
akaamka yakamkuta makubwa.

Ikiwa unapenda mambo haya soma kitabu hiki, Khrushchev
Remembers
, memoirs zake kaandika mwenyewe.

Pia angaia movie hii, ''The Tamarind Seed,'' Omar Sharif na
Julie Andrews...

Kuna mengi utajifunza.
 
Usisahau 'The Drifters wakifanya show show zao goan club na avalon na baadaye wakaja The Rifters[Kina Kingui???]
Abunuwas,
Nina picha niko na Adam Kingui na Rifters...
Namkumbuka rafiki yangu Adam (Allah amrehemu)...

Alikuwa akipiga guitar moja katika nyimbo ya Wilson Picket,
''A Man and a Half,'' guitar anapiga Bobby Womack...

Sijui Bobby Womack angemsikia Adam anavyomuiga upigaji wake
angesema kitu gani.

Adam alikuwa na kipaji.

Akicheza mpira Fulham United club ya Kipata karibu na nyumbani
kwao half back six, akicheza vizuri sana.

pdVfwKjmruRs1YrnhWrfWNEYt1p4tTYdlSCSAixOfHUC5AqScjQe1AOSVNcS-AILHL-sNGpaeiilekDJdyMyaFn-VJHnXEfH9mAVKOjLCnoOwdhkiBdb5xQLI1rfW-kMtzzZxDfBHSITDr40h0t3OmRUFK2-Cw04K8ePcbkJv4tz-yU8MuyvrC9slkeN0EX0XSrxPWPfg6WxtTL7U-UGIwvbkwGeI7pZqpYkrZegpFHGRdnoEnBSPa_Bu_qbGtYMqlTdKWP6VtwtUZo7j0Ckxhbey9MTgmfBqEsm_DvU-L_pfqFdQT0yE43iujs8z6MS-GvHXuK8ReMyQ5gqaS-GKrL8NQDLN-2Y-Z6cS58AX_PlEK9mNwnczQy2ItI-PHgkdI0DSREHw-1PGFdQhDiiXXIDW8B7G8vxD04HpXNjeRiNuYHTnxzY5HvbHZuimXOwjwGM8exVcshE-W0BTyGUjbmPaxT6mx7hYqGZh6sqNhDMfvFD7UDnA7OM2IvpOuEYNf4x8Fy0ycwpRSR288lC5047BZ9bKt3gNyr9BsP0mLzj0rKW2H_-Us2uRPQsq0nOYeObFXoatdKfc4z8GNI5DeEun9LmibfvcSALDTIiUpYDUXoBoQ=w876-h657-no

Kulia: Adam Kingui, Abdallah Mgambo, Kleist Sykes, Versi na Dimitri 1965
 
Shida ni kutaka utukufu wa kupitiliza,kuna mtu bila shaka alitaka kutengeneza taswira kwamba yeye ni kiumbe wa kipekee aliyeshushwa katika ulimwengu huu kwa ajili ya kuikomboa Tanganyika na kwamba bila yeye uhuru wa Tanganyika usingepatikana
nani huyo??
 
Jackline1,
Kabla ya kupelekwa Siberia kwanza nimgepitishwa Lubyanka.

Kweli usemayo kalamu yangu ni kali na mimi ni mtu huru sina
ufungamano na upande wowote.

Stalin alipokufa daktari wake akaambiwa athibitishe kifo.

Daktari aliogopa akasema wasubiri kwanza asije Stalin
akaamka yakamkuta makubwa.

Ikiwa unapenda mambo haya soma kitabu hiki, Khrushchev
Remembers
, memoirs zake kaandika mwenyewe.

Pia angaia movie hii, ''The Tamarind Seed,'' Omar Sharif na
Julie Andrews...

Kuna mengi utajifunza.
Nashindwa kuelewa,kujua kwote huku,you seems to be in the know in many aspects-kitu ambacho Tazania ina lack sana, how come you never hit the heights katika nchi hii. AU from the word go walikustukia utageuza ofisi kuwa place of worship??
 
J
Nashindwa kuelewa,kujua kwote huku,you seems to be in the know in many aspects-kitu ambacho Tazania ina lack sana, how come you never hit the heights katika nchi hii. AU from the word go walikustukia utageuza ofisi kuwa place of worship??
9
Jackline,
Mie si chochote nasafiria nyota ya wazee wangu.

Nimezaliwa kipindi kile cha kudai uhuru na watu
hawa na ndiyo sababu ya kujua yote hayo.
 
Sooth,
Katika miaka ya 1960 kulikuwa na kundi la vijana wakijiita, ''Chipukizi Club,''
wakipiga muziki wa ''pop.''

Alikuwapo Hussein Shebe, Raymond Chihota, Cuthbert Sabuni, Chico,
Nanji, Badrin, Henin Seif, Mariam, Sauda
na wengineo wakiungana na
vijana wa Kigoa na band yao, ''The Blue Diamonds.''

Walikuwa na kipindi Radio Tanzania kila Jumamosi mchana kikiitwa ''Chipukizi
Club.''

Kipindi hiki walikuwa wakikifungua na nyimbo inaitwa, ''Here We Go Luubiluu.''

Hii ndiyo ilikuwa ''signature tune'' ya kipindi hicho.

ewpqn4-FaFMKjGmhSafT_UMcz8t-FyKsVV-2-Gg-QAc38mavJQyD20ScvJZkaqjLwP4vrt1VS0H-ElKU5V0uQyasw5BXoXFnRRJoReaWRTHmFmtgBKBRwlz7LThkgWqYS2KKC_B0Uc_6D6MGknvogomi8Ul9MU7obw406TfhOX1NA7Zg90DoAPyOMYt7qWb_OzAnc_Lin9Qzr7jrYNx0dZTrzGO7EaeulcnIGP_Id5eEy1Abvjq8_kw2N-HHUuUDlxi6w5NXpOIYNLxuUptE94kO4WptOJrzbjg0alqNmLBP8rBZDt7BtkRFN7sdgGHuZXrsU-Xtg4blOiEDtzp7R33S_Q327ywJvJP0TNssrb9rOt2iryFXL3CuCxhBwD8BBIWHBRQgCypnJJXHmb0f8NnfdFYTn4-R76I3vWKwRJctndYu20yMAP70HOtMSeh4dCqdzMsj1UQSxhS298cXfUiQffQwRu0i0wnrChRkc7nTc0hDP-1zaZIrz7dCVNE017hU0WOo8-FYvBYrbVMTaE_Rk8ktHdw3VNAdg_CwlLj8vN1DDu-NPcWVz9jfExkl4eRbU9u23jfz6eb2sLAyS1RCRnk6CxalgpmafqkpiODigqScLQ=w670-h526-no

Miaka hiyo mimi ndiye huyo hapo Mnazi Mmoja na nyuma yangu ni barabara
ambayo baadae ikajapewa jina Titi Street na hizo nyumba ni Soko la Kisutu.
Shukran sana kwa History...
Namuelewa sana Ustadh Ilunga kwa maelezo yake....
 
Back
Top Bottom