Kisa kazi, mchumba wangu amenisaliti

Kisa kazi, mchumba wangu amenisaliti

Hicho kipengele cha mimba ndicho kidonge kichungu zaidi kumeza.

Hebu jaribu kuwaza mwanamke wako ambaye wewe unampa hadhi ya umalikia na cheo cha umakamo akitoka mama yako anaamua kwa utashi wake, kuanza mazoea na mwanaume mwingine tena kwa usiri. Anakubali kuwa karibu nae. Anakubali kupokea maneno ya ushawishi ya jamaa. Anaridhia kushawishika na anashawishika kwa maana kukubali jamaa aingie kwenye milango yake ya fahamu na kuanza kuwa na umuhimu.
🤣🤣 Jamaa akisoma hii anaeza lipuka
 
Nilikuwa na mwanamke toka shule mwishoni na hadi tukaenda kusoma vyuo tofauti yeye Dom na mimi Moro .mahusiano yaliendelea vizur alipofika mwaka wa 2 akabadilika nikafanya uchunguzi nikagundua anatoka na mwalimu nikampiga chini baadae majanga yakampata kumbe jamaaa alimvalisha hadi Pete ya uchumba yangu akavua at the end akaja kujua jamaa ameoa na ana watoto 2 tena ndoa ya kikursto akarudi kwangu analia nikasema No!! Akameza vidonge afe.mama yake anapiga cm analia nimsamehe mwanae atakufa nikasema no
 
Hicho kipengele cha mimba ndicho kidonge kichungu zaidi kumeza.

Hebu jaribu kuwaza mwanamke wako ambaye wewe unampa hadhi ya umalikia na cheo cha umakamo akitoka mama yako anaamua kwa utashi wake, kuanza mazoea na mwanaume mwingine tena kwa usiri. Anakubali kuwa karibu nae. Anakubali kupokea maneno ya ushawishi ya jamaa. Anaridhia kushawishika na anashawishika kwa maana kukubali jamaa aingie kwenye milango yake ya fahamu na kuanza kuwa na umuhimu.
Bro una talent ya kujaza mtu upepo.
 
Mjanja Wa Town
KWANZA POLE KWA YALIYOKUSIBU JAMAA YANGU ,

WANAWAKE WANA MAKUSUDI MENGI SANA NA WAKISHATIMIZA ADHMA YAO KWAKO KIKAMILIFU NDO HUKUONESHA MAKUCHA ,

JIULIZE KWANZA KAMA ALIKUBALI KULIWA TENA PEKU NA UJAUZITO AKAPATA NA KUUTOA UNADHANI WEWE UNA KIPI SPECIAL CHA KUMFANYA AKUPENDE ?

ANACHOJARIBU KUFANYA KWAKO NI KUKUHARIBIA MAISHA KWA NAMNA ANAVYOJUA YEYE NA HAPO NDO UTAPOTEZA DIRECTION NA KUWA MTU WA KAWAIDA SANA I SWEAR NAKWAMBIA,

JARIBU KUWA NA MSIMAMO THABITI WHEN U SAY NO U MEAN NO ACHA AVUNE ALICHOKIPANDA WEWE ANGALIA YAJAYO OTHERWISE UTAPOTEZA KILA KITU.........UTAKAPOPATA ANY STD's
 
Same experience, chuo kinawaharibu sana mademu. Wakiona Benz na Ist wanajua wamefika bila kujua hao wahuni wanawatumia tu wakishachoka wanawa dumb. Hapo hata angepiga simu bibi yake, hakuna cha msamaha.
Bro ni wanawa dump sio wanawadumb
 
Kuna watu wanapitia magumu.

Ingawa utamsamehe kwa kuona ni udhaifu ulimpitia lakini itakuja kubaki kwamba wee ni mnyonge..na mnyonge kwa kizungu ni COWARD
 
Kuna watu wanapitia magumu..
Ingawa utamsamehe kwa kuona ni udhaifu ulimpitia lakini itakuja kubaki kwamba wee ni mnyonge..na mnyonge kwa kizungu ni COWARD
100% kabisa
 
Hivi mtu wa dini ndo yupoje yupoje sielewi[emoji848][emoji848]


Mambo yasiwe mengi ACHANA NAE japo najua uweziii i[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Kila siku nasema uzinifu haujawai kumuacha mtu salama hata siku moja.angalia ndoa zenye migogoro lukuki chanzo ni uzinifu usio na mipaka.! Ushauri wangu tubu na huyo mwenzio alafu oa .mana huna pakwenda unaweza pata danga huyo ana afadhali.tatizo lenu ni uzinifu ndio umewapeleka huko.....

Sent from my vivo 1907 using JamiiForums mobile app
 
Poleni na majumukumu.

Mimi ni kijana wa miaka 29. Miaka kadhaa yuma nilipata nafasi ya kwenda kusoma nchi fulani. Huko nikakutana na binti mmoja tukaanzisha mahusiano.

Binti huyu ni yeye ndiye aliyenitafuta na kuonesha kuvutiwa na mimi. Hakuwa mrembo, ila alionekana ni mwenye imani ya dini sana na mpole. Wakati huo mimi nilikuwa playboy sina muda wala sikuwa in a relationship.

Siku tuliyokutana, mwaka 2015 nilimtembelea rafiki yangu katika mji mwingine wa nchi hiyo ndipo rafiki yangu akanitambulisha kwake. Alionekana kunichangamkia, uso wake ulijaa tabasamu alipoongea nami. Akamuaomba rafiki yangu aniachie namba yake ili tuwe tunawasiliana. Nilifanya hivyo, siku nasafiri kurudi kwangu, nikamtext kumuaga alifurahi akasave namba yangu.

Baada ya kufika kwangu, siku kadhaa mbeleni akaanza kunitafuta, akawa anaipigia simu hadi usiku, analazimisha tuongee masaa mengi, mm sikuwa mtu wa kuongea na simu masaa mengi. Basi ikaenda hivyo, ikafika siku akaniomba tuonane. Alitaka kunitumia nauli ya ndege nisafiri tuonane. Kutokana na ratiba zangu haikuwezekana. Zikapita siku, wiki, akaniambia anakuja kwenye mji wetu.

Kipindi hiko, mimi sikuwa na mpango nae, maana niliona kama hatuendani kwa sababu mimi nilikuwa bishoo tu, na yeye alionekana mtu mwenye kujiheshimu na aliyeshika imani ya dini ya kiislamu. Rafiki zangu, wakawa wananishawishi kuwa huyu mwanamke anakutaka, amefunga safari kwa ajili yako, malizana nae. Ukimuacha arudi kwao hivihivi utakuwa umekosea. Basi ikabidi tutoke dinner na mambo mengine yakaendelea. Hapo ndo ulikuwa mwanzo wa mahusiano yetu.

Kusema ukweli wa Mungu sikuwahi kupendwa before, kwa namna alivyonipenda huyu mwanamke. Alijitoa sana kwangu. Kila mtu alifahamu ni namna gani alinipenda. Mwanzo sikuwa na hisia nae lakini kutokana na upendo alionionesha, nikaona huruma kumuumiza. Ikabidi niachane na michepuko yote niingie kwenye serious relationship na yeye.

Baadhi ya watu walipiga vita mahusiano yetu. Walikuwa wakimuambia kuwa mimi nilikuwa namchezea tu, hatuendani. Ila hatukujali tukaendelea na mapenzi. Akawa ananiambia nimuoe sababu maisha ni yale yale na yupo tayari kuishi maisha yoyote na mimi. Japo mimi masikini lakini hajanipendea pesa. Tufunge ndoa tuishi kihalali. Basi kutokana na mapenzi yake, ikabidi nibadili mipango yangu sababu sikuwa nimewaza kuoa nikiwa chuo. Nikawapa taarifa wazazi wangu, mwanzoni walipinga ila baadae wakakubali. Nikamtambulisha nyumbani. Mimi sikuwahi kwenda kwao, ila nilikuwa najulikana.

Tukaanza process za uchumba, nikatoa mahari. Alifurahi sana. Mapenzi yalikuwa motomoto. Kila kitu kilienda sawa tukapanga kukirudi likizo nyumbani tufunge ndoa. Ila bahati mbaya au nzuri, dunia ikakumbwa na janga la covid19, mipaka ya nchi mbalimbali ikafungwa, hatukuweza kurudi likizo hivyo ikashindikana kutimiza azma yetu.

Tumedumu kwnye mahusano kwa zaidi ya miaka mitano. Mwaka jana, yeye alimaliza masomo yake, tukaagana. Mimi nilikuwa nimebakisha mwaka mmoja. Akarudi kwao, tukawa tunawasiliana, mapenzi yaliendelea, japo maisha yalibadilika financially sababu familia ziliathirika na janga la uviko. Mapenzi yaliendelea hadi hapo alipopata mchongo wa kazi.

Kuna siku alienda kugonga geti kwenye kampuni fulani, akaacha cv zake, akakutana na kijana mmoja muajiriwa wa hapo ambaye aliahidi kumsaidia kupata kazi. Alifurahi sana alinishirikisha vyote. Siku zikapita yule jamaa akamuambia arekebishe CV yake, akaniambia, mimi nikarekebisha kila kitu huku nikiwa na furaha japo nilikuwa na doubt. Sababu najua hakuna favour ya bure tu Dunia ya sasa. Nilimuonya mchumba wangu, nikamuambia awe makini. Ajaribu kuplay smart apate mchongo. Alinielewa basi michakato ya yeye kupata kazi ikaendelea.

Akaitwa kwenye interview, akapita na akapata kazi. Kipindi chote hiko alikuwa akinishirikisha kila kitu hadi conversations zake na huyo jamaa. Alimsifia kuwa ni mtu wa dini, na ni mwema sana. Baada ya muda kupita, akaanza kubadilika kuwa msiri. Akawa hainishirikishi tena mambo ya kazi. Akapunguza muda wa kunitafuta, nikimtafuta anasema yupo busy. Nikahisi kuna kitu kiaendelea baina yao. Nikawa kila nikimuuliza huwa anamtetea huyo mshkaji ma kusema ni mtu mwenye roho nzuri na amesaidia wengi. Basi tukawa tunagombana mara kwa mara, tunashuluhisha, anadai kazi zinabana, na mm sitaki kumuelewa. Ieleweke ameanza kazi miezi mitatu kabla ya mimi kurudi.

Basi kuna siku nikambana, akakiri kuwa alikuwa ananificha ni kwamba alikuwa alikuwa akikopwa hela na huyo jamaa ila hakunishirikisha, mara walikutana sehemu hakunishirikisha ila hakuna linaloendelea baina yao zaidi ya kazi. Basi mm nikasema ngoja nirudi maana hazijabaki siku nyingi.

Mungu si Asumani, nimerudi nyumbani salama, amekuja kunipokea airport. Mambo yakaenda fresh. Baada ya siku mbili nikiwa nae, naona texts zikiingia anaficha simu. Nikagundua anajaribu kunificha kitu. Baadae nachukua simu yake kusoma text, nakuta amefuta texts zote. Kumuuliza anababaika. Nikambana aniambie ukweli, nikamuambia akiniambia ukweli nitamsamehe na tutaendelea na mapenzi yetu.

Hapo ndo akakiri kuwa alianzisha mahusiano na yule jamaa, wakafanya hadi mambo yao bila kinga hata, na akapata na ujauzito ikabidi autoe. Kuumuliza why amenifanyia hivyi vyote after all we have been thru. Anasema eti jamaa alikuwa anatumia force, anamtishia kuwa atamuharibia kwa bosi na atakosa kazi. Hivyo hakuwa na jinsi.

Inavyoonekana ni kwamba jamaa alifanikiwa kumteka na kucontrol akili yake, so akawa anamtumia. Akakiri kuwa jamaa alimpiga hadi picha ya uchi akawa anamtishia ataisambaza kazini kote. Kiukweli niliishiwa nguvu, sikutegemea kama angeweza kufanya yote hayo. Kutokana na kunipenda sana, na kuwa mtu wa imani, ilipelekea mm kumuamini sana hapo kabla. Japo moja ya udhaifu wake aliokuwa nao muda mrefu ni kuamini watu kirahisi na huruma iliyopitiliza. Yani hata kuibiwa kwake ilikuwa rahisi sana.
Sijui hata nifanye nini kwa sasa.

Cha kushangaza after yote hayo, bado ananililia nimsamehe tuendelee na process za ndoa yetu. Anadai yupo tayari kuacha kazi. Mimi nimemuambia bora aniache, ili ibaki kuwa siri, nisimuharibie status yake Ila bado anasumbua. Amelia njiani na kupiga goti barabarani kiasi cha kuzua mshangao kwa wapita njia eti anaomba nimsamehe.

Kila mtu anafahamu kuhusu mahusiano yetu. Nashindwa jinsi gani ni-deal na hii situation. Cha kushanganza yote hayo yametokea within 3 months only. Naombeni ushauri wenu wakuu. Do you think this woman deserves forgiveness? What about familia yake, niwaambie kilichotoea wanirudishie mahari yangu au nifanyeje? Asanteni.
Tekeleza ulichoahidi, labda nikukumbushe, ulimwambia akikueleza kila kitu, utamsamehe na mtaendelea na mapenzi yenu. Sasa kama ulikuwa ukifanya mzaha, mwenzako hana mzaha!
 
PIGA CHINI.

Usijejaribu kuweka malengo kwa mwanamke mwenye huruma ambae tatizo dogo tu analialia kusaidiwa na wanaume huyo kuvua chupi ni jioni tu.

Huyo wako achana nae mkuu ashakutia doa kwenye hatua adhimu kabisa. Labda angekua teenager tungesema hajakomaa kiakili, sasa huyo yupo kazini kahisa na hadi mimba kaitoa. Ni alidhamiria kucheat, that means asingepata hiyo mimba na jamaa angeendelea kua nice kwake wewe ndo ungeachwa.

Na anakubebembeleza zaidi wewe kwakua kule kaharibu ko tegemezi ni wewe kumsitiri na hiyo aibu.

MKUU PIGA CHINI.
 
Back
Top Bottom