Mkuu Mohammed Said kwa upeo huu uliotukuka ingefaa uwe visiting professor of african history kwenye medani Ya kimataifa
Naamini ulikuwa very close ma prof Mazrui, Haroub Othman na A M Babu kabla hawajafariki
Sheriff...
Hao uliowataja wote ni walimu wangu.
Mimi siwezi hata kuwabebea makubazi yao.
Kushoto: Tamim Faraj, Prof. Ali Mazrui na Mwandishi
Kampala 2003
Tuanze na
Prof. Mazrui.
Nilimpa jina na kumwita, ''My distant Professor,'' na yeye naamini alilipokea jina hili.
Hili ni jina ambalo nililoandika kwenye kitabu cha
Abdul Sykes nilichompelekea
mwaka wa 1998 kilipotoka.
Watu wawili ndiyo walioniunganisha na
Mazrui -
Balozi Dr. Ramadhani Kitwana
Dau na
Dr. Harith Ghassany.
Kitabu changu nilimkabidhi
Dr. Dau na yeye ndiye aliyempa mkononi kitabu hicho.
Prof. Mazrui akaniaandikia kunishukuru.
Baadhi ya maneno aliyoandika ni kuwa nimemfurahisha kwa kuonyesha nini Waswahili
wamefanya Tanganyika.
Ikawa mara moja moja tunaandikiana.
Mwaka wa 2003 kulikuwa na mkutano Kampala ambao
Prof. Ali Mazrui alihudhuria na
mimi nilialikwa na niliwasilisha mada.
Dr. Ghassany akanituma nimfikishie salamu zake kwa
Prof. Mazrui.
Sote tulikuwa tunakaa Kampala Nile Hilton na nilizifikisha salamu zile.
Prof. Mazrui alifurahi sana kuniona na kupokea salamu za
Dr. Ghassany kutoka kwangu.
Prof. Mazrui alikuwa na
Dr. Ghassany Michigan.
Prof. Mazrui nilimmaliza nilipomwambia kuwa mimi ni rafiki mkubwa wa
Sal Davis.
Mazrui na
Sal Davis ni ''ndugu wa ndugu,'' kama mwenyewe Sal anavyopenda kueleza.
Sal Davis alipopelekwa na baba yake,
Shariff Salim Abdallah kwenda kusoma Manchester
akiwa na umri wa miaka 17 mwaka wa 1957 alipokelewa na
Prof. Mazrui na waliishi nyumba
moja.
Lakini nilimwacha kinywa wazi nilipomweleza kuwa nimefika hadi kijijini kwao Takaungu, nje ya
Mombasa na kuona msikiti wao na kisima cha msikiti ambazo kina takriban miaka 400.
Nilimfahamisha kuwa nina ndugu zangu akina Baamumin katika kijiji cha Mtondia ambao wao
ni ''squatters'' katika ardhi ya akina
Mazrui.
Nina mengi ya
Prof. Mazrui lakini tuishie hapa.
Prof. Haroub Othman yeye kanisomesha khasa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam ni mwalimu
wangu kabisa.
Kumbukumbu aliyoniachia
Prof. Haroub ni moja, ni siku tulipokutana pembeni ya Msikiti wa
Ibadh na tukazungumza kuhusu kitabu changu ambacho ndiyo kwanza kilikuwa kimewasili
nchini kutoka Uingereza.
Hii ilikuwa mwaka wa 1998.
Mwalimu wangu alikuwa amesawajika.
Alikuwa amesoma katika kitabu cha
Abdul Sykes mambo mawili au matatu yaliyomshtua sana.
Hakuwa anayajua kabla.
Kwanza historia ya
Abdul Sykes na mchango wa wazalendo wengine katika kuasisi TANU.
Prof. Haroub kama ilivyokuwa kwa walimu wengi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaa walikuwa
wanaamini kuwa TANU iliasisiwa na
Julius Nyerere na siasa za kudai uhuru hazikuwapo kabla
yake.
Pili, mgogoro baina ya Waislam na
Nyerere baada ya uhuru na yale niliyoandika kwa urefu kuhusu
kutumika kwa vyombo vya dola dhidi ya masheikh wakati wa mgogoro ule.
Prof. Haroub akanieleza kuwa yeye alikwenda kwa
Nyerere kumuona ili amsikilize nini maoni yake
kuhusu yale ambayo mimi niliandika.
Prof. Haroub alimuomba
Nyerere aandike na yeye ili dunia isikie na yale ya upande wake.
Alimuomba kuwa amjibu na
Ali Muhsin Barwani kwa yale aliyoandika dhidi yake katika kitabu
chake, ''Conflicts and Harmony in Zanzibar,'' (1997).
Ningeliweza kusema mengi kuhusu mwalimu wangu
Prof. Haroub Othman lakini na tuishie hapa.
Ahmed Rajab na Mwandishi London 1991
Abdulrahman Babu nilijulishwa kwake London na
Ahmed Rajab na siku nzima tulishinda pamoja
Brixton sisi watatu mimi nikijibu maswali yao kuhusu hali ya siasa Tanzania na uongozi wa
Ali Hassan
Mwinyi.
Nilizungumza mengi na
Babu na nilimuuliza kuhusu yeye kuandika historia ya Mapinduzi ya Zanzibar
ya 1964 na aliniambia kuwa ataandika In Shaallah.
Babu hakuandika historia ile kwa sababu ambazo nilikuja kuzijua baada ya miaka kumi takriban.
Hawa wote,
Prof. Mazrui,
Prof. Haroub Othman na
Prof. Abdulrahman Babu, ni walimu wangu
na ni miamba ambayo kwa kweli mie ni kichuguu mbele yao.
Ingia hapo chini kwa picha zaidi:
Mohamed Said: KUTOKA JF: PROF. ALI MAZRUI, PROF. HAROUB OTHMAN NA PROF. ABDULRAHMAN BABU